Mkuu wewe ulitamani kocha apangaje kikosi chake? Pacome na Azizi Ki ndio waliopo kwenye kikosi cha kwanza cha Gamondi, Chama kwenye mechi tough huwezi kuta kaanza lazima aanzie sub. Pengine mna muhukumu Pacome kwenye mechi dhidi ya Kagera, lakini mmeshindwa kuona wachezaji wote wa Yanga hawakucheza katika ubora wao. Kipindi cha kwanza Yanga ilipoteza nafasi nyingi sana za wazi. Kipindi cha pili timu ikapoteana kabisa. Binafsi sijaona kama Pacome kashuka kiwango, ndio naona ndiye mchezaji anayeifanya mpinzani aache mianya.