Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Uongozi wa klabu ya Yanga umemrejesha kikosini mshambuliaji wake Mcongomani David Molinga

Jana Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli alimtaja Molinga miongoni mwa wachezaji sita walioachwa

Hata hivyo nyota huyo aliyeifungia Yanga mabao manne kwenye ligi, amerejea leo na jioni ameshiriki mazoezi

Imefahamika kuwa Yanga imemrejesha Molinga baada ya kuachana na mpango wa kumsajili Owe Bonyanga nae kutoka DR Congo

Acha kutudanganya Molinga kagoma kuondoka[emoji16]
 
Duuh! Hivyo na wewe Mtani wataka kusema kwa ile mechi moja basi kocha wetu hafai kisha hajaanza na nyota njema? Uko siriazzz kweli Mtani?

Hizo methani kwa baadhi ya vitu zinakuwa sahihi kabisa ila kwa vitu vingine hapana kwa kweli Mtani hasa kama hiki tunachokiongelea Hapa.
Kijana anatumia nguvu nyingi kutulazimisha tumuone kocha wetu si mzuri. Aende akamchambue kocha wao kwanza. Au atuchambulie hapa tumsome
 
20200118_165220.jpg
NI SIKU NYINGINE TIMU YA WANANCHI IKO MAWINDONI KUZIWINDA POINTS 3.
 
20200118_165246.jpg

USAJILI MPYA

Anaitwa Erick Kabamba ni raia wa Zambia, amesajiliwa Yanga SC katika usajili huu wa dirisha dogo kwa mkataba wa miaka miwili . . anacheza wings zote 7 na 11! Amefanya majaribio kwa zaidi ya wiki mbili ameonesha uwezo mkubwa sana na kumpiku Owe Bonyanga.

KARIBU JANGWANI KABAMBA.

@Yangadaima.
 
20200118_165233.jpg

MORRISON AANZA MAZOEZI YANGA SC

Kiungo mshambuliaji mpya wa Yanga Bernard Morrison leo ameshiriki mazoezi kwa mara ya kwanza baada ya kusajiliwa na mabingwa hao wa kihistoria.

Morrison alipokewa kwa shangwe na wachezaji wenzake huku Molinga akiongoza shangwe la mapokezi ya winga huyo teleza.

Hakuna shaka ujio wake utaongeza zaidi makali ya safu ya ushambuliaji ambayo imesukwa upya.

Cc. Mtani Sapta Sapta. 😎😎😎
 
Aisee naona umekuja na nguvu mpya, nipe mtazamo wako unaonaje leo tutashinda kweli? Au tusubiri kunyweshwa juisi ya Ukwaju?

#Mechi35goli1
 
Back
Top Bottom