Makundi matatu ya viungo wazuiaji duniani. Kwanza kuna Destroyers, pili kuna Carriers na tatu kuna deep lying playmakers.
Destroyers ni watibuaji zaidi, wana uwezo mkubwa wa kukaba na kupora mipira. Carrier ni destroyer ambaye hakabi sana lakini ana uwezo kuisaidia timu kulinda kwa kutunza umbo la timu na kusambaza mipira.
Baada ya hapo yupo 'deep lying playmaker', huyu ni kiungo mzuiaji lakini hana uwezo mkubwa wa kupora mipira. Nguvu yake kubwa ipo kwenye kuchezesha. Deep lying playmakers wana uwezo wa kuchezesha kutokea nyuma.
Carlinhos anaangukia kundi hili la tatu. Ni deep lying playmaker. Uimara wake mkubwa upo kwenye kupiga na kutafuta njia za pasi. Si destroyer wala ball carrier.
Kwa maana hiyo ili umfaidi zaidi Carlinhos na kupata ubora wake inabidi umchezeshe kwenye timu inayomiliki sana mpira. Akusaidie kuchezesha kutokea nyuma.
Kwa bahati mbaya kumiliki siyo falsafa ya Yanga Afrika. Kucheza Mpira mwingi hakupo kwenye DNA ya Yanga Afrika hivyo kiungo kama do Carmo hana faida sana.
Kwa mpira wanaocheza Yanga Afrika, wanahitaji viungo wakabaji wagumu, watibuaji na wabeba mpira (Destroyers and Carriers) kama Tanombe Mukoko.
Kwangu mimi, si kwamba Carlinhos ana uwezo mdogo lakini mpira anaocheza na mpira wanaocheza Yanga Afrika havilandani.
Je Yanga Afrika wamepata pigo?? Hapana. Hajawahi kuwa mchezaji wa kutegemewa. Kwa upande mwingine wamefaidika. Kwanza gharama za kuvunja mkataba hazitakuwa juu yako, pili wanapata nafasi ya wazi ya kumtafuta mchezaji mzuri zaidi wa kigeni.
MY TAKE,
Kabla mchezaji hajasajiliwa ifanyike scouting ya kutosha kujua namna anavocheza. Takwimu tu na historia si kipimo sahihi cha kumfahamu mchezaji vizuri. Swali muhimu liwe, je uchezaji wake utaendana na falsafa yetu??
.
[emoji871]@deo_mwanasoka