Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

20191216_065943.jpg
 
YANGA IMEMALIZA ZIARA YAKE MKOANI KIGOMA

Jana Yanga imemaliza ziara yake mkoani Kigoma kibabe baada ya kuichapa Kigoma United mabao 3-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Lake Tanganyika

David Molinga 'Falcao' ndiye aliyekuwa shujaa wa mchezo huo akifunga mabao mawili huku bao jingine likiwekwa kambani na Mrisho Ngasa

Huo ni ushindi wa pili Yanga inapata mkoani Kigoma baada ya juzi kuichapa Namugongo Fc mabao 2-1

Mabingwa hao wa kihistoria wanarejea jijini Dar es salaam kuendelea na maandalizi ya mchezo wa kombe la FA dhidi ya Iringa United.
 
Uzi mrefu sana huu na watu si wengi ambao wanachangia wengi wanapita kimya kimya.
Ni kweli na sababu ya kutochangia ni haya mambo tunayoyasikia kwenye vyombo vya habari, mara leo kuna hiko mara kesho hiki, in short nadhani ndani ya timu bado kuna mambo hayapo sawa na ndo yanayotupa wasiwasi kila tukifikiria mstakabali wa hapo mbele itakuaje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli na sababu ya kutochangia ni haya mambo tunayoyasikia kwenye vyombo vya habari, mara leo kuna hiko mara kesho hiki, in short nadhani ndani ya timu bado kuna mambo hayapo sawa na ndo yanayotupa wasiwasi kila tukifikiria mstakabali wa hapo mbele itakuaje

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli kabisa Mkuu na inahitaji moyo wa chuma kuifuatilia Timu ya Wananchi hasa kipindi hiki mana ni zaidi ya kigumu.

Yaani kila kukicha kuna jipya. Ila yatakwisha siku moja.
 
Ni kweli na sababu ya kutochangia ni haya mambo tunayoyasikia kwenye vyombo vya habari, mara leo kuna hiko mara kesho hiki, in short nadhani ndani ya timu bado kuna mambo hayapo sawa na ndo yanayotupa wasiwasi kila tukifikiria mstakabali wa hapo mbele itakuaje

Sent using Jamii Forums mobile app
Twende tu na timu yetu,yatakwisha tu,naamini viongozi wanapambana sana kuokoa jahazi
 
LAMINE MORO MAMBO SAFI YANGA

Lamine Moro amerejea. Beki kisiki wa Yanga Sc Lamine Moro amerejea ndani ya kikosi cha mabingwa wa kihistoria Yanga na anatarajia kujiunga na kambi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kombe la shirikisho dhidi ya Iringa United pamoja na michezo ya ligi kuu Tanzania Bara

Aidha mdhamini wa Yanga @gsmtanzania amesema mashabiki wa Yanga wasiwe na hofu kuhusu usajili wa Dirisha dogo #GSM tumepania kuboresha kikosi cha @yangasc na kuwaahidi kwamba yanga wanayokwenda kuiona baada ya usajili wa Dirisha dogo siyo Yanga ile ambayo wameiona kwa kipindi kilichopita .

Pia Afisa Mhamasishaji wa Yanga @antonionugaz amesema Yanga siyo wanyonge tena tunakwenda kwenye hatua nyingine kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa pia amewapa dongo na kuwaeleza wapinzani wajiandae yanga itakuwa ya moto zaidi ya vile waijuavyo.

@yangafulldoz
 
MASHABIKI WATUPE USHIRIKIANO FURAHA INAREJEA JANGWANI 'MKWASA'

Kocha wa muda wa Yanga, Boniface Mkwasa ameridhishwa na jinsi ya wachezaji wake wanavyocheza kwa maelewano kitu ambacho ni kizuri amewataka mashabiki na wapenzi wa timu hiyo kukaa mkao wa kula.

Mkwasa anakaimu nafasi hiyo baada ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Mkongomani Mwinyi Zahera kutupiwa virago mwanzoni mwa mwezi uliopita.

Kocha huyo wazamani wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' amesema kadri siku zinavyozidi kwenda ndipo kikosi chake kinavyo imarika na wanatarajia kufanya vizuri katika mechi zinazo fuata. "Viwango vya wachezaji vinaimarika siku hadi siku ni jambo zuri, wachezaji wana morali na wanapokea vizuri mafunzo tunayo wapa, tunatarajia kufanya vizuri kwenye ligi na michuano ya FA iliyo mbele yetu," alisema Mkwasa.

Yanga inarejea leo jijiji Dar es Salaam kutoka mkoani Kigoma ilipokuwa na mechi mbili za kifariki dhidi ya Mwangungo FC walioshinda 2-1 na Kigoma Stars ambao waliibuka na ushindi wa mabao 3-0.
 
20191219_163501.jpg
RASMI NCHIMBI NI MALI YA YANGA

Uongozi wa klabu ya Azam umethibitisha kuwa umemalizana na Yanga juu ya usajili wa mshambuliaji Ditram Nchimbi aliyekuwa anacheza Polisi Tanzania kwa mkopo.

Nchimbi yupo nchini Uganda na kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania bara 'Kili Stars' kinacho shiriki michuano ya Cecafa Senior Challange.

Msemaji wa klabu hiyo, Jaffer Iddi amesema Yanga iliwaandikia barua juu kutaka huduma ya mshambuliaji huyo aliye kwenye kiwango bora kwa sasa na baada ya kumuuliza Nchimbi mwenyewe amewajibu yupo tayari kujiunga na mabingwa hao zamani wa Tanzania.

Jaffer ameongeza kuwa Nchimbi alikuwa amebakisha mkataba wa miezi sita na walikuwa na nia ya kumuongeza lakini baada ya mwenyewe kukubali kujiunga na Yanga na wamelipa kiasi walicho kubaliana wameamua kumuachia mchezaji huyo. "Sasa ni rasmi Ditram Nchimbi ni mchezaji halali wa Yanga, wametulipa pesa tuliyo kuwa tunaihitaji na mchezaji mwenyewe amekubali kujiunga na Yanga kwahiyo ni sasa ni mchezaji wao," alisema Jaffer.
 
20191219_165304.jpg
Jana Yanga imetambulisha usajili wa mlinzi wa kushoto Adeyum Saleh aliyetua kutoka klabu ya JKT Tanzania

Adeyum amesaini kandarasi ya miaka miwili kuwatumikia mabingwa hao wa kihistoria

Akizungumza katika hafla ya utambulisho wake uliofanyika Makao Makuu ya klabu ya Yanga, Afisa Mhamasishaji Antonio Nugaz amesema usajili wa Adeyum ni mapendekezo ya Kaimu Kocha Mkuu Charles Mkwasa "Tulikuwa na majina manne mezani katika nafasi ya beki wa kushoto. Kocha Mkwasa akampendekeza Adeyum kuwa ndiye aina ya mchezaji ambaye anahitajika Yanga kwa sasa," amesema


#MWANAJANGWANI
 
20191219_165829.jpg
Timu ya Wananchi Jumamosi hii itawakabili Iringa United uwanja wa Uhuru kombe la FA.
 
MAPINDUZI CUP KUFANYIKA BAADA YA MECHI YA WATANI

Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Zanzibar imeitangaza Kamati ya kusimamia Mashindano ya Kombe la Mapinduzi (Mapinduzi Cup) na tarehe ya kuanza Mashindano hayo ambayo ni sehemu ya maadhimisho ya Sherehe za miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Katika taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Wizara hiyo Omar Hassan Omar ‘King’ mashindano hayo yanatarajiwa kuanza January 5, 2020 na kumalizika January 13, 2020 ambapo jumla ya timu 8 zinatarajiwa kushiriki Mashindano hayo ambayo yatachezwa kwenye viwanja vya Gombani Kisiwani Pemba na Uwanja wa Amaan Kisiwani Unguja.

Katika timu 8 zitakazo shiriki Mashindano hayo 4 kutoka Zanzibar ambazo ni Zimamoto, Chipukizi, Jamhuri na Mlandege na 4 kutoka Tanzania bara ambazo ni Simba, Mtibwa, Yanga na Mabingwa watetezi Azam.

Mashindano hayo yamepangwa makundi mawili kundi A na B ambapo Kundi A kuna timu za Yanga, Jamhuri, Mlandege na Azam huku kundi B kuna Simba, Mtibwa, Chipukizi na Zimamoto.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kombe la Mapinduzi ni Sharifa Khamis Salim na Katibu wa Kamati hiyo ni Khamis Abdulla Said.

Wajumbe wa Kamati ni Khamis Mussa Omar, Issa Mlingoti, Seif Kombo Pandu, Mohamed Ali Hilali (Tedy), Aiman Othman Duwe, Fatma Hamad Rajab, Salum Ubwa Ali Khalil, Juma Mmanga na Suleiman Pandu Kweleza.
 
Back
Top Bottom