Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

20191222_083754.jpg
 
Lunyasi sisi ni wema sana, tunataka mje uwanjani mkiwa hamna kisingizio sijui cha hatuna kocha, hatuna mazoezi mara tumeng'atwa na nyuki ili kichapo kiwe cha halali na kiwaingie barabara mkiwa na akili zenu timamu na bila kushawishiwa wala kulazimishwa na mtu yeyote
We Jimwambafay tu Ses wakati zimebakia siku 12 pakachimbike Taifa.
 
Kwa mwili huo
Kwa mwili huo ulioumbika vyema Mashaallah pressure huwezi kua nayo ili hao Chuta FC unaowashabakia ndio wanakuweka katika hatari ya kupata mpressure sasa mamii, hivi huwezi kuachana nao?🙈🙈🙈
Daah!! Naachaje kuishabikia Yanga mimi. 🤔🤔🤔🤔

Wacha iniue. Mwenzangu huyu. 😅😅😅
 
YANGA KWENDA MBEYA JUMATATU

Kesho Jumatatu kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuelekea mkoani Mbeya tayari kwa michezo miwili ya ligi kuu dhidi ya Mbeya City na Tanzania Prisons

Keshokutwa Jumanne, Disemba 24 Yanga itacheza na Mbeya City katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Sokoine kisha kuwavaa Tanzania Prisons katka mchezo mwingine ambao utapigwa Disemba 27

Wanachama wa klabu ya Yanga mkoani Mbeya walikutana jana kuweka sawa mapokezi ya timu yao

Mkutano huo uliongozwa na Mwenyeki wa Mkoa Chuma Mahinya akiwa na mgeni kutoka Makao Makuu Saad Khimji ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji

Katika Mkutano huo, Wanachama walichanga pesa taslim Tzs 1,010,000/= huku kiasi cha Tzs 405,000/- zikiwa ahadi

Wanachama wa Matawi nao wamechanga Tzs 975,000/=
 
BALAMA:- YANGA IMENIONGEZEA KUJIAMINI

Kiungo anayekuja kasi Tanzania Mapinduzi Balama amesema usajili wake Yanga umekuwa na manufaa kwake.

Balama aliyesajiliwa na Yanga mwezi Juni akitokea klabu ya Alliance Fc, amesema ushiriki wake katika mechi za Kimataifa na kikosi cha Yanga umemuongezea kujiamini "Tangu nisajiliwe Yanga kutokana tumecheza mechi nyingi za Kimataifa, kwa kweli nimeongeza kujiamini" "Sasa hivi sihofiii kucheza mechi yoyote itakayokuja mbele yangu," amesema Balama.

Aidha kiungo huyo fundi amesema wanafahamu wanakabiliwa na michezo migumu mkoani Mbeya dhidi ya Mbeya City na Tanzania Prisons lakini wamefanya maandalizi ya kutosha hivyo wana matumaini ya kufanya vizuri.

Balama amekuwa na kiwango kizuri tangu alipojiunga na mabingwa hao wa kihistoria mwanzoni mwa msimu.

Nyota huyo anaunda safu ya kiungo ambayo itamjumuisha Haruna Niyonzima aliyesajiliwa hivi karibuni.

Papy Tshishimbi, Abdulaziz Makame, Mohammed Issa 'Banka', Feisal Salum, Raphael Daudi na Said Juma ni nyota wengine wanaounda safu hiyo.

@Yangadaima
 
Back
Top Bottom