Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

20191231_061539.jpg
 
Hivi hawa wapumbavu bado tu hawajakubali yaishe? Mbona nasikia walisainiana mkataba Wa kimangungo na Azam juu ya uhamisho wake Wa mkopo? Mana nasikia walikubaliana tu kwa mdomo kwamba aende polisi kwa mkopo Wa msimu mmoja na baadae azam wamewachenjia gia angani? Wametumwa hawa au!?
Haya sijajua aisee. Huenda wametumwa.

Mana Zengwe mbona halijaja toka muda ule aliposaini?

Ila tusubiri tuone mwisho wake Mkuu.
 
Mwinyi Zahera alitufanyia kitu mbaya sana! Kumuuza Makambo na kutuletea David Molinga! Mchezaji gani hana kabisa nguvu za miguu! Shuti lake utadhani ni la mtoto wa darasa la sita! Hana kabisa stamina. Aaaaaaaghhhh!!

Nina imani muda utakapowadia, Ditram Nchimbi na huyo Tariq nani sijui! watamchomesha mahindi mpaka aamue mwenyewe kuvunja mkataba na kurejea Congo.

Mkwasa ameanzisha viungo wanaocheza aina moja ya mchezo! Sijui lengo lake ni lipi. Mfano kuwaanzisha Kaseke, Ngasa na Sibomana. Kwa aina hii ya mfumo, kupata matokeo ni bahati nasibu. Aongeze mshambuliaji mwingine na kupunguza kiungo mmoja wa pembeni.

Mpira uko slow, hauvutii kabisa kwa wanajangwani.
Ujue hata na mie jana nilibaki kushangaa tu. Pia wachezaji hawana juhudi za kuhitaji matokeo.

Na ilisaidia alipoingia Tshishimbi na yule Mapinduzi angalau tukawa na uhai kidogo.

Sa sijui shida iko wapi kwa wachezaji? 🤔🤔
 
Back
Top Bottom