Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Ila benchi letu la ufundi ni la ajabu kweli sasa waliwapangia nini wakati tuna big match mbele. [emoji17][emoji17]

Nasikia na Tshishimbi pia eti naye si sehemu ya mchezo wa kesho kwani ana kadi tatu za njano. Sijui ni kweli?
Duuu asee Naomba tuishie hapo kwa hao wawili,ikiwa na tshishimbi mbona mikia watachekelea sana?. Ila kama unavyosema kuhusu hilo benchi,kiufundi lina matatizo, ndio mana nlisema Mkwasa anafaa kuwa kocha msaidizi na si Mkuu
 
KUKOSEKANA KWA LAMINE MORO SIO TATIZO
Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa kesho dhidi ya Simba licha ya kuwakosa Lamine Moro na Tariq Seif.

Moro anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano (mbili ligi na moja FA) wakati Tariq alipata majeraha kwenye mchezo dhidi ya Biashara United.

Hata hivyo Mkwasa amewahakikishia mashabiki wa Yanga kuwa kukosekana kwa wachezaji hao hakuwezi kuiathiri timu kwani wapo wachezaji wa kuchukua nafasi zao.

Huenda atawatumia Kelvin Yondani na Ally Mtoni au Andrew Vicent kama walinzi wa kati huku safu ya ushambuliaji akiwategemea David Molinga, Ditram Nchimbi na Yikpe Gnamien.
 
Duuu asee Naomba tuishie hapo kwa hao wawili,ikiwa na tshishimbi mbona mikia watachekelea sana?. Ila kama unavyosema kuhusu hilo benchi,kiufundi lina matatizo, ndio mana nlisema Mkwasa anafaa kuwa kocha msaidizi na si Mkuu
Mkwasa kaongea na waandishi wa habari kamtaja Moro peke yake huenda habari ya kukosekana kwa Tshishimbi si kweli Mkuu.
 
YIKPE GNAMIEN, NIYONZIMA RUHSA KUIVAA SIMBA KESHO

Nyota watano waliosajiliwa na Yanga kwenye usajili wa dirisha dogo wamepata vibali na wanaweza kushiriki mchezo dhidi ya Simba hapo kesho.

Baada ya kufanikiwa kupata leseni za wachezaji wazawa, Adeyum Saleh, Tariq Seif na Ditram Nchimbi, ITC za wachezaji wa kigeni Haruna Niyonzima na Yikpe Gnamien nazo zimewasili.

Kwa maana hiyo Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa kazi itabaki kwake kuamua nani aanze.

Ukimuondoa Niyonzima ambaye aliwasili jana, wachezaji wengine wamefanya mazoezi na timu kwa angalau wiki moja au zaidi hivyo wako tayari kwa mchezo huo.
 
Duuu asee Naomba tuishie hapo kwa hao wawili,ikiwa na tshishimbi mbona mikia watachekelea sana?. Ila kama unavyosema kuhusu hilo benchi,kiufundi lina matatizo, ndio mana nlisema Mkwasa anafaa kuwa kocha msaidizi na si Mkuu
Tusubiri tuone huyo Kaimu Meneja mpya atakuja na yepi.

Halafu nashangaa mwanzoni habari za kutafuta kocha mpya zilikuwa moto moto ila ghafla zimekuwa tulii.

Watutafutiage Kocha bwana.
 
20200103_182658.jpg
 
YIKPE GNAMIEN, NIYONZIMA RUHSA KUIVAA SIMBA KESHO

Nyota watano waliosajiliwa na Yanga kwenye usajili wa dirisha dogo wamepata vibali na wanaweza kushiriki mchezo dhidi ya Simba hapo kesho.

Baada ya kufanikiwa kupata leseni za wachezaji wazawa, Adeyum Saleh, Tariq Seif na Ditram Nchimbi, ITC za wachezaji wa kigeni Haruna Niyonzima na Yikpe Gnamien nazo zimewasili.

Kwa maana hiyo Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa kazi itabaki kwake kuamua nani aanze.

Ukimuondoa Niyonzima ambaye aliwasili jana, wachezaji wengine wamefanya mazoezi na timu kwa angalau wiki moja au zaidi hivyo wako tayari kwa mchezo huo.
Hapo kwa Yirpe angalau hatutakuwa na shortage ya strikers. Na mie nlitamani aanze Yirpe badala ya molinga
 
Japo nawaza 🤔🤔🤔 ataweza kuwa na muunganiko na wenzake.

Mana hana muda mrefu kwenye timu na hajawahi kucheza mechi hata moja.

Nionavyo kwa upande wangu awekwe sub ili awe anausoma mchezo akiwa benchi.
 
Back
Top Bottom