Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

SASA KUMEKUCHA

Napenda kuwafahamisha ya kuwa, siku ya Jumanne saa kumi jioni wachezaji wote wa @yangasc wataripoti Uwanja wa Mazoezi kwa ajili ya Vipimo mbalimbali kama Uzito, Covid19, Malaria, Glucometer-Kupima Sukari Mwilini etc na maelekezo mbalimbali jinsi ya kujikinga na Covid19.

AIDHA tumemualika Dr Marealle Mjumbe wa Kudumu wa Kamati ya Tiba CAF na Mjumbe wa Kamati ya Tiba TFF! kuja kutoa darasa kwa ufupi kwa vijana wetu kuhusu Covid 19.

Mwenyekiti wa Klabu pamoja na Wadhamini wetu watapata wasaa wa kuzungumza na wachezaji kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo michezo yetu iliyobaki na maana yake kwa timu yetu!

Hakutakuwa na Ruhusa kwa yeyote kuingia Uwanjani kwenye Mazoezi ya Timu Kwa ajili ya Uzingativu wa Maelekezo ya Serikali yetu.

TUMEKUJA KIVINGINE TUTAELEWANA TU.

DEO MUTTA
KATIBU
KAMATI YA MASHIDANO
YANGA.
Tunashukuru kwa taarifa

The only thing to fear is fear itself
 
SASA KUMEKUCHA

Napenda kuwafahamisha ya kuwa, siku ya Jumanne saa kumi jioni wachezaji wote wa @yangasc wataripoti Uwanja wa Mazoezi kwa ajili ya Vipimo mbalimbali kama Uzito, Covid19, Malaria, Glucometer-Kupima Sukari Mwilini etc na maelekezo mbalimbali jinsi ya kujikinga na Covid19.

AIDHA tumemualika Dr Marealle Mjumbe wa Kudumu wa Kamati ya Tiba CAF na Mjumbe wa Kamati ya Tiba TFF! kuja kutoa darasa kwa ufupi kwa vijana wetu kuhusu Covid 19.

Mwenyekiti wa Klabu pamoja na Wadhamini wetu watapata wasaa wa kuzungumza na wachezaji kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo michezo yetu iliyobaki na maana yake kwa timu yetu!

Hakutakuwa na Ruhusa kwa yeyote kuingia Uwanjani kwenye Mazoezi ya Timu Kwa ajili ya Uzingativu wa Maelekezo ya Serikali yetu.

TUMEKUJA KIVINGINE TUTAELEWANA TU.

DEO MUTTA
KATIBU
KAMATI YA MASHIDANO
YANGA.

Uwanja wa mazoez wa kwenu au mnaenda kwenye uwanja wa shule[emoji3]
 
Hahah mkipangwa na sisi ndoto zenu za kushiriki mashindano ya kimataifa zitafutika

The only thing to fear is fear itself
Woooiii!! Nadhani unaijua Timu ya wananchi ile iliyokusapuraizzz mechi mbili ya nje na ndan hivyo ombea usipangwe na sisi mana hutatamani ubingwa wa Vpl kwani utakuwa unamajeraha kibao.
 
Woooiii!! Nadhani unaijua Timu ya wananchi ile iliyokusapuraizzz mechi mbili ya nje na ndan hivyo ombea usipangwe na sisi mana hutatamani ubingwa wa Vpl kwani utakuwa unamajeraha kibao.
Hahah hayo mambo yenu ya dharau yatawatokea puani safari hii shauri yenu

The only thing to fear is fear itself
 
KLABU ya Yanga imesema wiki hii, watasaini ushirikiano wa kazi na mshauri wa La Liga, Carraca Antonio ambaye atasaidia kuwashauri juu ya njia sahihi kutekeleza mabadiliko.

Yanga wanakaribia kuanza safari ya mabadiliko ili iweze kufanya kazi kwa njia yenye faida kwa kukumbatia mfumo wa uendeshaji wa uwekezaji.

Akizungumza, Ofisa mwamasishaji wa klabu hiyo, Antonio Nugaz alisema wakisaini mkataba, wataanza rasmi mabadiliko.

Hii inakuja baada ya klabu kufanya utafiti wa kina juu ya nani mshauri ambaye anaweza kusaidia kuiongoza timu hiyo kwenye ustawi wa kiuchumi na kuifanya kuwa moja ya klabu za ushindani kwenye barani Afrika. “Kwa kuzingatia hili, tulimchagua La Liga kuwa mshauri, tunaamini kwamba ana sifa zinazotufanya kufika mbali kwenye mabadiliko,” alisema Nugaz.

Pia alitoa wito kwa mashabiki na wanachama kutoa ushirikiano uongozi ili ndoto za kuibadilisha Yanga zifanikiwe kwa urahisi. “Vitu vingi vitaathiriwa tunapokwenda kwenye mabadiliko katika suala la usimamizi wa klabu, idara ya masoko na idara zingine pia. “Wote tufanye kazi kwa kushirikiana Mwenyekiti wetu Mshindo Msolla ili tufike katika nchi iliyoahidiwa kwa urahisi na kuruhusu michakato ianze mapema,” alisema Nugaz.

Hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Msolla alianzisha agenda ya ‘Twende Kwenye Mabadiliko’ ambayo alisema kuwa ni hatua ya kwanza kufikia kilele cha mabadiliko ya klabu. “Moja ya ahadi zangu wakati wa kipindi cha kampeni ni Yanga kuelekea mabadiliko na kuiwezesha kujiendesha kwa njia ya kisasa. Ndoto hiyo imefikiwa polepole ndio sababu tunahitaji kuwa pamoja katika mchakato mzima.

“Nimefurahi tumeanza msingi wa kufanikisha jambo hili kubwa katika historia ya klabu yetu na tutaendelea kuihabarisha familia ya Yanga kila hatua tunayofanya kupitia Azam TV na Yanga TV,” alisema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Habari ya klabu hiyo, Hassan Bumbuli aliwahakikishia wana Yanga nchini kwamba watajumuishwa katika mchakato mzima wa mabadiliko. “Tutakuwa tunawahabarisha kila hatua tuliyofikia kwa sasa tunangojea kusaini rasmi mkataba na mshauri wa La Liga ambaye atatusaidia katika mchakato wote wa mabadiliko.”
 
Mkuu wa benchi la ufundi la Young Africans, Luc Eymael amesema kama mambo yatakwenda kama anavyotarajia, kikosi chake kitakua na sura ya kutisha kuanzia msimu ujao wa ligi kuu ya soka Tanzania bara.

Eymael ametamba kwa kujiamini kwamba, akili yake kwa sasa ipo kwenye ushambuliaji na winga zote mbili katika usajili mpya.

Kocha huyo kutoka nchini Ubelgiji ameshamalizana na baadhi ya wachezaji na anashukuru kwamba, uongozi chini ya udhamini wa GSM wanakwenda kasi katika kuhakikisha mapendekezo ya wataalamu wa benchi la ufundi yanafanyiwa kazi.

Akizungumza moja kwa moja kutoka Ubelgiji alipo kwa sasa, Eymael amesema anataka timu yenye kasi na watu wa kazi ambayo hata straika aina ya Bernard Morrison awe anasota kupata namba kwenye kikosi cha kwanza.

Pia, amesema hata mchezaji anapokosekana kikosi basi hakuna pengo kutokana na waliopo kuwa na uwezo wa kuziba nafasi hiyo na mashabiki wanafurahi.

Alisema anamhitaji pia kiraka Mbelgiji, Andrea Fileccia anayechezea klabu ya ridhaa ya daraja la kwanza nchini humo ya Royal Francs Borains. “Nataka kuwa na wigo mpana hasa kule mbele, yaani aliyeko ndani na aliyeko benchi wote wawe na ubora stahiki wenye hadhi ya kuichezea Yanga. “Huyu Andrea ni kama Morrison makali yake, lakini yeye ana uwezo wa kucheza hadi nafasi ya mshambuliaji wa kati. Huyu sehemu ni Morrison na sehemu ni Nchimbi,” alisema akimaanisha kwamba, anaweza kucheza pembeni na katikati, ana asisti na kufunga.

Eymael alisema akipata saini za washambuliaji na mawinga wa kigeni kutoka DR Congo, Ghana na Rwanda aliowapendekeza pamoja na wale wazawa, basi Young Africans itakuwa moto kweli kweli. “Nikiwa na Morrison (Benard), Nchimbi (Ditram) na wengine wapya, ninataka kuwa na kikosi bora ambacho kitakuwa kinapata matokeo mazuri kila mechi,” alisisitiza Eymael.

Mpaka sasa Young Africans ina uhakika wa kuwapa mastaa wawili kutoka DR Congo kwenye ushambuliaji ambao ni Tuisila Kishinda wa AS Vita na Mpiana Mozizi wa FC Lupopo.

Kocha huyo amesisitiza msimu huu wakirejea uwanjani amepanga kuukamilisha kwa heshima ya aina yake kwa vile nafasi yao ya ubingwa ni finyu, lakini akili zao zipo kwenye kombe la FA.

Anasema kwamba lazima wabebe FA.

@Yangafulldozz
 
Mshambuliaji wa Yanga Ditram Nchimbi amesema atatumia mechi zilizobaki kujiimarisha kwenye kikosi cha kocha Luc Eymael.

Nchimbi maarufu kama 'Duma', amesema amefuata ipasavyo program ya mazoezi aliyoachiwa na kocha hivyo yuko tayari kuuwasha moto pale ligi itakaporejea
Akiwa mmoja wa nyota wa kutegemewa kwenye kikosi cha Yanga, Nchimbi amesema pamoja na wachezaji wengine, watahakikisha wanamaliza msimu kwa kishindo

"Binafsi nimekuwa nikifanya mazoezi kujiweka sawa, nimefuata program ya Mwalimu hivyo nimefurahi ligi kurejea na niko tayari kwa asilimia 100," alisema
Nchimbi ni mmoja wa wachezaji ambao wamejihakikishia namba kwenye kikosi cha Eymael akiwa na uhakika wa kuendelea kukipiga na mabingwa hao wa kihistoria licha ya ujio wa nyota kibao wanaotarajiwa kusajiliwa dirisha la usajili litakapofunguliwa.

@Yangafulldozz.
 
Back
Top Bottom