Shadeeya
JF-Expert Member
- Mar 12, 2014
- 49,759
- 118,798
Uongozi wa Yanga umesema kocha mkuu wa timu hiyo Luc Eymael ambaye aliwasili jana, atawahi mkoani Shinyanga kuungana na timu kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mwadui Fc ambao utapigwa Jumamosi ijayo
Muda mfupi baada ya kuwasili, Eymael alieleza kuwakumbuka wachezaji pamoja na majukumu yake katika kikosi cha Yanga
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema timu hiyo inaandaa utaratibu wa kumuwezesha kocha huyo aweze kufika mkoani Shinyanga kwa wakati
Eymael huenda akaambatana na nyota waliobaki jijini Dar es salaam ambao jana hawakusafiri na timu hiyo kutokana na sababu mbalimbali
Nyota hao ni Bernard Morrison, Metacha Mnata na David Molinga ambaye alidai hakujumuishwa katika msafara.