Feisal is Too Overratted! Kuna sifa nyingi anapewa kwa kudanganywa. Sijui ni bahati mbaya au ni kwa makusudi, Watu wameamua kumdanganya FeiToto
Hii haimjengi. Itamdumaza na mwisho wa siku ataishia kukumbukwa kama kiungo mwenye kipaji kikubwa aliyevuma Yanga na kumaliza soka lake Simba
Ni kama ilivyokuwa hadithi ya Chuji na Boban. Ilianza kwa kusisimua, ikaisha kwa kukera. Nani alijali?
Tusisubiri Feisal achelewe. Bado tuna wakati wa kumshauri na kumwambia ukweli
Si kwa faida yake tu, ni kwa Faida ya maendeleo ya mpira wetu kwa ujumla. Fei ana kipaji kikubwa sana lakini inaonekana hana Jitihada za kupush standard yake
Nimeirudia tena kuitazama kuitazama mechi ya Yanga Vs Prison.. Kwa makini sana
Mashabiki wanaamini Feisal alicheza vyema sana. Ukiwauliza Kwanini? Watakwambia alificha sana mpira.. Alipiga turn za kutosha na pasi za vibao... Basi!
Hamna aliyewaza 'turn' zake zilikuwa na athari gani kwa Timu
Dhidi ya Prison, Feitoto amepiga square pass (Pasi za pembeni) nyingi kuliko pasi za mbele. Sio Takwimu nzuri kwa Kiungo mshambuliaji
Katika pasi 47 alizopiga na kufika, nyingi amegongeana na Kaseke na Zawadi Mauya
Attacking Midfielder anatakiwa kuwa na akili ya kushambulia. Idadi ya pasi zake nyingi ziwe zinatafuta mikimbio ya mastraika na mawinga
Na kwenye soka la kisasa, ili uwe na quality hizo ni Lazima uwe fiti kweli kweli
Sio akili pekee, inakulazimu uwe na mapafu yaliojaa pumzi na mwili unaonyumbulika
Kiungo wa kisasa anafika haraka kwenye nafasi ya kupokea mpira na kugeuka haraka kupunguza eneo la kiwanja kwa hatua za kwenda mbele
Feisal ana struggle kuutuma mwili wake. Ana cover eneo dogo la kiwanja! Hii inamfanya ashindwe kutengeneza au kuattack spaces nyingi mbele ya lango la mpinzani
Feisal anatakiwa aongezee bidii mazoezini. Asiishie kuiamini akili yake pekee! Kwa mpira wa kisasa, Eneo analocheza linahitaji watu wenye Energy sana
Naamini kipaji chake. Naamini pia ana nafasi ya kuimprove zaidi. Tusiendelee kumdanganya Feisal
Lile eneo analocheza, Shiboub alikuwa na Assist 6 na Mabao 2 licha ya kucheza dakika 900 tu msimu Uliopita.. Na bado akaonekana Si Lolote!