Afisa habari wa Klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli, amesema klabu ya Simba inatakiwa pia iwakemee mashabiki wake pale wanapoenda kutazama mechi za Yanga wasiende kwa lengo la kuwakera na kuwakejeli mashabiki wa Yanga kwa sababu kejeli siku zote hazivumiliki lazima mtu atapaniki.
Bumbuli amesema pia klabu ya Simba inatakiwa pia iwakemee mashabiki wake kuachana na kauli za kusema wanaenda kuangalia mechi za Yanga kwa lengo la kuhakikisha Yanga inafungwa huo unakuwa ni uvunjifu wa amani, kwa sababu hata mtu anapokuja kwako na kukuambia atahakikisha wewe haulali vyema na familia yako hautomchukulia vizuri sababu atakuwa na Nia mbaya na familia yako.
#Sportarena