Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Kupata kimbwanga kama hiki tuma neno Shadeeya kwenda namba 99623. Ahsante
Kimbwanga hicho kwiiio.
IMG-20191204-WA0001.jpg
 
Niliona sura za injinia na bosi zinatia huruma, hata hawaamini kabsa kama hii ndio yanga![emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Ujue bana kikawaida raha na hata nyuso kuwa na furaha ni kuona bao zinaingia huku likichezwa soka la uhakika sasa ikiwa namna ile lazima roho ziwapae hasa wakikumbuka mahela yao waliyoyamwaga.

Tulicheza lakini kiwango kilikuwa si kile nilichokizowea.
 
Mshambuliaji wa zamani wa Yanga Amissi Tambwe ameupongeza uongozi wa mabingwa hao wa kihistoria kwa kumuajiri Cedric Kaze kuwa kocha mkuu wa timu hiyo

Tambwe aliyewahi kuitumikia Vital'o ya Burundi wakati Kaze akiinoa klabu ya Atletico ya nchini humo, amesema anamfahamu kocha huyo, anafundisha soka la chinichini

Aidha Tambwe amesema ni muhimu kwa Wanayanga kutompa presha kocha huyo ili aweze kuunda timu imara ambayo ana uhakika itafanya vizuri

"Kaze ni kocha mzuri kutokana na jinsi ninavyomjua tangu zamani wakati nacheza Vital’O hapa Bujumbura, yeye alikuwa akifundisha Atletico, kweli timu yake ilikuwa inacheza mpira wa chini wenye pasi nyingi," alisema Tambwe

"Nadhani labda kitu ambacho kinaweza kusumbua ni hizo presha za hapo Tanzania, Lakini nje ya hapo Kaze ni kocha mzuri, anafundisha mpira wa chini siyo wa kutupa tupa yaani ule wa kubutua butua naamini atawasaidia sana Yanga kwa kuifanya icheze mpira mzuri, wapinzani wanatakiwa kujiweka sawa kweli"

Kaze aliondoka Burundi mwaka 2012 kuelekea kule nchini Ujerumani ambapo alipata mafunzo ya juu ya ukocha na akapata nafasi ya kufanya kazi na timu ya Taifa ya Ujerumani

Baadae akapata fursa ya kuwa mkufunzi katika Academy za Fc Barcelona, akifanya kazi hiyo Ujerumani na Canada

Amewahi kuinoa timu ya Taifa ya Burundi ambapo mwaka 2012 alichaguliwa kuwa kocha bora wa CECAFA

Wanayanga wanasubiri ujio wake, taarifa zimebainisha kuwa Kaze anatarajiwa kuondoka nchini Canada kesho Jumatatu au Jumanne na huenda akawasili nchini siku ya Alhamisi
 
Amis is our legend!
 
Back
Top Bottom