Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Huo ndio ukweli na wanajua mashabiki wengi wa yanga hatuwez kifikiri

Ikifuatilia hili sakata toka siku za mwanzo kabisa yule mnayemuita Eng Hersi alisema kila kitu ashamaliza tusiwe na hofu

Siku zilivyozid kwenda wachezaj wengne wanatambulishwa watu wakaanza kuhoj mbona Djuma Shaban hatambulishwi akajibu kuwa msiwe na waswas

Muda umefka wanaanza kutengeneza drama nyingi na majibu yasyo na uhalisia wowote

Kifup yanga hakuna mchezaj tuliyevunj mkataba kutoka nje tulochofanya n kuvizia wale ambao hawafai na timu zao huko na sisi tumewachukua

Mwaka wa 3 huu wanatoka wachezaj lundo tunaingiza lundo la wachezaj hiv jaman kwa utaratibu huu muunganiko utoke wapi hapo?

Makocha ndio usiseme wantimuliwa kila siku na ajabu wakamleta NABI ambaye kizungu hajui kiswahil hajui na wanajua kabisa weng was wachezaj wetu wanajua kiswahili angalau na kiingereza

Leo Dr mshindo msolwa akitaka kuongea na kocha anahitaj mkaliman na yeye ndio waongee kweli jaman hapo kuna shida mahali kwa yanga

Kuna Mahal nimesoma NCHIMBI anasema hamwelewi kocha huko mazoezn kwasababu ya lugha

Sababu ya kuona lugha n shida wakaona watujazie wachezaj wanaoongea kifaransa kutoka kongo ili kupata wakaliman

SAIDO NTOBANZOKIZA yupo yanga kwsababu ya mpira au ya ukalimani
maana hili nalo linahitaj mjadala mwingine kabisa

GSM yupo yanga kwa interest zake na si kuisaidia yanga kama tunavyoaminishwa

Tunaambiwa mechi za CAFCL hazina mashabiki lakn wao wanachangisha nauli watu waende huko NIGERIA swal la kujiuliza wanaenda kutembea au kufanya nn maana mashabiki hawaruhusiwi huko Kama timing Haina nauli ya kukod ndege so waseme tuchangie


SIUONI MWISHO MZURI WA TIMU YANGU

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Undeni kwanza mfumo rasmi wa kuendesha timu, Kisha rudini mezani mtengeneze Mambo yenu. Sasa hivi hapo klabuni ni Kama kila mtu anasharubu Kama familia ya kambare.

Simba huwa mnaibeza na mo wake, lkn muda utafika mtaelewa na kukubali mfumo mpya wa Simba!
 
Mkuu kiukwel hii timu naona Kama viongoz wamefika ukomo wa kufikiri mkuu

Sasa unawaambia watu wakate tiketi za ndege halafu tunajua viwanjan hawaruhusiwi mashabiki HUONI KAMA HUU N WIZI KABISA MKUU

Unaambiwa mwenyekiti wa klabu hana nguvu kabisa yupoyupo tu

Msolwa ukimchunguza Sana hata uongeaji wake n Kama ana MTINDIO WA UBONGO VILE hayupo sawa yule jamaa

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
[emoji3][emoji3]Mwenyekiti sijawahi kuelewa wala kumkubali. Kwanza huwa Naamini ni mwana Simba yule!. Kiujumla viongozi wanaendesha mambo bila weledi kabisa kiasi kwamba wanaabisha utu wao Na nafasi zao!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Undeni kwanza mfumo rasmi wa kuendesha timu, Kisha rudini mezani mtengeneze Mambo yenu. Sasa hivi hapo klabuni ni Kama kila mtu anasharubu Kama familia ya kambare.

Simba huwa mnaibeza na mo wake, lkn muda utafika mtaelewa na kukubali mfumo mpya wa Simba!
Na wewe unavyoshauri tuunde mfumo rasmi utadhani ninyi mna mfumo rasmi![emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Wawakilishi Wetu Kimataifa Kumbukeni Kazi Bado Haijaisha-Michezoni leo​


KAZI inaendelea kwa sasa hasa kwa timu ambazo zinaiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya kimataifa.

Tanzania Bara tunazo timu nne na hii ni fursa kubwa ambayo inabidi ilindwe na kila timu kwa sasa ili na wakati ujao tupeleke timu nne pia kwani ni heshima na furaha kwa Tanzania kuwa na timu nyingi ambazo zinaipeperusha bendera ya nchi hii.

Ukianza kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, kuna Azam FC na Biashara United, hizi zote zimeanza kwa ushindi kwenye mechi zao za awali.

Ni Azam FC, hawa walikuwa nyumbani pale Uwanja wa Azam Complex, Dar na waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Horseed FC ya Somalia. Biashara United wanaojiita Wanajeshi wa Mpakani, kazi yao ilikuwa dhidi ya FC Dikhil ya Djibouti.

Ushindi wa bao 1-0 ugenini bado haimaanishi kwamba kazi imekwisha, ukurasa bado unaendelea kufunguka na muhimu kwa kila mchezaji kujua kwamba kazi ipo palepale.

Mchezo wa pili ni zaidi ya fainali kwa kuwa mwisho zina hukumu nani ataendelea mbele na nani atapewa mkono wa shukrani aendelee na maisha mengine katika hatua ya awali.

Ipo wazi kwamba wawakilishi wetu kwenye Kombe la Shirikisho Afrika mnastahili pongezi lakini hamstahili kujisahau kwa kuwa kazi bado ipo kusaka ushindi kwenye mechi za marudiano.

Ukiwatazama Azam FC watakuwa nyumbani kwa mara nyingine licha ya kwamba ule mchezo wa awali uliochezwa Azam Complex wao watakuwa ni wageni.

Ikumbukwe kwamba mchezo wa pili nao utakuwa na ushindani kama ilivyo kwa wenyeji namna wanavyosaka ushindi. Kwenye mchezo wa kwanza, Azam FC ilianza kwa kuruhusu bao, lakini ikajipanga vema na kushinda, hivyo inapaswa kuongeza umakini katika mchezo wa pili.

Biashara wana jukumu la kuongeza juhudi kwenye mchezo wao wa marudiano pia ili kuweza kulinda ushindi ambao ulipata awali kule ugenini.

Ukiweka kando na hawa wanaowakilisha nchi kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, Yanga na Simba hawa wapo kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga imeanza kwa kuchechemea mchezo wa awali baada ya kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Rivers United ya Nigeria, kumbukeni kazi bado haijaisha.

Mchezo wa pili ni muhimu kwa Yanga kufanya maboresho kwa yale ambayo waliyafanya mchezo wa awali, inawezekana kama wageni waliweza kushinda hapa Tanzania basi na Yanga inawezekana kushinda Nigeria.

Kikubwa ni maandalizi na kila mmoja kuweza kutimiza majukumu yake kwa wakati. Kwenye mpira kila kitu kinawezekana, kikubwa ni maandalizi mazuri na nidhamu katika utendaji wa kazi.

Simba hawa hawataanza hatua ya awali kwa kuwa waliweza kufanya vizuri msimu uliopita baada ya kutinga hatua ya robo fainali ndani ya michuano hii.

Kwa hatua ambayo waliifikia msimu uliopita hapa wana kazi nyingine ya kufanya ili kuweza kupata ushindi kwenye mechi watakazocheza ili waweze kufika mbali zaidi.
 
Uto mnataarifa,Air Tanzania imekosea kutua huko,badala ya kutua Nigeria ikatua Guinei kwa kanali Mamady Boumbouya.huu ni uchawi uliozidi mipaka kwa hawa Rivers,Utopolo zidisheni dua.
 
Hahaha
IMG-20210917-WA0039.jpg
 
Back
Top Bottom