Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Leo 23/12/2023 tunakipiga na Tabora United hii ndo game yetu ya mwisho mwaka huu Kwa upande wa NBC PREMIER LEAGUE...
Hii timu ni mpya kwenye na hatujawahi kucheza nayo by the way ni timu inayopitia misukosuko mingi ya kufungiwa kusajili wachezaji kutokana na madeni mengi kutokana na kuvunja kiholela mikataba na wachezaji wao wa zamani....

Leo tunahitaji ushindi mkubwa kama zawadi ya Xmas lakini pia kujiweka kwenye position nzuri ya kutetea ubingwa wetu...

Natamani kumuona Clement Mzize akipewa nafasi na Gamondi I hope he gonna perform well...

All the best wananchiiiiiiiiiiiiiiiii [emoji91]
IMG_20231223_073539.jpg
 
Leo 23/12/2023 tunakipiga na Tabora United hii ndo game yetu ya mwisho mwaka huu Kwa upande wa NBC PREMIER LEAGUE...
Hii timu ni mpya kwenye na hatujawahi kucheza nayo by the way ni timu inayopitia misukosuko mingi ya kufungiwa kusajili wachezaji kutokana na madeni mengi kutokana na kuvunja kiholela mikataba na wachezaji wao wa zamani....

Leo tunahitaji ushindi mkubwa kama zawadi ya Xmas lakini pia kujiweka kwenye position nzuri ya kutetea ubingwa wetu...

Natamani kumuona Clement Mzize akipewa nafasi na Gamondi I hope he gonna perform well...

All the best wananchiiiiiiiiiiiiiiiii [emoji91]View attachment 2850364
Nmeota goli 7
 
Kama kawaida Timu ya Wananchi tumejiimarisha kileleni.
View attachment 2851071
Naam Tupo nafasi ya pili tukiwa na point zetu 30 na michezo 11 point moja nyuma ya Kinara Azam FC yenye Point 31 na michezo 13....

Hapo ukiangalia Kwa wastani ni kama kila game tulipata point 2.7 ambayo ni approximately to point 3.! Bila kusahau jumla kumefunga magoli 31 na tukiruhusu 6 Tu... Gamondi ana balaa nyie na hapo anadai bado hajaipata Ile Yanga anayoitaka [emoji28]

Ukimuangalia mpinzani wetu Azam FC yeye Kwa wastani amevuna pointi 2.3 Kwa kila game...
Msimu huu Azam ni wa Moto kwenye upande wa kupachika magoli kwani ndie kinara akiwa na Goli 35 huku yeye karuhusu bao 10....

Anyway kila goti litapigwa za ndaaaaaaaani kabisa kuna Forward moja huyo anakuja dirisha hili dogo ana balaa
Wapinzani wetu watakua wanakuja na huku wamefunga vitambaa vyeusi maana itakua ni msiba kila mechi [emoji2]
 
leo hatuchezi babu..?
 
Mkuu kukazia ako kaparagraph ka mwisho ni kuwa wajiandae kulia kila game. 😀
 
Hapana NBC PREMIER LEAGUE league itarudi baada ya michuano ya AFCON kuisha so simply itakua na mwezi wa pili....
Tifuatifua na bodi wamevilea viporo kwa kuahirisha mechi ambazo timu zingecheza, mfano ya Mikia FC vs Azam Nov 28.
 
Jaman mm Kuna shida sizioni picha zinazotupiwa humu

Nifanye Nini kuziona
 
Hizi Ndo Moment Bora Zaidi 2023 Kwa Dar Young Africa Nakazozikumbuka Daima..

5. Azam 0 Yanga 1 tr 12/06

Zikiwa zimepita siku 9 tu Tangu tutoke kucheza Fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika... Yanga tulikua tunapitia kipindi kigumu kutokana na mrundikano wa mechi kwani baada ya kucheza game ya fainali na USM Alger tr 3/6 tulicheza game nyingine tr 6/6 dhidi ya Mbeya City, tukacheza tena tr 9/6 dhidi ya Tanzania Prisons....

Hii game iliikuta Yanga ikiwa Hoi kwani ndani ya siku kumi na mbili tulitakiwa kucheza game nne ngumu Sana.. Mbaya zaidi kwenye hii game striker nyota Fiston kalala Mayele hakua Fit kucheza hivo kulikua na Presha kua huenda Yanga atakutana na kichapo cha mbwa koko kutoka Kwa Azam...

Lakini game ilipoanza Azam walizidiwa sana, Kwani Yanga ilitandaza soka Safi kichizi kiasi kwamba wachezaji wa Azam walitamani wapewe tochi ili wamulike kuutafuta mpira [emoji28]... Shukurani Kwa Superstar wetu Kennedy Musonda Kwa Bao lake Safi lililotupa kombe la FA Kwa mara ya pili mfululizo....

4. USM Alger 0 Yanga 1 tr 3/06

Baada ya fainali ya Kwanza iliyochezwa may 28 jijini Dar es Salaam kutuacha na simanzi wanayanga baada ya kuchezea kichapo kutoka Kwa USM Alger sasa ilikua fainali ya mkondo wa pili wengi waliitabiria Yanga kichapo kikali huko Uarabuni lakini siku ya game mambo yalikua tofauti Yanga walicheza mpira wa kiwango cha dunia hadi wapinzani wakaanza kufanya fujo....

Hii game ilituacha na simanzi Kwa kukosa kombe hilo muhimu sana kiasi cha kumtoa machozi aliyekua kocha wetu mkuu Professor Nabi...

Wataalamu wa maswala meusi waliianza kumlaumu mtani Kwa kufanya ulozi wa mvua kwenye mechi ya awali eti ndio ilikua sababu ya kupoteza Ile game hivo ilitakiwa aje kulipa kwa kupewa adhabu kali kwa yale aliyoyatenda.. (nitasimulia huko mbele au basi [emoji16])

3. Ihefu 2 Yanga 1 tr 4/10

Ilianza kama utani siku kadhaa kabla ya game wasioitakia mema Yanga walitabiri Yanga atapigwa na Ihefu kutokana na kufungwa na timu hiyo msimu uliopita.... Hatimaye siku ya hukumu ikafika.. ilikua dakika ya nne tu ya mchezo ambapo Pacome Zouzoua alipokea pasi Safi toka Kwa under 20 Clement Mzize na kuiandikia Yanga bao la kwanza... Kumbe tulikua tomekojolea upele..

Ihefu waliamaka na kucheza soka Safi na kushinda Bao mbili na nchi yote ikawa chungu Kwa mashibiki ya Yanga kumbuka tulikua tumetoka kufuzu makundi ya CAF champions League baada ya kusota Kwa miaka mingi, furaha yote ikageuka karaha.

Kwa mara ya Kwanza nilihisi kumchukia Gamondi [emoji1787]

2. Yanga 1 Al ahly 1 tr 2/12

Kama Yanga angepoteza hii game huenda tungepoteza kila kitu.. maana upande wa pili wangeongea hadi tufe pia tungeonekana si lolote si chochote kwenye michuano ya champions League.....

Kumbuka Al ahly ndo walitangulia kupata Goli tena dakika ya 86 yaani dakika za lala salama aisee kuna watu walishangilia hadi wakavunja viti.. lakini Mungu fundi Kupitia Kwa Pacome Zouzoua dakika ya 91 aliisawazisha walau mji ukapoa...

Watu tulikua tunawaza tutatokaje Banda umiza [emoji2]

1. Simba 1 Yanga 5 tr 5/11

Kama ungekua umelala halafu ukaamka na kufungua Livescore ili upate matokeo huenda usingeamini kile ulichokiona... Naam sitaki kusema mengi lakini hii ndo game Bora Sana kwangu mara nyingi nikiwa Banda umiza hua sishangilii lakini hii siku nilipiga kelele Sana Hadi nikajishangaa...

Baada ya kuwafunga JKT na KMC Goli tano kuna mwandishii alimuuliza msemaji wa Simba Ahmed Ally kua Yanga wanadai wamezitunza Goli tano Kwa ajili Yao ... Lakini Ahmed Ally alihoji Tu Kwa dharau "yaani Sisi tufungwe tano?" Lakini kilichotokea kimeacha mgogoro mzito mzito mitaa ya Msimbazi [emoji23]

Supu day na bango mjini Kati ilikua sehemu ya kuuenzi huu ushindi maana ilikua ni adhabu Kwa uchawi wao uliotunyima kombe Kwa mwarabu! Anyway niwatakie heri ya mwaka mpya 2024... Naamini Yanga itaendelea kutupa good and bad moment but all in all
#Daimambelenyumamwiko

[emoji169][emoji172]
 
Jaman mm Kuna shida sizioni picha zinazotupiwa humu

Nifanye Nini kuziona
Jaribu njia hii. Gusa hayo maandishi chini ya picha, itaingia kivuli. Juu kulia kutatokea vidoto vitatu, gusa hivyo vidoto. Chagua kwa kugusa open in browser.
 
Back
Top Bottom