Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

EXCLUSIVE 4 - Nabi: Nililia kwa ajili ya Yanga, mama, Rais Samia

mwanaspoti.co.tzFeb 16, 2024 2:30 PM

Mechi zipo mfululizo sana ligi ya hapa inachezwa wiki nzima, hakuna nafasi ya kutoa muda wa wachezaji kupumzika vizuri, nakubaliana na kwamba kuna wakati wiki moja ndani ya mwezi mkacheza katikati ya wiki lakini isiwe wiki zote ndani ya mwezi wachezaji wanaumia sana na sisi makocha tunakuwa katika wakati mgumu pia.

“Kuna wakati nilikumbana na adhabu ya kufungiwa hili nalo liliniumiza baadhi wa waamuzi nadhani wanatakiwa kujifunza lugha sio kila wakati mtu akiwa mkali kwako basi amekutolea lugha chafu, mimi ni mtu ninayejua kuwaheshimu wengine, sisi sote tunafanya kazi zinazotofautiana kidogo sio rahisi kwangu kumtukana mtu mwingine ni vigumu sana.

“Baadhi ya waamuzi wamekuwa wakifanya makosa yanayoumiza sana kuna vitu vya wazi sana walikuwa wanashindwa kuvitolea uamuzi unapolalamika anakutoa kwa kadi nyekundu wakati wote ambao waliniadhibu walinionea lakini nimewasamehe hakuna shida.

MECHI ZA MAKUNDI

“Tulipocheza mechi za hatua ya makundi hatukuanza vizuri tulitangulia kupoteza dhidi ya US Monastir, mechi ile iliniumiza kwa kuwa ile ndio timu ninayoipenda kutioka kwetu, nilitamani niwafunge ili kupeleka ujumbe kwao kuwa mtoto waliyenilea nimekuwa lakini haikuwa hivyo.

“Baada ya hapo tuliona mapungufu yetu tukabadilika na hata wachezaji waliazimia kubadilika kwenye mechi iliyofuatia dhidi ya TP Mazembe, tulibadilisha pia mifumo kutoka ule wa 4-2-3-1 na baadaye tukatumia 4-3-3 hapa ndipo tulianzia safari ya kushinda mechi zilizosalia, bahati mbaya sana tulipata sare ya ugenini kwenye mchezo ambao ilitakiwa tushinde.

Baada ya mechi za makundi kidogo tulibadilika na kuanza kuangalia mpango wa kucheza mechi kwa mechi lakini hapa tulitumia nguvu kubwa kwenye kuwachambua wapinzani ambao tulikuwa tunakutana nao, ilikuwa hatua nzuri kwa klabu kumleta Khalili (Ben Youssef) ambaye alifanya kazi kubwa tukishirikiana na sisi wengine ambaye alikuwa anatupa mwanga mkubwa wa kipi cha kufanya katika timu tulizokutana nazo.

HAKUSHANGAA YANGA KUTINGA FAINALI

"Tulipomaliza mechi za robo fainali na kisha nusu fainali siku shangaa kuona tunacheza fainali tayari kama kocha niliona kuna nafasi ya kucheza fainali lakini ilihitajika nguvu kubwa ya kuandaa timu ili hilo likamilike na kweli tukafika.

"Hapo nilianza kufikiria kwamba itakuwa vyema na heshima kwa klabu hii na Tanzania kwa ujumla tukichukua taji kwa kuwa hatukuwa kwenye eneo la kushindwa kupambana na USM Alger, kazi kubwa tuliifanya kuwandaa wachezaji kisaikolojia unajua sio wachezaji ambao waliwahi kufika ngazi hiyo kazi ambayo tuliona tumefanikiwa.

"Nilifanya kazi na Hersi katika sura mbili kwanza kabla ya kuwa Rais na baada ya kuwa Rais kusema ukweli huyu ni kijana ambaye ameyatoa maisha yake kwa ajili ya Yanga, nitawaambia sababu, kuna sajili ngumu ambazo zimefanyika hapa kama angekuwa ni ambaye hana mapenzi na Yanga asingehangaika lakini Hersi amekuwa kama mwanajeshi wakati wowote yuko tayari kuipigania Yanga.

"Hata baada ya kuwa rais maisha yake yamekuwa hayohayo, sisi tuliokuwa kwenye timu tunajua presha ya Hersi tunapokuwa tunakwenda kucheza mechi ngumu, kuna wakati anakuwa mkali kupitiliza lakini nilikuwa namuelewa kwa kuwa hata mimi hunitokea kuwa mkali kwa wachezaji pale ninapoona mambo hayaendi sawasawa.

"Sio Hersi peke yake na kamati yake ya utendaji angalia maisha ya Arafat (Haji makamu wa rais) naye ni mtu wa aina hiyohiyo ni watu wanaojituma bila kuchoka na wajumbe wao wa kamati ya utendaji, chini yao kuna Andre (Mtine Afisa mtendaji mkuu) naye ni mtu mwenye busara na aliyenyooka amekuwa msaada mkubwa kwangu.

"Naweza kusema huu ni uongozi ambao wanachama na mashabiki wa Yanga wanatakiwa kujivunia bahati nzuri wengi ni vijana hata kama watakuja kufanya makosa nani amekamilika chini ya jua? sisi sote tunaweza kufanya makosa jambo zuri kuna mazuri mengi wanafanya hebu angalia kwa umri wao mdogo wameiwezesha klabu kucheza fainali ya CAF kwangu ni uongozi ambao nitaukumbuka kwa wakati wote ambao nilifanya nao kazi.

"Pia nimshukuru Dk Msolla ambaye nilimkuta hapa na watu ambao pia niliwakuta walinipa ushirikiano mkubwa mpaka wanaondoka madarakani, alikuwa msaada kwangu alikuwa akiona kitu hakipo sawa anakufuata kesho yake na kukushauri.

"Kwenye klabu nyingi ambazo nimefundisha naweza kusema huu ni uongozi mzuri nadhani kama watampa ushirikiano kama huu kocha anayekuja basi Yanga itaendelea kufanya vizuri, kuondoka kwangu sitaki kuwa adui wa klabu hii na watu wake niko tayari kutoa ushirikiano wowote pale watakapohitaji mimi ni mwananchi kabisa

AWATOA WASIWASI MASHABIKI

"Najua mashabiki hawakufurahi kuondoka kwangu lakini nawaomba wanisamehe lakini niwaambie ni Nabi anandoka klabu kubwa kama hii wamepita makocha wengi lakini bado maisha ya mafanikio yalikuja, timu ipo bahati nzuri kila kinachotakiwa kuboreshwa kinajulikana hakutakuwa na shida kuendeleza mazuri haya ambayo nayaacha nyuma kwa jinsi ninavyoziona hesabu za viongozi wa Yanga naiona bado Yanga itaendelea kuwa klabu ya mataji zaidi.

C&P
 
Na hii ndio ingekuwa dawa. Hivi kwani game yenyewe saa ngapi?
Viongozi wa Yanga wamechemka sana kupenda kucheza mechi saa moja. Hawajui kupanga mambo kimkakati, wangeomba wacheze hata saa kumi. Waarabu wamezoea kucheza mechi zao usiku hivyo ingewapa tabu ile joto la mchana. Tungepanga mkakati wa kumariza biashara ya kufuzu mapema kabisa kwa kuhakikisha timu inapata goli nne
 
Viongozi wa Yanga wamechemka sana kupenda kucheza mechi saa moja. Hawajui kupanga mambo kimkakati, wangeomba wacheze hata saa kumi. Waarabu wamezoea kucheza mechi zao usiku hivyo ingewapa tabu ile joto la mchana. Tungepanga mkakati wa kumariza biashara ya kufuzu mapema kabisa kwa kuhakikisha timu inapata goli nne
Kweli kabisa.
 
Ingekuwa mbinu nzuri,sema CAF ndiyo uruhusu mechi ichezwe muda fulani kulingana vigezo vyao.
Hapana mkuu sio hivyo, swala la muda lipo chini ya wenyeji wenyewe (TFF na Yanga)
 

Attachments

  • IMG_20240219_222146.jpg
    IMG_20240219_222146.jpg
    273.2 KB · Views: 8
Wapi Yanga imetajwa kwenye hicho kifungu? Huu ni uchuro wa TFF peke yake.
Hapo imetajwa host association ambapo kwa Tanzania ni TFF. Na TFF kazi yake kubwa ni kupeleka taarifa CAF na sio kupanga. Yanga wanaweza kuamua mechi yao ya CAF ichezwe popote pale ili mradi uwanja ukidhi vigezo vya CAF kiubora.
Na ndio maana unaona TP Mazembe au timu yeyote kutoka nje inaamua kupeleka uwanja nje ya nchini mwao mfano uwanja wa Mkapa au Azam au Al Mereikh alipeleka mechi yao Rwanda. Au unakumbuka mechi ya Yanga vs Pyramids ilivyopelekwa CCM kirumba?
TFF hawawezi kupanga muda na uwanja pasipo wao Yanga wenyewe kukubali.
 
Wapi Yanga imetajwa kwenye hicho kifungu? Huu ni uchuro wa TFF peke yake.
Hapana mkuu sio hivyo, swala la muda lipo chini ya wenyeji wenyewe (TFF na Yanga)
Wakuu mbona kwenye ile press ya juzi kuelekea hii mechi ya jumamosi Ally Kamwe alisema mwenye kupanga muda wa mechi ichezwe saa ngani ni wenye mashindano yao yaani CAF wenyewe.

Au na yeye katupiga kamba.
 
Wakuu mbona kwenye ile press ya juzi kuelekea hii mechi ya jumamosi Ally Kamwe alisema mwenye kupanga muda wa mechi ichezwe saa ngani ni wenye mashindano yao yaani CAF wenyewe.

Au na yeye katupiga kamba.
Hizi ni sheria za mashindano ya CAF champions league, ukisoma kipengele namba 10 kinaelezea juu ya siku ya mechi, uwanja na muda wa mechi. Ally Kamwe huenda kaongea vile ili tuone hawakuwa na mamlaka kwenye hilo hivyo hawana cha kulaumiwa au pengine hajui sheria za CAF champions league.
 

Attachments

Huyo ni Ally Kamwe ila hii hapa chini ni sheria ya CAF inavyosema. Sasa je Ally Kamwe anataka kusema sheria za CAF ni za uongo?
Hapa kilichopo Mkuu huyo Kamwe huenda hazijui sheria za CAF kama usemavyo au kama anazijua basi kwa mawazo yake anajua mashabiki walio wengi hatujui hizo sheria za CAF.

Ila mwisho wa siku hamna namna kwa kuwa wao ndo wameshaamua hivyo.
 
Back
Top Bottom