Monsignor
JF-Expert Member
- Jan 29, 2009
- 523
- 14
asalaaam aleykum kandambili wote.... ninawapa pole kwa kuwakosa wakongo lakini nategemea yule beki wa malawi hamtampanga tena..
Mimi sina huruma na Yebo yebo kabisa. Hawana moyo wa kiuana michezo kabisa. Walivyoona timu yao mdebwedo inakamuliwa wakaamu ku-hack JF ilitusiwashushue. Belo na Balatanda acheni kushabikia maradhi. Wachezaji wana njaa watacheza vipi?
Wachezaji Yanga walia njaa
Monday, 15 February 2010 04:16 *Uongozi kujadili kipigo leo
Na Mwandishi Wetu
BAADHI ya wachezaji wa timu ya Yanga, wameulalamikia uongozi wa klabu hiyo kwa kuwacheleweshea mishahara yao ya Januari, huku wakiwa hawana taarifa zozote juu ya mishahara hiyo ambayo wao wanaitegemea kwa matumizi mbalimbali.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Dar es Salaam jana na kuomba majina yao yahifadhiwe, wachezaji hao walisema wanashangaa kuona mpaka wanacheza mchezo wao wa kwanza katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika, bila kulipwa mshahara wa Januari jambo ambalo linawatia wasiwasi na kuwavunja moyo.
''Huwezi kuamini mpaka sasa, hatujalipwa mishahara yetu ya Januari, alafu jambo la kushangaza viongozi wanachozungumza hatukielewi, sasa mimi naona ni bora watuambie moja hatma ya fedha zetu, kama kukopa tuanze kukopa,'' alilalamika mmoja wa wachezaji hao.
Aliendelea kusema kwamba licha ya kuwa walituambia wangetupa kabla ya kuanza kwa michuano hiyo ya kimataifa, lakini wanashangaa siku zinakwenda bila kupewa taarifa zozote, kitu kinachowanyima raha kila wakirudi nyumbani kwani wao wanafamilia zinazowategemea.
Akizungumzia sakata hilo Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Lawrance Mwalusako alikiri kwamba ni kweli mshahara wa Januari, hawajawapa wachezaji wao lakini tayari kila kitu kipo vizuri na kuanzia leo huo mchakato wa kuwalipa fedha zao utaanza.
''Ni kweli mshahara wa Januari hatujawalipa wachezaji wetu hadi sasa, lakini tulikubaliana kwamba tutawapa mishahara hiyo baada ya kumalizika kwa mchezo wetu dhidi ya Lupopo ambao tayari tumeshacheza, hivyo kuanzia kesho (leo) tutaanza kuwapa mishahara yao,'' alisema Mwalusako.
Wakati huo huo, Mwalusako alisema leo Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo, inatarajia kukutana na benchi la ufundi, kujadili na kupanga mikakati ya mchezo wao wa marudiano dhidi ya FC Lupopo, utakaopigwa wiki mbili zijazo nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC).
Alisema watakutana kujadili ni vipi walipoteza mchezo huo wa kwanza kwa kuangalia makosa yao na kujipanga upya, pamoja na kupanga mikakati ya kuaminika katika kuhakikisha wanaingia hatua ya pili ya michuano hiyo.