Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Yanga 3 Lupopo 2

Zimeongezwa dakika 30 Kandambili Wanashambulia kama Mancity teh teh teh

Jameni acha utani tupe matokeo ya mechi hata kama hayatatufurahisha!! Naona hata BBC Sports bado hawaweka results!!!

Tiba
 
Kwa sasa ni half time naburudika na Bolingo hapa Yanga 1 Lupopo 0 goal scored by Jerrison Tegete

Mfukunyuzi inabidi Uwaombe Radhi Mashabiki wa Kandambili kwa Kuleta Matokeo Kinyumenyume

Hadi Mwisho wa Mchezo

Lupopo 1 Kandambili 0

Eti wanasingizia JOTO kali
 
Afadhali umeua mzizi wa fitna manake tulikuwa tunachanganyikiwa tu na baadhi ya posts. Haya kanda 2 rudini home manake ninyi mnaalergy na ligi za kikubwa lol
 
Afadhali umeua mzizi wa fitna manake tulikuwa tunachanganyikiwa tu na baadhi ya posts. Haya kanda 2 rudini home manake ninyi mnaalergy na ligi za kikubwa lol

Mkuu Nimeona Nivunje Ukimya baada ya Kuona wenye Sredi hawaleti Matokeo
 
Kitendawili watani?
"Kuti likwanyukapo katu halivyai mani, Kuti mpe hata mkwezi alipandishe, Kuti likanyukapo katu halivyai mani'
 
yanga bwana wanatufurahiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiisha na utumbo wao
hivi kusumbuka kote huko mpaka nchi yenye vita ile walikuwa wanafuata nini?
si wangebaki tu bongo wakisubiri mkono au mguu wa simba udondoke waokote ubingwa??

teh teh halafu kwenye first post ya hii thread wanajiita timu yenye mafanikio zaidi tanzania,mafanikio ya ligi ya ndani tu?kama ubingwa huwa manunua tutajueje?

mbona mkitoka nje ya tanzania au mkishindanishwa na timu za nje mwachemsha vibaya?je timu iliyotwaa mara nyingi kombe la tusker,kombe la cecafa(kagame),timu bora ya karne ya tanzania kwa mujibu wa FAT MWAIJUA NYIE MABAHAU WA KANDAMBILI?

RUDINI BONGO MJE MNUNUE MECHI ZA JKT NA MANYEMA NDO KAZI MNAYOWEZA
 
nawapongeza saaana yanga kwa kuchutama na kupewa kamoja tu, maana hali haikuwa bora sana
 
Haya tena, rudini home muwafunge Toto 6-0 mfadhili afurahi!
 
Sinkala vipi hiyo avatar hapo na mkulu invisible?
 
YANGA inatua Dar es Salaam leo saa 12.40 jioni lakini kocha wake mkuu Kosta Papic amefunua moyo wake na kuweka bayana mambo matatu yaliyoitoa Yanga kwenye ligi ya mabingwa.

Yanga ilifungwa bao 1-0 na FC Lupopo katika mechi ya marudiano iliyofanyika Jumamosi Stade de Kenya mjini hapa.

Mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya Bara walihitaji ushindi wa mabao 2-0 kusonga mbele kutokana na kufungwa mabao 3-2 katika mchezo wa awali jijini Dar es Salaam. Yanga imetolewa kwa jumla ya mabao 4-2.

Papic amesema kuwa kuna mambo matatu yameiponza timu yake ambayo ni uwanja mbovu, hali ya hewa pamoja na matokeo ya Dar es Salaam.

"Kiufundi hapa timu ilikuwa vizuri kabisa muda wote kuliko mechi yoyote tuliyowahi kucheza, lakini uwanja umetuharibia mbinu zetu umejaa maji na matope unateleza tu kila mara."

"Wachezaji walipokuwa wanapanga mashambulizi kwa kasi lazima mmoja wao alikuwa anaanguka na kutoa faida kwa mwenyeji ambaye anaonekana kuzoea hii hali kwahiyo tukawa tunatumia nguvu kubwa sana.

"Ilifika wakati kukawa hakuna ufundi mpira unapigwa tu mbele kutafuta matokeo kutokana na hali ya uwanja, kama ulikuwa mkavu kama Dar es Salaam tungebadilisha matokeo."

"Mambo mengine yaliyotuharibia ni kufungwa Dar es Salaam pamoja na hali ya hewa ya hapa ni mazingira mageni.

Timu yangu imeondolewa kwenye mashindano pale Dar es Salaam siyo hapa, Lubumbashi imecheza sana," alisema Papic.
Yanga ambayo wachezaji wake saba wa timu ya Taifa waliwasili Dar es Salaam jana, inaondoka hapa leo saa 5.15 asubuhi na kutua Nairobi saa 10.25 na saa 11.25 itaondoka na kuwasili Dar es Salaam saa 12.40 na ndege ya Shirika la Ndege la Kenya, KQ 424.
 
yanga bwana wanafurahisha kweli,wanasingizia uwanja mbovu mbona sasa walipigwa hapahapa kwenye uwanja bora barani afrika kusini mwa jangwa la sahara na kaskazini ya afrika kusini?visingizio kila siku si waseme lupopo yalikuwa maji marefu?
 
Papic popote ulipo!! sisi watanzania visingizio hivi tumeshavisikia tumechoka!! kama uwanja mbovu kwani Lupopo walikua wanacheza wakiwa hewani?

Matokeo ya Dar? Hii sio sababu labda ungetupo sababu ya kupata matokeo mabuvu Dar, usiseme ulifungwa kwasababu ya matokeo ya Dar.
KUMBE HATA WEWE NI WALE WALE TU!
ENDELEA KUTOA DOZI KWA TOTO AFRICA (6-0)
 
mmmmh Papic kamba hizo, kwani Lupopo ndio wamezoea kucheza kwenye matope?

kama Lupopo wamezoea kucheza matopeni mbona walitundandika shamba la bibi ambalo tuliwafunga Toto Afrika bao 6.
 
Yanga haina wachezaji wa kuweza kuifunga LUPOPO full stop.
Yanga haina mazoezi ya kisasa
Yanga inaongozwa kizamani mno
YANGA FUKUZA WANACHAMA WOTE . HAWANA MANUFAA KWA KLABU. YANGA UZA HISA KLABU IWE NA WATU WENYE PESA WANAOWEZA KULETA MABADILIKO KM WENZETU ULAYA NA SI KUTEGEMEA WANACHAMA WALE TUNAOWAONA WAMECHOKA NAMNA ILE.
Papic, hakuna lolote utakalo achieve kwenye ligi hii ya Bongo ambako ligi inashirikisha timu ambazo ni matawi ya timu nyingine(Mfano Yanga-Toto Africa). Sana sasa Mh. Paic unazidi shusha CV yako.
Wachezaji wetu hawana malengo, wanacheza tu mpira kwa kutaka umaarufu au kupata mademu mtaani.

Mpaka hapa wana YANGA tusitegemee miujiza huo ndo ukweli, TIMU YETU HAIWEZI ACHIEVE CHOCHOTE NJE YA NCHI, mtachukua ubingwa hapa hata miaka mia lkn mkinusa nje ya nchi BAOOOOOOOOOOOOOOOOOOO tu.
 
Papic amesema kuwa kuna mambo matatu yameiponza timu yake ambayo ni uwanja mbovu, hali ya hewa pamoja na matokeo ya Dar es Salaam.
Na mambo gani yaliyoponza mpaka matokeo ya Dar es Salaam yakawa hivyo? Sababu zitatolewa kwa mtindo wa backwards hadi mchawi apatikane !!
 
Back
Top Bottom