Kumekuwa na mabadiliko makubwa sana katika views za wasanii wetu huko youtube baada ya bei za mabando kupanda bei, kwa sasa kinachoendelea nje ya mipaka yetu inaonekana kwamba muziki wetu umekosa mvuto kwasababu views zimepungua sana, Hakuna video iliyofikia hata views milioni 1 na nusu tangu bei zipande.
Ikumbukwe ya kwamba moja kati ya sababu kubwa zilizofanya mziki wetu ufike mbali ni kwamba wasanii wetu walipata attention kubwa sana katika platfors maarufu ya Youtube kwa kigezo cha views, hiki kigezo kilifanya hata tv na radio za bje kucheza muziki wetu, waandaaji wa tuzo kama bet na afrimma nao walitupia jichi huku bongo kwasababu internet ya gharama nafuu iligeuka kuwa silaha kubwa sana ya kuwapaisha wasanii wetu hata nje ya mipaka
gharama nafuu ndizo zilifanya wasanii wetu kuwepo kwenye list ya wasanii wa Africa wenye subscribers wengi, Msanii kama Diamond aliwea rekodi ya video zake zote za youtube kupata views bilioni, n.k. haya mambo yalikuwa yanafanya tufatiliwe hata na nchi nyingine
Views milioni ambazo huku kwetu hata msanii wa kawaida alizipataa, zilikuwa zinatamaniwa sana na wasanii wa nchi nyingi sana kiasi kwamba wengi walivuka mipaka kuja huku kwetu kuomba collabo.
Views hazikuwa ujivuni pekee, views ni pesa, msanii akiruhusu kuwe na tangazo kabla video yake haijaanza huwa kuna pesa analipwa na youtube, malipo haya yaliwapa motisha wasanii wetu kurekodi miziki katika studio nzuri na kugharamia vizuri video zao huku wakiwa na uhakika wakurudisha baadhi ya gharama ama kupata faida kabisa,
kwa sasa ni dhahiri na wazi kabisa wa Nigeria wanagonga cheers maana tumejiharibia sisi wenyewe