Yuko wapi Rais Magufuli? Msiache tetesi zienee. Kama anaumwa mnasema "ANAUMWA"

Status
Not open for further replies.
Rais wetu yupo wapi? msilete mchezo tutakwenda mahamani kudai tujue yupo wapi ati - tuna haki hiyo kikatiba kujua where about ya rais wetu.
 
Hakuna aliyesema tusichukue tahadhari. Tunachosema ni kumtanguliza Mungu mbele na tahadhari nyingine zote zinafuata nyuma! Na utukufu wote apewe Bwana Mungu.
Usijitoe ufahamu unaweza toa hiari ya kuchukua tahadhari kwenye kupambana na janga? acha kubadili kauli ,kiburi kitawaumbua
 
Mpaka wewe umesema, hakika wamekuudhi na umewachoka.
Mficha Maradhi, Mungu ampe afya njema
 
Yeyote akiugua ni bahati mbaya! Ukweli ni kwamba kwa mazingira yetu, hakuna mwenye uwezo wa kuchukua tahadhari kama inavyotakiwa! Hali na mazingira haviruhusu, ndio maana tunamtanguliza Mungu!
Last time wakati tunaambiwa Mungu alituponya which is right tahadhari zilicukuliwa kama zote ko ilikuwa maombi na tahadhari lakini saizi imeachwa kuwa hiari na maneno ya kejeri juu.

Mungu asisingiziwe kwenye uzembe,mbona mipaka haijafungwa licha ya kuambiwa kuwa mdudu wa sasa ni hatari kuliko wa awali,siwezi kutetea ujinga hata kidogo.

Mnachotakiwa kujua ni kwamba watu wenye maisha ya ahueni ndio wako hatarini zaidi kuliko maskini
 
Mike sonko na Raila odinga pia wamelazwa nairobi hospital kama sikosei ndiyo hospital aliyokuwa amelazwa Tundu lissu
Mkuu kama ni kweli basi Lissu ametonywa na jamaa zake hapo Nairobi ,lakini pia hiyo hospitali ya Nairobi imeizidi kiasi hicho Muhimbili jamani hii ni ngumu kumeza labda S.A
 
Aaaah kumbe kwa vile hajaonekana hadharani BASI mnazua Rais anaumwa, nyie VIPI? Huyu ni Rais na ana kazi nyingi na hana ulazima wa kuonekana hadharani eti tu kwa sababu ni mazoea! Asipoonekana, basi mnazua ya kuzua, eti anaumwa. Hivi kweli Rais hawezi kukaa na kufanya kazi za kiofisi na asionekane hadharani? Kwenu hilo ni KOSA, na tayari mtazua anaumwa, mara hivi, mara vile ili mradi mkamate mawazo na fikra za watu kwa nia na lengo la kuleta taharuki. Hiyo ndiyo mbinu mpya mliokuja nayo this time around baada ya kukosa hoja za nguvu. Mshindwe!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…