Ugonjwa ni jambo la kawaida,hakuna binadamu ambaye anaweza kuishi bila kuumwa.so ikiwa mh. kweli anaumwa nilitegemea kuwa pamoja na kumuombea uzima.cha ajabu watu wanashangilia!so sad for Tanzanians.hii jf iko worldwide si pati picha tunasomekaje nje ya mipaka ya Tanzania,ndio maana Yule kaburu wa south Africa,a president by then aliwahi sema,
Waafrica hawapaswi kuwa huru na kujitawala,akasema wanapaswa kuongozwa,kwa sababu hawana uwezo wa kujitawala ,lakini pia hawapendani wao kwa wao.
Akasema hata ukiwakabidhi bunduki Leo za kuilinda nchi,wataanza kufyatuliana risasi wao kwa wao.akahoji pale kwenye ile conference ,je watu Kama hawa tunapaswa kuwaamini watuongoze!!??
Makaburu wote wakashangilia,wakiashiria hoja iko sawa.na wanaunga mkono.
Ukweli kwa hali ilivyo hapa tz,unaweza kukubaliana na huyu raisi wa serikali ya makaburu kule s.africa by then.Watanzania tumekosa kuwa na umoja na upendo kabisa,tofauti na wenzetu nchi za magharibi Kama marekani,kipindi alipoumwa Trump,hatukuona chama pinzani Cha akina Obama na wafuasi wao washangilie kuugua kwake,kipindi alipoumwa borrison pia hatukuona ,uponzani au wafuasi wa uponzani wakishangilia kuugua kwake,zaidi walimtakia apone,hata Kama waliongea kwa unafiki ,lakini walificha hisia zao za itikadi za kisiasa.na kumtaki kheri apone.
Wamarekani kwenye tatizo wanakuwa kitu kimoja,Tofauti na ss hapa Tanzania.chuki zimejaa kwenye mioyo ya watu mpaka zimewapa upofu,wanasema chochote kinachokuja mdomoni ,haijalishi kina Jenga utaifa au kinabomoa,haijalishi kina fariji au kinaumiza,hawa ndio watanzania wa leo.hii inatupa picha mbaya Sana kwa majirani zetu,na dunia kwa ujumla.
Watanzania hasa vijana wa sasa,sisi ndio wakuifanya nchi hii itambulike kwa sifa njema,au itambulike kwa sifa mbaya ya chuki.Hakuna malaika atakaye kuja kunifanya Tanzania irudi kwenye heshima yake ya awali,Bali ni sisi vijana wa leo,watt wetu wakija nao wendeleze pale tutakapo ishia.je kwa chuki hizi watt wetu na wakujuu wetu,watakuwa na nn,je waridhi hizi chuki na wao wawaridhishe wajao!!??
Wakati wa shida tuwe kitu kimoja,hata Kama tunakinzana kisiasa na mitazamo.