Yuko wapi Rais Magufuli? Msiache tetesi zienee. Kama anaumwa mnasema "ANAUMWA"

Status
Not open for further replies.
Kwahiyo umejiunga leo ili uje ukomenti huu utumbo!??
Alipumzika zaidi ya mwezi mzima kwao chato mkamwaga maneno Watanzania bhana sijui Ni kwasababu ya kukosa kazi ama kweli ukikosa kazi ya halali shetani atakupatia kazi
 
Atapuuzwa tuu kama alivyopuuzwa kwa kusema ndie aliyempiga risasi huku akiwa hana mchango wowote kutoa ushahidi kwenye vyombo stahiki

Mungu ibariki Tanzania
 
Sisi kama watanzania tunapaswa kuwa pamoja na kiongozi wetu.
Mungu akuponyeshe haraka Rais wetu kama ni kweli huu mgonjwa.
 
Msichokijua ni kwamba ,kama hizo habari za kuwepo kwa watu wasiojulikana ni mpango wa CCM,basi hata akiondoka huyu bado hamtaweza kuwagusa kwakua hawakua chini ya mtu mmoja bali ni system ambayo hata yule atakaechukua nafasi yake atazidi kuilinda.
Uliza wale wa Hitler walikua kujulikanaje...!!?
 
Rais wetu ni binadamu, hata kama kweli anaumwa ndio ukamilifu wa ubinadamu wake, nadhani tufanye kazi tuache kuhusika na habari zisizo na chanzo rasmi . Aliumwa Mkapa, aliumwa na Kikwete. Kikwete alipo rudi ndio alitupa habari nini kilimsibu... tubaki kua watanzania na kuiombea nchi yetu.
 
Sio lazima. Mwanzo alizushiwa kifo na hakuwahi kutokeza mtu yeyote kukanusha. Kwahiyo wacha wajinga waendelee kutiana ujinga.
Correct,ni sawa kutotangaza.Usually tuna-weigh faida na hasara katika kufanya jambo lolote.Kwa mtizamo wangu taharuki itakuwa kubwa zaidi kama ikisemwa kwa mfano anaumwa sana.Ngoja watu wabakie kwenye two worlds,it's better.

Unajua mkuu,wapo watu wengi mno among us,ambao hawaitakii nchi yetu mema,hawa ndio wanaoshinikiza serikali itangaze kwamba Rais anaumwa.Sijui wanapata faida gani.Na wangefurahi kweli kweli,kama ingetangazwa kwamba he is suffering from respiratory problems.Mara moja wangekimbilia kusema ni Corona,na wangeongeza, kiko wapi sasa,si alikuwa ana-deny uwepo wa Corona,na alisema maombi yatasaidia,imempata mwenyewe sasa,mbona maombi hayajasaidia,dawa ni chanjo tu.Haya yote wange-bwabwaja bila hata kuwa na uhakika wa kiini cha tatizo.

Mkuu,hawa ni makarai ya zege yanayotumiwa na serikali za nchi za magharibi, they are mind controlled,na wengine hata naamini wameuza roho zao kwa Shetani,so niwa-kudharau.Agenda ovu against us za nchi za magharibi ndizo agenda zao,wamedandia meli wasiyojua hata inakwenda wapi!
 
Sasa ni wapi hapo niliposema kwamba haipo Tanzania kama ulivyodai?

Uko zuzu kiasi hicho?
 
Lisu anaendelea kujivua chupi mbele ya hadhara.
Magufuli huyo zake chato akimuapisha Katibu mkuu mpya wa CCM.

Nb. Lissu ana ndoto za kua Rais wa Tanzania lakini hata timiza ndoto zake.

Nawashauri watanzania wenzangu tumpuuze.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…