Yuko wapi Rais Magufuli? Msiache tetesi zienee. Kama anaumwa mnasema "ANAUMWA"

Yuko wapi Rais Magufuli? Msiache tetesi zienee. Kama anaumwa mnasema "ANAUMWA"

Status
Not open for further replies.
Kwahiyo umejiunga leo ili uje ukomenti huu utumbo!??
Alipumzika zaidi ya mwezi mzima kwao chato mkamwaga maneno Watanzania bhana sijui Ni kwasababu ya kukosa kazi ama kweli ukikosa kazi ya halali shetani atakupatia kazi
 
Sasa itakuwaje kwa Lissu ikiwa mheshimiwa ni mzima na yeye kesharipoti na kunakiliwa na vyombo vikuu vya habari kuwa yutaabani Nairobi kwa covid.
Itakuwa kuna mchezo amechezewa nao ni kupewa jukwaa bandia kusemea ili halafu ashushwe chini kabla ya wakati.Huu mchezo upo muda mrefu wanasiasa wa upinzani lazima waujue.
Atapuuzwa tuu kama alivyopuuzwa kwa kusema ndie aliyempiga risasi huku akiwa hana mchango wowote kutoa ushahidi kwenye vyombo stahiki

Mungu ibariki Tanzania
 
Mimi nadhani ifike mahali u bin Adam ushike nafasi yake.
Sisi ambao tumekulia na kulelewa katika dini tumeambiwa Jambo lolote ambalo usingependa likupate Basi usimtakie mwenzako yoyote limpate.

Kama ni kukosewa Basi amekosewa Mwenzezi Mungu kiasi ambacho hakuna kipimo kinachoweza kupima makosa hayo, lakini badala ya adhabu kutoka kwake Mungu imekua rehema.

Nae Mungu amesema Kama Mimi nilivyowasamehe nyinyi nanyi msameheane.

Akasema tena mpende na kumtakia mema yule anae waumizeni, yaani mtendee kinyume cheke yule anae kutendea baya.

Muombee asie kupenda, mpende anaekuchukia mtendee jema naekuudhi.
Hapo ndipo mtakapoonekana tofauti Kati ya wema na wabaya nae Mungu atakua upande wenu.


Badala yake Sasa sisi tumekua tukimtakia lililo baya kiongozi wetu katika nchi kisa yeye nae ametutendea mabaya, hii itapelekea wote kuhesabika Ni wabaya kwa namna hii.

Mungu ndie yupo juu ya wote na yote na vyote, hivyo Basi yeye atujuaye toka zamani atatutunzia yalio mema hata Kama tutapitishwa katika mabaya kiasi gani.

Haya yooooote yanayosemekana, yanayo hisiwa, yanayo takiwa kwa kiongozi wetu naomba yawe kinyume cheke AMINA.
Sisi kama watanzania tunapaswa kuwa pamoja na kiongozi wetu.
Mungu akuponyeshe haraka Rais wetu kama ni kweli huu mgonjwa.
 
Msichokijua ni kwamba ,kama hizo habari za kuwepo kwa watu wasiojulikana ni mpango wa CCM,basi hata akiondoka huyu bado hamtaweza kuwagusa kwakua hawakua chini ya mtu mmoja bali ni system ambayo hata yule atakaechukua nafasi yake atazidi kuilinda.
Uliza wale wa Hitler walikua kujulikanaje...!!?
 
Rais wetu ni binadamu, hata kama kweli anaumwa ndio ukamilifu wa ubinadamu wake, nadhani tufanye kazi tuache kuhusika na habari zisizo na chanzo rasmi . Aliumwa Mkapa, aliumwa na Kikwete. Kikwete alipo rudi ndio alitupa habari nini kilimsibu... tubaki kua watanzania na kuiombea nchi yetu.
 
Sio lazima. Mwanzo alizushiwa kifo na hakuwahi kutokeza mtu yeyote kukanusha. Kwahiyo wacha wajinga waendelee kutiana ujinga.
Correct,ni sawa kutotangaza.Usually tuna-weigh faida na hasara katika kufanya jambo lolote.Kwa mtizamo wangu taharuki itakuwa kubwa zaidi kama ikisemwa kwa mfano anaumwa sana.Ngoja watu wabakie kwenye two worlds,it's better.

Unajua mkuu,wapo watu wengi mno among us,ambao hawaitakii nchi yetu mema,hawa ndio wanaoshinikiza serikali itangaze kwamba Rais anaumwa.Sijui wanapata faida gani.Na wangefurahi kweli kweli,kama ingetangazwa kwamba he is suffering from respiratory problems.Mara moja wangekimbilia kusema ni Corona,na wangeongeza, kiko wapi sasa,si alikuwa ana-deny uwepo wa Corona,na alisema maombi yatasaidia,imempata mwenyewe sasa,mbona maombi hayajasaidia,dawa ni chanjo tu.Haya yote wange-bwabwaja bila hata kuwa na uhakika wa kiini cha tatizo.

Mkuu,hawa ni makarai ya zege yanayotumiwa na serikali za nchi za magharibi, they are mind controlled,na wengine hata naamini wameuza roho zao kwa Shetani,so niwa-kudharau.Agenda ovu against us za nchi za magharibi ndizo agenda zao,wamedandia meli wasiyojua hata inakwenda wapi!
 

[/HEADING]
[HEADING=3]Nyani Ngabu

Platinum Member​

May 15, 200687,8522,000
C-19 imepaishwa sana. Si kali wala hatari kama tulivyoaminishwa.

Ingalikuwa kweli ni kali na hatari, basi ingejulikana tu.

Watu walio wagonjwa hawawezi kufichika.

Shule zimefunguliwa toka mwezi gani vile?

Kampeni za uchaguzi zilianza mwezi gani vile?

Miafrika Ndivyo Tulivyo.
Thanks Quote Reply
Report
Sasa ni wapi hapo niliposema kwamba haipo Tanzania kama ulivyodai?

Uko zuzu kiasi hicho?
 
Lisu anaendelea kujivua chupi mbele ya hadhara.
Magufuli huyo zake chato akimuapisha Katibu mkuu mpya wa CCM.

Nb. Lissu ana ndoto za kua Rais wa Tanzania lakini hata timiza ndoto zake.

Nawashauri watanzania wenzangu tumpuuze.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom