Ndugu Mwanakijiji, tatizo lako unajitoa ufahamu kiasi kwamba unajifanya huelewi kwanini "kuna wanaoombea Magufuli awe mgonjwa" huku wengine wakitamani aondoke kabisa. Unafahamu fika kuwa moja ya mafanikio makubwa ya utawala wa Magufuli ni kujenga chuki ambayo haijawahi kuonekana katika historia ya Tanzania. Sasa kama ambavyo huwezi kupanda goroli shambani ukategemea kuvuna njegere, ndivyo ambavyo ukipanda chuki unavuna chuki.
Mlikuwa na fursa ya kumshauri abadili mwenendo, aache siasa za chuki na badala yake afanye jitihada kurejesha umoja na mshikamano wetu. Lakini mkawa mpo bize kumuimbia ngonjera na mapambio hata pale alipomwaga sumu kwenye umoja wetu.
Na alipoweka kando PhD yake ya Kemia na kugeuka mtu wa tunguri kuhusiana na Korona, hata ninyi mnaoishi Marekani iliyoathiriwa vibaya na Janga la Korona, mkakaa kimya, na occasionally mkawadhihaki wale waliosisitiza kuwa korona ipo na inaua.
Nisiume maneno. Mikono ya Magufuli imejaa damu lukuki. From za waliouawa MKIRU to akina Injinia Lwajabe to unknown number of our fathers and mothers, brothers and sisters waliokufa, wanaokufa na watakaokufa kwa korona kutokana na Rais Magufuli kuuhadaa umma kuwa ugonjwa huo ni "wa kawaida kama malaria."
Ndio anaumwa lakini usijitoe ufahamu kutarajia kuwa serikali hii inayondeshwa kimagumashi itawaambia ukweli Watanzania kuwa Magufuli anaumwa. Iseme ukweli ichekwe? Kwamba lile jabali lililoishinda korona limeishiwa kuangushwa chali na korona hiyo hiyo? No way!
Lemme remind you this [emoji117] working with the devil is a choice... one you should always avoid. You guys are going to learn this the hard way!