KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
Kuna sababu za kutotangaza hata kama anaumwa.Nchi imepigwa ganzi huku tetesi mbaya zikiendelea. Wenye dhamana ya usalama wa mh Rais kwanini mnaacha inafikia huku?
Mambo hayaendi hadi viboko? Tujulisheni hata kama kweli anaumwa tumwombee mpendwa wetu.
Yeye mwenyewe alishajiweka kwenye kona ambayo watumishi wake hawawezi kumwondoa hapo.
Alishajitangazia kuwa 'mungu' ndiye mlinzi wake mkubwa, kiasi kwamba akisikika akisema anaumwa, watu wataanza kuhoji kama "imani" yake kwa mungu wake imepungua.
Maana yake ni kwamba, yeye hawezi kuugua kwa sababu imani yake kwa mungu ni kubwa.
Na hasa kama ugonjwa wenyewe unaohusika ni corona, wafuasi wake wataanzia wapi kutangaza (kujulisha) kwamba na yeye "kaugonjwa kadogo haka ka kishetani" kanaweza hata yeye kumweka kitandani? Hiyo itakuwa ni aibu kubwa asiyoweza kuivumilia.
"HOFU ni ugonjwa mbaya zaidi ya ugonjwa wenyewe", yaani hataki kuwatia HOFU waTanzania kusikia kwamba haka ka corona kanaweza kumweka kitandani hata yeye mwenye mabunduki na mabomu yote ya machozi.
Ataanzia wapi sasa kuanza kuwahimiza wananchi wavae barakoa, huku akiwatishia wasaidizi wake wasizivae mbele yake! Kukubali kuwa anaumwa ni kuutangazia umma wa waTanzania kwamba kiongozi wao ni mwongo.
Aumwe? Dawa zote zile zilizogunduliwa na wataalam wake, ikiwa ni pamoja na kujifukiza zitakuwa zimeshindwa kumkinga yeye? Itakuwaje kwa makapuku raia zake anaowahimiza wazitumie hizo dawa na waachane na zile za mabeberu wanaotafuta kutuibia utajiri wetu!
Kwa hiyo, kuna sababu lukuki zinazozuia isitangazwe kuwa mkuu wa nchi anaumwa, hata kama ni kweli alikuwa anaumwa.
Labda useme kwamba anaweza yeye mwenyewe, akishapona vizuri kuutangazia umma wa waTanzania kwamba ameushinda huo ugonjwa kwa kutumia dawa ya Bupiji, kujifukiza na njia nyingine anazoziamini yeye.
Hii itakuwa njia nzuri ya kujitangazia ushindi katika anayoyaamini yeye; na bila shaka atajizolea sifa nyingi na kuwapata wafuasi wengi katika imani yake hiyo.
Na kama itakuwa hivyo, tujiandae kwa jeshi lake lililopo humu JF; maana ukumbi mzima utakuwa ni wa kwao.
Na kwa wale wengine wetu; kama ikidhihirika kuwa ni corona ndiyo ilikuwa imemnyamazisha..., tutashukuru kwamba Mungu amamlinda kiongozi wetu, lakini pia tutaridhika kwamba angalau amepata uzoefu wa kuonja joto ya jiwe ya Corona. Hatukumtakia imuue, lakini fundisho atakuwa amelipata hata kama ataendelea kushupaza shingo kwa sababu ya kuona AIBU kwa msimamo wake uliomfikisha huko.