Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Na hoja ndio ipo hapa!Kama Reuters wanataka serikali ikanushe habari ,serikali ipo kimya,duh naanza kuamini rumors hizi
Kulikua a heart attack hapo kati ya COVID-19 na IndiaMh yaani mtu aumwe corona apelekwe India? Devil is a lie.
USICHOFAHAMU NI KWAMBA PALE NAIROBI HOSPITAL LISSU NI KAMA NYUMBANI KWAO KULE KIJIJINI SINGIDA, HIVYO INATARAJIWA ANA VYANZO VINGI KUHUSU HILI ANALOLIZUNGUMZA. VYOMBO VYA HABARI VIKUBWA KAMA REUTERS, TELEGRAPH, BBC, THE GUARDIAN (UK) SIO WAPUUZI KUMFANYA SOURCE. LAKINI JAMBO KUBWA KABISA BADALA YA KUMSHAMBULIA LISSU KWANINI USIPIGE KELELE SERIKALI YETU ITUELEZE RAIS WETU KIPENZI YUKO WAPI MAANA NI HAKI YETU KUJUA!Mnamwamini huyu mwehu? Atupe taarifa alizipataje wakati yuko ughaibuni akitumikia mabwana zake? Shame on you Lissu. Unatafuta kiki kirahisi.
Kwani kasema kafa?
Kasema anaumwa na ameanza kutibiwa Nairobi - Kenya na sasa yuko India..
Akipona na kurudi, haitafuta ukweli kuwa aliugua; akapelekwa Kenya na kisha India...
Kama siyo, kanusheni. Kimya maana yake manakubaliana na ukweli huu...!!
Agenda bado ni mitano tena?
Amkusikia imenenwa imani yako ndiyo itakayo kuponya na pia imeandikwa usimjaribu BWANA MUNGU wakoLissu asema Magufuli amehamishiwa India akiugua Covid-19
Na Iddi Ssessanga
![]()
Kiongozi mkuu wa upinzani Tanzania, Tundu Lissu, amesema Alhamisi kuwa rais John Magufuli, ambaye hajaonekana hadharani kwa karibu wiki mbili, yuko India akitibiwa virusi vya corona na kwamba yuko katika hali mbaya.
Tundu Lissu, ambaye alishindwa na Magufuli kwenye uchaguzi mkuu mwaka jana, ametaja duru za kiafya na usalama kama vyanzo vya taarifa kwamba rais Magufuli amehamishwa kutoka hospitali nchini Kenya na kupelekwa India akiwa hali mahututi - lakini hakutoa ushahidi.
Wasemaji wa serikali ya Tanzania wamesalia kimya wakati uvumi ukienea kuhusu uwepo wa rais Magufuli mwenye umri wa miaka 61 pamoja na hali yake ya kiafya. Wawakilishi wa serikali za Kenya na India waliotafutwa na shirika la habari la Reuters hawakutoa taarifa pia.
Akiwa madarakani tangu 2015 na kupewa jina la utani la "Bulldozer," Magufuli alionekana kwa mara ya mwisho Februari 27 akiwa mwenye afya njema wakati wa hafla katika ikulu ya rais mjini Dar es Salaam.
Lissu aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba Magufuli alipelekwa kwenye hospitali ya nchini Kenya mwanzoni mwa wiki hii na kisha mahala pasipojulikana nchini India. "Amezimia tangu jana asubuhi," aliiambia Reuters bila kutoa ufafanuzi.
![]()
Magufuli akisalimiana na makamu wake Samia Hassan Suluhu.
Gazeti la Nation la nchini Kenya lilinukuu duru zisizotambulishwa za kisiasa na kidiplomasia siku ya Jumatano zikisema kwamba kiongozi wa Kiafrica, ambaye halikumtaja, alikuwa akitibiwa Covid-19 na akipumua kwa msaada wa mashine katika hospitali ya Nairobi.
Wawakilishi wa hospitali waliiambia Reuters hawakuwa na taarifa za kutoa. Mkurugenzi wa mawasiliano wa rais Magufuli Gerson Msigwa na msemaji wa serikali Hassan Abbas hawajajibu ujumbe wa Reuters kuzungumzia suala hilo. Wizara ya mambo ya nje ya India na ubalozi wake mjini Nairobi pia haukuwa na la kusema.
Ukanushaji wa Covid watatukatatuka
Magufuli amepuuza kitisho cha Covid-19, akisema Mungu na tiba za nyumbani kama vile kujifukiza vingewalinda Watanzania. Alivikejeli vipimo vya virusi vya corona, kukosoa chanjo akiitaja kuwa sehemu ya njama ya mataifa ya magharibi kuchukuwa utajiri wa Afrika, na alipinga uvaaji wa barakoa na watu kutotangamana kwa ukaribu.
"Ukanushaji wake wa Covid-19 umetatukatatuka, kukumbatia kwake sala tu na kupuuza sayansi kumemgeukia," alisema Lissu katika ujumbe wa Twitter mapema Alhamisi.
Soma pia: Corona: Rais Magufuli awaomba watanzania kufunga na kuomba
Kwa mujibu wa katiba ya Tanzania, makamu wa rais Samia Suluhu Hassan atachukua hatamu za uongozi kwa kipindi kilichosalia kwenye muhula wa miaka mitano ikiwa rais hawezi kutekeleza majukumu yake.
Tanzania iliacha kutoa takwimu kuhusu virusi vya corona Mei mwaka jana, wakati iliposema kwamba ilikuwa na visa 509 na vifo 21, kwa mujibu wa data zilizopo kwenye shirika la afya duniani WHO.
Mkurugenzi wa WHO barani Afrika Matshidiso Moeti aliuambia mkutano wa waandishi habari siku ya Alhamisi kwamba hana taarifa za moja kwa moja kuhusu afya ya rais Magufuli na kwamba haitakuwa busara kuvumisha. Amebainisha kwamba Tanzania sasa imetambua hatari ya Covid-19 kufuatia vifo vya maafisa wawili wa juu serikalini, na kusema data zaidi kutoka nchini humo zinakaribishwa.
"Vyovyote ilivyo kuhusu rais Magufuli, tunaweza tu kumtakia vema iwapo taarifa hizi zina ukweli, na tunakariri utayarifu wetu kuisadia serikali na watu wa Tanzania," alisema.
![]()
Rais Maguli akila kiapo kuongoza muhula wa pili baada ya kuchaguliwa tena Oktoba 2020, ambapo alimshinda mgombea wa Chama cha Democrasia na Maendeleo CHADEMA, Tundu Lissu. Lissu anadai Magufuli ni mgonjwa mahututi.
Magufuli, profesa wa zamani wa kemia kutoka kijiji cha Chato kaskazini-magharibi mwa Tanzania, alipanda haraka ngazi ya kisiasa baada ya kushinda kiti cha ubunge mwaka 1995. Magufuli aliechaguliwa rais mwaka 2015, amekabiliwa na tuhuma kutoka mataifa ya magharibi na vyama vya upinzani kwa kukandamiza demokrasia, madai ambayo anayakanusha.
Picha za televisheni zilimuonyesha Magufuli Januari 8 akimshukuru mwanadiplomasia wa juu wa China Wang Yi kwa kuja bila barakoa kukutana naye wakati wa ziara yake barani Afrika. Magufuli alisema hilo lilionyesha kwamba waziri huyo alikuwa akifahamu kuwa Tanzania haina Covid-19 na aliendelea kupeana naye mkono mbele ya kamera wakati wawili hao wakitabasamu. Maafisa wengine wa China waliokuwepo walivaa barakoa.
Moderator msifute hii habari kama ilivyo kawaida yenu au kuihamisha.
😂😂😂😂😂Imeshafutika hiyo Best. It’s just a matter of time before it is official that mitano tena is no more kwishney.
Sasa wale 19 watakula kodi za bure mpaka 2025Imeshafutika hiyo Best. It’s just a matter of time before it is official that mitano tena is no more kwishney.
Cha ababi siku hizi wagonjwa wa corona wanazimiaHayo mapovu mpelekee lissu afulie gwanda zake.
Mnapapalika sana yaani hadi huruma
Yaani mtu aumwe corona akimbizwe india,kwani india wana dawa ya corona?
Sio kila vuvuzela linajibiwa
Sasa wale 19 watakula kodi za bure mpaka 2025
Sasa kama taarifa unazo kwanini huzitoi alafu wengine wakitoa unakereka?
Hivi unajielewa kweli?
Kenya health system is so shitty haiwezi manage heart attack?Kulikua a heart attack hapo kati ya COVID-19 na India
Tunasubiri five againHii Sio Mara ya kwanza kumzushia raisi wetu Ugonjwa hivyo endeleeni tuu