Wasalaam
Limejitokeza wimbi la taarifa za mtaani kuwa kiongozi wetu mkuu wa nchi anaumwa hizi taarifa hazijathibitishwa na serikali wala hakuna kiongozi yeyote wa serikali aliyekanusha wala Taifa halijapata public notes/official statement kutoka mamlaka husika kuwa kiongozi wa nchi haumwi.
Mh.kutokuoneka wiki ya pili kwenda ya tatu sasa ndo kunatoa ukakasi kwamba huenda ni kweli kiongozi wetu anaumwa ,ila zinatumika nguvu nyingi huku mtandaoni kuaminisha umma kuwa kiongozi huyo sio lazima aonekane kanisani kwa sababu sio paroko,sio lazima aongee ongee kwa sababu yeye sio msemaji wa club kama Manara,sio paroko kwamba amepangiwa misa aende kubuhiri,sio sio sio zimekuwa nyingi.
Katika jambo ambalo kiongozi kwa sisi tunaomjua asingenyemaza kimya ni hili la mahindi kuzuiliwa mpakani Mh.Rais ni binadamu ,kama walivyo binadamu wengine wa kawaida , binadamu anaziliwa,anaishi ,anaugua,anakufa pia.
Kama ilivyo kawaida yake Mh.Rais ni mtu anaependa kuonekana hadharani kila mara,lakini awamu hii ya amependa kukaa kimya akiwa ofisni hilo kwetu sisi wananchi halitupi tabu sana.
Kwa nini sasa Mawaziri,wabunge na baadhi ya wateule wake watumie nguvu kumsifia na kupost kwenye mitandao kama vile wanamuombea afya njema na kumtia nguvu kipindi ambacho ndo kuna sintofahamu ya alipo rafiki yetu huyu Mh.Rais ,je kufanya hivo si ndo kuleta taharuki zaidi mtaani na maswali lukuki ya kujiuliza.
Makamu wa Rais wa zamani wa serikali ya Zanzibar Mh. Sharif alivyougua tuliambiwa hadi umauti unamkuta sio chama chake sio serikali ya Zanzibar ilikanusha.
Mwalimu Nyerere alipougua kansa ya damu na kwenda kutibiwa Uingereza tulijulishwa.
Mkapa alipoenda Uswiswi kutibiwa nyongwa tulijulishwa
Kikwete alivyougua tezi dume na kwenda Marekani kutibiwa tezi dume tulijulishwa sio hao tu kuna maraisi Africa wamekua wakienda kutibiwa Ulaya dunia inajulishwa pia TANZANIA yetu kigugumizi kinatoka wapi kwani Rais kuugua ni dhambi ?
Ni vizuri kuacha uvumi wa mtandaoni na serikali ije ikanushe jambo hili kuwa Rais haumwi yupo zake IKULU magogoni au CHAMWINO, sio kila waziri ana tweet au ana post kwenye mitandao yake hovyo hovyo na kuongeza taharuki kwa wananchi
Taharuki yoyote inayogusu maisha na afya ya namba moja lazima ijibiwe na mamlaka husika.
CCM na baadhi ya wateule wa Rais ,acheni kupost post hovyo hovyo mtandoni kana kwamba hamna akili
(Jokate,Mwana FA,Babu Tale,mliofanya ni utoto na ujinga kwenye mitandao yenu).
Rais wetu kama upo ofisini jitokeze tukuone tumekuzoea
Mh.Rais kama unaumwa pia tujulishwe ili tuzidishe maombi upone haraka urudi katika hali yako ya kawaida.
Ijumaa Kareem