Yuko wapi Rais Magufuli? Msiache tetesi zienee. Kama anaumwa mnasema "ANAUMWA"

Status
Not open for further replies.
Ninachofanya ni kujaribu kuitafuta historia yake ya kugombea ubunge,kuna mahali nilisoma kuwa si mtu wa kushindwa au kukubali kushindwa!
Lakini aliwahi kugalagazwa na mwalimu au sijui mkulima? mmoja huko kwao!

Kuna mambo hayana utashi wa "kukubali au kukataa"

Kama corona ikimwingia, hana utashi wa kukataa isimwingie.

Kwa hiyo hali hiyo inaweza kumtoa mbele za macho ya watu, apende au asipende.
 
Hii ndiyo tunataka sasa; hatutaki nchi kila mtu anajiropokea tuuu. Who are you!???
Ujinga umekujaa kwani nani kakwambia nchi ni mtu mmoja. Huko karibu yake kuna watu wanaoishi na ndugu wengine baada ya saa za kazi.
Taarifa zipo na zinasemwa; analipwa mshahara kwa kodi za wananchi lazima taarifa yake itolewe...kwani kazi msemaji wa serikali pamoja na ikulu ni nini?

Wengine wanasema eti uzushi isijibiwe mbona uzushi kuhusu milipuko ya magonjwa yamekua yakijibiwa?
 
umeongea ukweli kabisa Sema naogopa Ku like nsijenkaambiwa nithibitishe nilichoki like
 
Wasalaam

Limejitokeza wimbi la taarifa za mtaani kuwa kiongozi wetu mkuu wa nchi anaumwa hizi taarifa hazijathibitishwa na serikali wala hakuna kiongozi yeyote wa serikali aliyekanusha wala Taifa halijapata public notes/official statement kutoka mamlaka husika kuwa kiongozi wa nchi haumwi.

Mh.kutokuoneka wiki ya pili kwenda ya tatu sasa ndo kunatoa ukakasi kwamba huenda ni kweli kiongozi wetu anaumwa ,ila zinatumika nguvu nyingi huku mtandaoni kuaminisha umma kuwa kiongozi huyo sio lazima aonekane kanisani kwa sababu sio paroko,sio lazima aongee ongee kwa sababu yeye sio msemaji wa club kama Manara,sio paroko kwamba amepangiwa misa aende kubuhiri,sio sio sio zimekuwa nyingi.

Katika jambo ambalo kiongozi kwa sisi tunaomjua asingenyemaza kimya ni hili la mahindi kuzuiliwa mpakani Mh.Rais ni binadamu ,kama walivyo binadamu wengine wa kawaida , binadamu anaziliwa,anaishi ,anaugua,anakufa pia.

Kama ilivyo kawaida yake Mh.Rais ni mtu anaependa kuonekana hadharani kila mara,lakini awamu hii ya amependa kukaa kimya akiwa ofisni hilo kwetu sisi wananchi halitupi tabu sana.

Kwa nini sasa Mawaziri,wabunge na baadhi ya wateule wake watumie nguvu kumsifia na kupost kwenye mitandao kama vile wanamuombea afya njema na kumtia nguvu kipindi ambacho ndo kuna sintofahamu ya alipo rafiki yetu huyu Mh.Rais ,je kufanya hivo si ndo kuleta taharuki zaidi mtaani na maswali lukuki ya kujiuliza.

Makamu wa Rais wa zamani wa serikali ya Zanzibar Mh. Sharif alivyougua tuliambiwa hadi umauti unamkuta sio chama chake sio serikali ya Zanzibar ilikanusha.

Mwalimu Nyerere alipougua kansa ya damu na kwenda kutibiwa Uingereza tulijulishwa.

Mkapa alipoenda Uswiswi kutibiwa nyongwa tulijulishwa. Kikwete alivyougua tezi dume na kwenda Marekani kutibiwa tezi dume tulijulishwa sio hao tu kuna maraisi Africa wamekua wakienda kutibiwa Ulaya dunia inajulishwa pia TANZANIA yetu kigugumizi kinatoka wapi kwani Rais kuugua ni dhambi ?

Ni vizuri kuacha uvumi wa mtandaoni na serikali ije ikanushe jambo hili kuwa Rais haumwi yupo zake IKULU magogoni au CHAMWINO, sio kila waziri ana tweet au ana post kwenye mitandao yake hovyo hovyo na kuongeza taharuki kwa wananchi

Taharuki yoyote inayogusu maisha na afya ya namba moja lazima ijibiwe na mamlaka husika.

CCM na baadhi ya wateule wa Rais ,acheni kupost post hovyo hovyo mtandoni kana kwamba hamna akili
(Jokate,Mwana FA,Babu Tale,mliofanya ni utoto na ujinga kwenye mitandao yenu).

Rais wetu kama upo ofisini jitokeze tukuone tumekuzoea
Mh.Rais kama unaumwa pia tujulishwe ili tuzidishe maombi upone haraka urudi katika hali yako ya kawaida.

Ijumaa Kareem
 
Watuambie basi alipo jamani tuwaze mambo mengine
toka juzi tunamuwaza yeye tu.
Tupo kipindi cha Kwaresma.....pengine yupo kwenye mfungo na hataki kuonekana hadharani?
 

Mwanakijiji alishauliza hayo maswali mkuu.
 
Utoto na ujuaji kama upi ndugu?
Wewe kutwa ni kutishia ID za humu kuhusu sheria za mtandao, we changia mada hizo sheria kila mtu anazijua. Sasa unapoteza muda kutishia na kupiga mikwara isiyo na tija na unajua hakuna kitu unaweza kufanya.
 
Wewe kutwa ni kutishia ID za humu kuhusu sheria za mtandao, we changia mada hizo sheria kila mtu anazijua. Sasa unapoteza muda kutishia na kupiga mikwara isiyo na tija na unajua hakuna kitu unaweza kufanya.
Ohoo, hivi mtu akikwambia kutembea na mwanafunzi kutakufanya uende jela miaka 30 anakua amekutisha sio?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…