Yuko wapi Rais Magufuli? Msiache tetesi zienee. Kama anaumwa mnasema "ANAUMWA"

Yuko wapi Rais Magufuli? Msiache tetesi zienee. Kama anaumwa mnasema "ANAUMWA"

Status
Not open for further replies.
Sio lazima. Mwanzo alizushiwa kifo na hakuwahi kutokeza mtu yeyote kukanusha. Kwahiyo wacha wajinga waendelee kutiana ujinga.
nadhani licha kuwa ni ishara mbaya.. au sio tabia nzuri kundi fulani kumzushia kiongoz wa nchi kifo.
kuna haja ya viongozi hawa kuhitafakari, why hate against them imeongezeka?
haswa kipindi hiki?
 
Nzige nao wanaendelea kuchanja mbuga wengine wanaenda kuwa kitoweo cha Wagogo huko kanda ya Kati na kundi jingine linaelekea mkoa wa Tanga
 
Mnaotaka kujua Raisi yuko wapi

Yuko kwenye maombi ya siku 40 ya kwaresma kuombea nchi iondokane na Corona .Kama alivyobeba hilo jukumu kipindi cha Corona awamu ya kwanza sasa kaingia maombi awamu ya pili ya kuishinda Corona round hii ya pili.

Waombaji tuungane naye na katika hizi siku 40 za mfungo wa kwaresma tutaibuka washindi sisi na Mungu wetu .Migani na isiyoamini Mungu itabaki midomo wazi na itajua kuwa Yulo Mungu wa Tanzania aliye tofauti na miungu wa nchi zingine.Wa Tamzania ana nguvu kubwa ya kuipiga mateke Corona nje
Lakini si angeenda Chato kumwomba mungu wenu kama alivyozoea, huko Nairobi wana Mungu wao ambaye badala ya kuondoa Covid-19 akampenda zaidi yeye na Waziri wake. Wananchi wanapolia kuwa hospitali zetu hazina madaya, vifaa wala watumishi wakutosha Viongozi wetu ndo wanakuwa wa kwanza kusifia kuwa dunia nzima, pamoja na Wakenya, watu wanakuja kutibiwa kwetu lakini wao wakishikwa na Changamoto ya kupumua tu wanakimbilia Nairobi. Huyu Waziri walijaribu kuficha ugonjwa wake karibu miezi miwili lakini akajitokeza mwenyewe kuwa amepona anarudi kazini kuchapa kazi sasa huko Nairobi amesindikiza mgonjwa au ana pneumonia?
 
Kwani wakati wa utawala wa wenzake maisha yalikuwa rahisi? Mbona kwa mfano mimi kwa sasa nipo nafuu kiuchumi kuliko utawala wowote wa nchi yetu ila jamaa hapana! Kwangu mtu asiyejali utu wa mwingine simkubali hata akitununulia Noah sisi wote.

Utu kwanza, vitu baadaye. Haiwezekani unaamuru watu wampige risasi binadamu mwenzako kisa siasa. Haiwezekani watu wanaokotwa kwenye viroba wewe unachekelea tu. Waandishi wa habari za uchunguzi wanatekwa na kupotezwa mchana kweupe wewe meno nje tu.

Haiwezekani! Kazi kuwapandikiza vibaraka eti wadai uongezewe muda wa kutawala ili ufanye nini cha ziada? Unawakemea hadi viongozi wa dini wanaohamasisha watu kuchukua tahadhari ya magonjwa ya kushindwa kupumua, unawazodoa watumishi waliochukua tahadhari ya afya zao na za wengine kwa kuvaa barakoa. Wewe nani?
Good point
 
Lakini si angeenda Chato kumwomba mungu wenu kama alivyozoea, huko Nairobi wana Mungu wao ambaye badala kuondoa Covid-19 akampenda zaidi yeye na Waziri wake. Wananchi wanapolia kuwa hospitali zetu hazina madaya, vifaa wala watumishi wakutosha Viongozi wetu ndo wanakuwa wa kwanza kusifia kuwa dunia nzima, pamoja na Wakenya, watu wanakuja kutibiwa kwetu lakini wao wakishikwa na Changamoto ya kupumua tu wanakimbilia Nairobi.
Nairobi ni karibu na Chato,si kwa ajili ya ubora wa tiba zao.
 

Warumi 2​

Neno: Bibilia Takatifu​

2 Kwa hiyo huna udhuru wo wote, hata ukiwa nani, unapowahu kumu wengine. Kwa maana unapowahukumu wengine unajihukumu mwe nyewe, kwa kuwa wewe uliye hakimu unafanya mambo hayo hayo. 2 Tunajua kwamba hukumu ya Mungu huwafikia kwa halali wote wanaotenda mambo haya. 3 Je, wewe uliye binadamu tu, unapowahuku mu watu wanaofanya mambo hayo na huku wewe mwenyewe pia unafanya hayo hayo, unadhani utaepuka hukumu ya Mungu? 4 Au labda unad harau wingi wa huruma, uvumilivu na subira ya Mungu, ukasahau kwamba wema wake una shabaha ya kukufanya utubu?
Wenye Mamlaka wanapofanya Hukumu basi wayatende kwa HAKI. Wasipofanya hivyo basi nao Hukumu ya Mungu itakuwa juu yao. Ndiyo maana maandiko yanasema Hakimu wa kweli ni Mungu pekee. Tenda Haki unapokuwa umekikalia Kiti cha Maamuzi.
 
Nzige nao wanaendelea kuchanja mbuga wengine wanaenda kuwa kitoweo cha Wagogo huko kanda ya Kati na kundi jingine linaelekea mkoa wa Tanga
Kwa iyo nchi hadi kuvamiwa na nzige unasikia raha ? ndio.maana chadema tuliwapiga chini mko zero kwenye uzalendo.Hata nzige tu kuvamia madhba ya watu.mnachekelea

Yaani wewe wapiga kura wako mashamba yao kuvamiwa na nzige unachekelea kama bwege.Kinachokupa raha hapo nini? Wapiga kura kufa njaa .Wewe shetani kabisa na lichama lako
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom