Yuko wapi Rais Magufuli? Msiache tetesi zienee. Kama anaumwa mnasema "ANAUMWA"

Yuko wapi Rais Magufuli? Msiache tetesi zienee. Kama anaumwa mnasema "ANAUMWA"

Status
Not open for further replies.
Nampenda sana Rais wangu. Watwambie kama ni mgonjwa tuanze kufanya sala kwa bidii ili apone. Hatuwezi kuanza zoezi hilo bila ukweli kufahamika. Maana unaweza kuanza kuwombea mara unamwona huyo............ anashika kikapu chake kwenda feri kunua samaki., kama yuko Dar. Au mara unamwona huyooo.......... anapanda kwenye mwamba na kulala hapo akiota jiwe, kama yuko Dodoma.
 
Nimeona magari ya jeshi yamebeba mizinga.
Sijui wanaelekea wapi?[emoji26][emoji26][emoji26]
 
Kwanini bwashee?

Kila panapokuwepo na ulazima wa kuhabarisha umma juu ya jambo lolote kurugenzi ya mawasiliani ikulu imekuwa ikituhabarisha.
Kwani bwashee kwa hali ya sintofhamu kama hii unaona hakuna ulazima wa kuuhabarisha umma kuhusu fununu hizi? Kumbuka urais tumempa sisi. Hivyo tuna haki ya kufahamu.
 
Nampenda sana Rais wangu. Watwambie kama ni mgonjwa tuanze kufanya sala kwa bidii ili apone. Hatuwezi kuanza zoezi hilo bila ukweli kufahamika. Maana unaweza kuanza kuwombea mara unamwona huyo............ anashika kikapu chake kwenda feri kunua samaki., kama yuko Dar. Au mara unamwona huyooo.......... anapanda kwenye mwamba na kulala hapo akiota jiwe, kama yuko Dodoma.
Kama ni maombi hakuna siku inapita bila watu wa dini akina sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam na wenzake kumuombea affya na amani
 
Hiyo Nairobi hospital hakuna kitu pale, Nina rafiki yangu alikuwa ana sumbuliwa tumbo kila akienda Nairobi hospital wana pima anaambiwa ugonjwa hauonekani, amekuwa akifanya hivyo kwa zaidi ya miaka 7, baadae kuna rafiki yangu kutoka Malaysia alikuja kenya kussuport project, katika kuongea nae nikamuuliza kama kuna hospital nzuri inayo tibu malazi ya tumbo.

Baada ya siku mbili akapata DK mmoja , nikaongea nae baada ya hapo Yule DK aka niambie nimtumie majibu ya rafiki yangu kutoka Nairobi hospital, nilipomtumia kesho yake akamtumia analysis ya tatizo ambalo lina msumbua, baadae jamaa alikwenda Malaysia akatibiwa na akapona tena kwa gharama kidogo.

Hao hao wanaodai Nairobi hospital ni nzuri kwa nini walimpeleka tundu lissu Belgium? Angebaki tu hapo akatibiwa, huduma zap ziko chini matangazo ndio mengi na gharama ambazo hazina mantiki.
 
Unadhani kama hutaki kuamini, basi wote wana akili duni kama yako!???

😁😁😁😁😁😁😁😁
Hata kichaa hua anadhani watu wengine woote ni vichaa isipokua yeye. Sio wa kubishana nao watu sampuli ya wewe.

Mwenendo usio sahihi.
 
Kitendo cha serikali kukaa kimya ilhali uvumi unaendelea kuenezwa mitandaoni kuwa yu mgonjwa na kulazwa hospitali nje ya nchi ni suala linalotoa mwanya wa kurutubika kwa uvumi huo na kusababisha taharuki miongoni mwa jamii ya Watanzania.

Rais ni "taasisi ya umma" ambayo haipasi kunyamaziwa jambo lolote likiongelewa kuhusiana na taasisi hiyo.

Wahusika wajitokeze na kutoa ufafanuzi kwani suala la kuugua sio AIBU WALA HATIA. Maadam yeye ni binadamu anaweza kuugua kama yeyote kati yetu na kama ni mzima basi ajitokeze na kuwatia aibu wanaomzushia.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom