Kabende Msakila
JF-Expert Member
- Oct 7, 2020
- 2,091
- 1,918
Wanabodi;
Nianze kwa kuwapongeza kurudi kuwa kundi moja la kuijenga nchi na kuongeza uzalishaji kwenye kaya zenu.
Nimegundua kuwa nchi hii usipokuwa makini unaweza kutapeliwa kisiasa, unaweza kupitiwa na upepo wa nyakati na nusu wakati. Ni takriban mwezi na ushee tukiwa tumemaliza uchaguzi nchini - nachojiuliza ni:-
(i). Yule mgombea Urais aliyejitambulisha wakati wa kampeni kwa jina la Tundu Lissu yuko wapi? Kawaacha wapi akina Ponda, Bagonza?
(ii). Tunaingia msimu wa Kilimo lakini watanzania hatuoni achilia mbali kusapoti wakulima lakini hata kuhamasisha kilimo ili wananchi wajiongezee kipato - msimu wa Kilimo ukiisha aje kula kivulini?
(iii). Wanavyuo wa vyuo vya elimu ya juu wamemaliza mapumziko na kurudi vyuoni - hapiti hata kuwashukuru kwa kura walizompigia Oktoba 2020 - atakuja kuwashawishi eti waandamane kwa kuwa kura zake hazikutosha?
(iv). Wafanyabiashara wadogo "machinga" aliotuhubiria habari zao na wakampigia kura kwa upendo kaondoka bila hata kuwaaga - siku nyingine aje kuwaomba kura?
Kwa ujumla huyu Tundu Lissu alipaswa awepo nchini ili kwa taaluma yake ya mambo ya Sheria amsaidie Rais na Taifa kwenye nyanja hizo - mbona akina mama Mughwira hawakutoroka? Mbona akina Rungwe wapo? Mbona akina Lipumba wapo? CDM mshaurini huyu mheshimiwa aje nchini ajenge nchi yake - mkataa kwao ni mtumwa.
Taifa kwanza
Maendeleo hayana vyama
Mungu ibariki Tanzania
============
Hata tukio la viti maalum 19 kakaa kimya - kweli huyu alikuwa serious na kutaka urais? CDM shitukeni kama tulivyokwisha mshitukia huyu kuri wa mabeberu!