Yupi bora, mwanaume anayeacha pesa au anayenunua mahitaji yote mwenyewe?

Mko wachache sana wenye hii tabia wenzio sikuizi wanataka wabane kila sehemu
 
Una nafasi yako peponi 👊
 
Mimi kila kitu nanunua .

Na pia nitampa Pesa kwaajili ya Mambo mengine ambayo sio lazima aniambie.



Haya mambo ya kuacha Pesa mezan kila siku , yanafanya Mwanamke aweke akilin Pesa sana,kuliko kukuweka wewe akilini.
[emoji38][emoji38][emoji38] mkuu unafanya vyema wenye mkono wa birika wanapigiwa tu wake zao
 
Natamani wanaume wengine wajifunze kutoka kwako
 
Wapo hao watu ,tena wengi anaweza akashindia mihogo ya kukaanga na maji ya kudownload na watoto wakashindia uji ili mradi a_make akanunue kijora.
Kama kijola unamnunulia hiyo ela nyingine anafanyia nini
 
Tafuta kazi ya kufanya utakuwa huru wala hautakuwa unawaza kuanzisha uzi wa namna hii.
 
Mko wachache sana wenye hii tabia wenzio sikuizi wanataka wabane kila sehemu
Kuna siku wife nlimuambia kuwa hata kama hii pesa ya gesi nikikaa nayo mimi lazima niitoe tu pale ambapo gesi itaisha hivyo hakuna faida ya kukaa nayo mimi wakati ina matumizi yake ambayo lazima itumike,sasa kukaa nayo nafaidika nini ?

Ingekuwa ukikaa nayo na matumizi yanapungua hapo sawa

Alafu kitu kingine ni kuwa naona inanijazia wallet tu wakati sio yangu ile pesa.

Alafu ukikaa nazo mwanaume pesa za matumizi stress zinazidi unaona unatoa tu pesa,unatoa tu pesa,unatoa tu pesa,unatoa tu pesa,unatoa tu pesa,unatoa tu pesa unatoa tu pesa mpaka unajiuliza heee inakuwaje pesa inaenda hivi,kumbe ungemuachia wife kila kitu wala yasingekuja mawazo hayo
 
Watu kama wewe ukinitembelea kwangu nakuchinjia mbuzi tunakula huku tukipanga mipango yakuwa watu wenye nguvu zaidi nchini miaka 10 ijayo.

Siyo kujadili mambo ya jikoni huku unakuna kidevu, Kazi ya kike kabisa.
 
1.5km hadi utumie gari?
 
Baadhi ya wanawake unaweza ukaacha pesa na ukapigiwa simu ukirudi njoo na sukari,chumvi na nyanya.

Mimi nanunua vitu vya ndani vya kutumia na pia natoa hela ya emergency mezani.
Ukiona anazingua, unamnunulia mfuko wa sukari kilo 50, unamnunulia mchele kilo 100, unamnunulia chumvi kilo 20, unanunua mafuta lita 50.

Upime tena atamanage vipi
 
Una mawazo ya kizamani sana, sikushauri uoe mchagga au uje uishi huku ughaibuni.
Nadhani huo huenda ni udhaifu wangu. Hata sasa hivi ninakaa na washkaji, huwa sihangaiki na mambo ya manunuzi ya mahitaji ya ndani.

Tulishaona tunakulaje ( chakula common ) tunachanga, mimi nawapa tu hela.

Kama ikitokea tuna hamu ya chakula kingine nje ya budget Mwenye nayo anatoa tu, au tunachanga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…