Zaa kwa mahesabu, sio uzae watoto waje kufanywa Watumwa huku Duniani

Zaa kwa mahesabu, sio uzae watoto waje kufanywa Watumwa huku Duniani

ZAA KWA MAHESABU, SIO UZAE WATOTO WAJE KUFANYWA WATUMWA HUKU DUNIANI!

Anaandika, Robert Heriel
Shahidi!

UTUMWA!
Usukule!
Kutumwa tumwa! Kuvujishwa jasho pasipo malipo, Kulambishwa mavumbi ya viatu pasipo utu. Kuimba pambio katika wimbo wa walao nchi.

Manamba na vibarua wa mashamba, HAO ndio utakaowazaa waje kujambishwa na watoto wa wenzako? Sitaki majibu Yako hapa! Baki nayo.

Zaa Kwa Hesabu zenye jawabu. Sio uzae kama panya, kuzaa watoto wengi Kwa Zama hizi bila Hesabu sio tuu kukosa upendo Bali ni ukatili Kwa watoto wako.

Katika ulimwengu WA teknolojia na Ujuzi na maarifa wingi sio hoja Bali vioja.

Unakuwa na watoto wengi ambao wanatumikishwa kwenye viwanda Kama randa la mbao ndivyo wanavyoranda Randa wakinuka jasho.

Nazaa watoto Saba, najiita kidume kwenye mfumo dume.
Taikon sina shamba wala kiwanja, lakini ninawatoto Saba.

Haipendezi kuzaa watoto waje watumikishwe na kuteswa alafu mzazi bila aibu nawe Kwa ukatili mtoto unamnyonya zaidi mwanao licha yakuwa kipato chake ni duni.
Huo ni ukatili, unyanyasaji na ukosefu wa utu.

Tuzae Kwa Hesabu.
Watoto ambao tunauwezo wa Kuwatunza na kuwaandalia maisha MAZURI na Urithi ili wasiwe Watumwa.

Sio unazaa wapiga Kura wa watoto wa wenzako waluoandaliwa.
Sio anazaa watoto ambao watakuja kuwa vibarua.

Sisemi Kwa ubaya, au kupangia mtu Maisha.
Ila Kwa kweli hakuna kitu kibaya Kwa mzazi mwenye upendo kuona umezaa watoto ambao umewaleta kuja kuteseka na kuteswa na wanadamu wengine.
Mzazi asiye na upendo WA dhati hawezi ona uchungu Kwa mwanaye.

Kwani wengi huzaa Kwa ubinafsi wao tuu. Wakitaka watoto wao waje wawasaidie baadaye lakini hawataki kuwaandaa watoto hao kuishi maisha MAZURI.
Huo ni Ubinafsi na ukatili.

Kama huna uwezo wa kuandaa watoto waishi maisha mazuri, zaa Kwa hesabu. Watoto wachache wanaokutosha.

Jitahidi uangalie Quality zaidi kuliko Quantity.
Sio mtu unajivunia unawatoto wengi lakini watoto uliozaa ni Watumwa, misukule, na watu wanaoteswa na watu wengine.

Zamani watu walizaa watoto wengi Kwa sababu walikuwa wanauwezo wa kuwarithisha mashamba, maboma, na Urithi mwingine.
Lengo jingine na kuleta nguvu kazi katika jamii.
Lakini vipi Zama za leo?

Je tutazaa Kondoo wengi ambao wataongozwa na Simba mmoja?
Au tutazaa Simba mmoja kuongozwa Kondoo wengi?
Au tutazaa Simba wengi kutawala Mbuga?

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
True
 
[emoji4][emoji4]
Sahani zipo nyingi Sana.
Tatizo nyingi Kati ya hizo sahani zipo kwenye Meza ya usukule na utumwa
Kuzaa manamba , watumwa na vijakazi . Tena bora wangekuwa manamba wanaolipwa maslahi yenye future ,ni hands to mouth ,vicious cycle ya ukapuku generation after generation.
 
Kuna mtawala mmoja aliwahi kutawala Tanzania huku sijui akiwa amesahau kauli ya Rais ina Power pia ni Sheria alitamka kwenye mkutano wa hadhara kwamba "watanzania zaeni sana" nikajiuliza kwani nchi ina uhaba wa watu? maana mimi ninavyojua Watu ni rasilimali ya nchi pia katika kukuza Maendeleo.
Tanzania ina watu wa kutosha na wengi hawana ajira ni majobless. hujawapa kazi hawa bado unataka watu wazae he was not serously!

Rafiki yangu mmoja ana watoto saba mama tofauti anaishi nyumba ya kupanga he have not stability of finacial. aysee hapana watoto tunawapenda lakini tuangaliale na utaraibu wa kuzaa jamani nadhani hata na uelewa wengi hawana.
hakuna mashamba kama zamani ya kulima nowadays ushindani wa ajira ni mkali sana. ukuwaji wa technology kila kukicha unakuwa na wengi wanapoteza ajira due to ukuwaji wa tehema.
Wakiambiwa uzazi wa mpango wanasema mabeberu wanataka tusizae watutawale ,what a stupid argument ,kuna watu ni wapumbaf nchi hii basi tu
 
Jitu linazaa watoto 10 halafu hata kodi halitaki kulipa , linataka hao watoto wasome bure na kupata huduma za afya bure ,at whose expense ,angalia mamikopo nchi hii inavyotoboka eti ujenzi wa madarasa ,ujenzi gani wa madarasa huo usio isha ,pesa zinatumika kufanya mambo yale yale ,kuchimba vyoo za kujenga madarasa
 
Muheshimiwa alikuwa sahihi na huo ujinga wakufikiria ajira ndo unaleta uoga na upumbavu kwani kila mtu ataajirwa?
Hii mentality yakufikiria ajira tu kila mtu anataka kuwa ofisini ni utumwa pia tena inatakiwa ajira zipunguzwe zaidi ili watu wazoee hali watoke kweny utumwa huyu muheshimiwa alifungua milango kwa wafanyabiashara wadogo pia waendelee kujitegemea hii nchi inatakiwa iwe ya kibiashara ili isonge mbele iwe na watu wengi ili tutoke kwenye mawazo mgando yani ukifikiria ajira unakuta kuna wenzako kama elfu 50 hawana..

System inatakiwa ituforce tuwe wapambanaji tu kwenye biashara

Mkuu alikuwa sahihi ndo maana hakuajiri [emoji123][emoji123][emoji123]
Unaongea hivyo huku umebinua kinyelo kwenye makochi ya shemeji yako hapo ,unajiona mjanja as sio ?
 
Point, zaa ambao unaweza kulea na kama huwezi kulea usizae. Hakuna mtu atakusaidia kulea.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Hiyo ya kumtoa kafara mshua Noma sana
Kwanini wasikutoe kafara , umezaa tu watu waje wateseke huku ,nani anataka kuwa mtumwa na kuteseka ? ,Lazima wakupige na kitu kizito ili ukome ,ni kuwahiana siku hizi
 
Maisha hayana kanuni wewe bwabwaja ulale.
Kuna mtu kazaliwa peke yake lkn wazazi wameshindwa kumtunza na sasa ni kuli.
Kuna wapo walizaliwa wawili na wazi matajiri lkn sasa mwingine kahaba na mwingine mbwia unga.

Nwabwaja roho yako isuuzike ulale
Unaongea ujinga hao watoto wa matajiri wanaoishia kuwa hivyo ni kujitakia , tunazungumzia tabia chafu ya ubinafsi unazaaa kama panya huku ili watoto waje wateseke kwa kuishi kilofa kama watumwa huku duniani
 
Narudia...maisha hayana kanuni moja.
 
ZAA KWA MAHESABU, SIO UZAE WATOTO WAJE KUFANYWA WATUMWA HUKU DUNIANI!

Anaandika, Robert Heriel
Shahidi!

UTUMWA!
Usukule!
Kutumwa tumwa! Kuvujishwa jasho pasipo malipo, Kulambishwa mavumbi ya viatu pasipo utu. Kuimba pambio katika wimbo wa walao nchi.

Manamba na vibarua wa mashamba, HAO ndio utakaowazaa waje kujambishwa na watoto wa wenzako? Sitaki majibu Yako hapa! Baki nayo.

Zaa Kwa Hesabu zenye jawabu. Sio uzae kama panya, kuzaa watoto wengi Kwa Zama hizi bila Hesabu sio tuu kukosa upendo Bali ni ukatili Kwa watoto wako.

Katika ulimwengu WA teknolojia na Ujuzi na maarifa wingi sio hoja Bali vioja.

Unakuwa na watoto wengi ambao wanatumikishwa kwenye viwanda Kama randa la mbao ndivyo wanavyoranda Randa wakinuka jasho.

Nazaa watoto Saba, najiita kidume kwenye mfumo dume.
Taikon sina shamba wala kiwanja, lakini ninawatoto Saba.

Haipendezi kuzaa watoto waje watumikishwe na kuteswa alafu mzazi bila aibu nawe Kwa ukatili mtoto unamnyonya zaidi mwanao licha yakuwa kipato chake ni duni.
Huo ni ukatili, unyanyasaji na ukosefu wa utu.

Tuzae Kwa Hesabu.
Watoto ambao tunauwezo wa Kuwatunza na kuwaandalia maisha MAZURI na Urithi ili wasiwe Watumwa.

Sio unazaa wapiga Kura wa watoto wa wenzako waluoandaliwa.
Sio anazaa watoto ambao watakuja kuwa vibarua.

Sisemi Kwa ubaya, au kupangia mtu Maisha.
Ila Kwa kweli hakuna kitu kibaya Kwa mzazi mwenye upendo kuona umezaa watoto ambao umewaleta kuja kuteseka na kuteswa na wanadamu wengine.
Mzazi asiye na upendo WA dhati hawezi ona uchungu Kwa mwanaye.

Kwani wengi huzaa Kwa ubinafsi wao tuu. Wakitaka watoto wao waje wawasaidie baadaye lakini hawataki kuwaandaa watoto hao kuishi maisha MAZURI.
Huo ni Ubinafsi na ukatili.

Kama huna uwezo wa kuandaa watoto waishi maisha mazuri, zaa Kwa hesabu. Watoto wachache wanaokutosha.

Jitahidi uangalie Quality zaidi kuliko Quantity.
Sio mtu unajivunia unawatoto wengi lakini watoto uliozaa ni Watumwa, misukule, na watu wanaoteswa na watu wengine.

Zamani watu walizaa watoto wengi Kwa sababu walikuwa wanauwezo wa kuwarithisha mashamba, maboma, na Urithi mwingine.
Lengo jingine na kuleta nguvu kazi katika jamii.
Lakini vipi Zama za leo?

Je tutazaa Kondoo wengi ambao wataongozwa na Simba mmoja?
Au tutazaa Simba mmoja kuongozwa Kondoo wengi?
Au tutazaa Simba wengi kutawala Mbuga?

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam

Nadhani hata wewe hapo nyumbani Kwako unae h.girl/h.boy,vip wasingezaliwa hizo kazi ungefanya wewe?acheni hizo mambo na muheshimu uzao wa watu.wapo waliolazimika kuwa watumwa wa watu kutokana na wazazi kupoteza maisha pengine kwa ajali
 
Wapi nimesema tusiheshimu watu Mkuu.
Mimi nimetoa tuu tahadhari hasa Kwa watu wenye upendo Kwa watoto wao.

Lakini Kwa ambao hawajali na makatili basi waendelee
 
Wakati mwingine unakuwa na akili, wakati mwingine dishi linayumba 180°
 
Kuna watu ukiwaua sio dhambi.
Ila kwa serikali ni kosa kisheria.

Mama yake kabla sijamuoa anajua mumewe ni mtu wa namna gani.

Mimi sio Wale wakuvumilia mambo ya kipuuzi hasa yaliyo ndani ya uwezo wangu na ndani ya familia yangu
Hayo ni maneno tu hata kwenye khanga yapo
 
Swala la kuzaa niwezavyo sihitaji ushauri, sababu ninayo na nia ninayo. Siri ni moja mtu mvivu huogopa kuzaa.
 
Back
Top Bottom