TANZIA Zacharia Hanspope, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba afariki Dunia kutokana na Covid-19

TANZIA Zacharia Hanspope, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba afariki Dunia kutokana na Covid-19

Umelala kapteni hanspope,umekwenda mwamba wa vita.

Daima utaishi katika mioyo yetu sisi wahafidhina wa simba sport club sababu,
mapenzi yako kwa simba sport club hakuna kitu kiliweza kuvuka iyo line kwako katika maisha yako.
Baada ya kuachiwa huru wewe na wenzio kutoka
Kwenye kesi iliyowakabili wenzio kuamua kurudi shamba kulima.
kamanda uliamua kuvaa gwanda tena na safari hii uliamua maisha yako yote yaliyobaki kupambana kwa ajili ya klabu uliyoipenda kuliko kitu chchote simba sport club.
Hakuna kitu wanasimba tulitamani ikiwezekana uwe mwenyekiti wa maisha wa klabu yetu ila ilishindikana sababu ya mambo uliyopitia uko nyuma.
Moja ya heshma kubwa ambayo wanasimba tutakukumba nayo milele ni kua unatoa pesa zako bila kuulizia chenchi wala kudai kama walivyofanya wat wengi huko nyuma.
Siku zote umekua na klabu hii ya maisha yako katika vipindi vyote.
Mbali na huko nyuma kwenye klabu yetu makundi makubwa mawili ya friends of simba na simba asili kua yanapozekana kutoa wenyeviti wa klabu yetu but always hakuna mwenyekiti aliengia akathubutu kwenda bila wewe kama mwenyekiti wa kamati ya usajili.
Kazi uliyoifanya miaka yote katika vipindi vyote vigumu vya simba ukijua mwenyewe pesa unazitoa wapi.

Nenda mwamba daima utaishi katika mioyo yetu wanasimba,
Siku ngumu ambayo wanasimba tutaikumbuka milele.
Tangulia tutakutana baadae mwamba wa vita,chuma
ZACHARIA HANSPOPE.
 
alipatwa na mshtuko baada ya kuskia hawa jamaa ni darasa la 7
FB_IMG_16313069560092741.jpg
 
Back
Top Bottom