TANZIA Zahara wa Afrika Kusini afariki Dunia. Imedaiwa aliwekewa Sumu na Ndugu yake katika Sherehe ya Baada ya Mahari

TANZIA Zahara wa Afrika Kusini afariki Dunia. Imedaiwa aliwekewa Sumu na Ndugu yake katika Sherehe ya Baada ya Mahari

Habari ya kwanza niliyokutana nayo leo kwenye mitandao ya kijamii inahusu kifo cha mwanadada Mwimbaji Bulelwa Makutukana ( Zahara) kilicho tokea jana huko Johanesburg baada ya kuugua ini kwa muda mfupi.

Zahara amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 35.

Binafsi nitamkumbuka sana Zahara kwa wimbo wake "Loliwe".

Wimbo huu uliwahi kunisaidia katika nyakati ngumu.

To be honest with you. Taarifa ya kifo cha Zahara imefanya nafsi yangu iwe troubled kama nafsi ya Yesu ilivyokuwa troubled alipopewa taarifa za kifo cha rafiki yake Lazaro.

Asante Mungu kwa kuipa dunia zawadi ya kipaji kikubwa kama Zahara.


LALA NGOXOLO ZAHARA.

Update: Inadaiwa chanzo cha kifo chake ni multiple organ failure iliyo sababishwa na yeye kulishwa sumu na mmoja kati ya wanafamilia mara baada ya Zahara kutolewa mahari..

Taarifa nyingine inadai kwamba Zahara alilishwa sumu ya kichawi " muthi" kwenye chakula wakati ya sherehe ya kulipa mahari yake.

Duh kwamba kuna mwanafamilia alichukia kuona Zahara katolewa mahari? Just like that? Ooh please God protect your children from evil.
---

View attachment 2839995
Tasnia ya Burudani nchini humo imepata pigo lingine kutokana taarifa za kifo cha Mwimbaji Bulelwa Mkutukana maarufu Zahara (35) baada ya vifo vya AKA Februari 10, na CostaTitch, Machi 11, 2023.

Taarifa zimeeleza kuwa Kifo cha Zahara aliyetamba na nyimbo mbalimbali zikiwemo Loliwe' na Phendula kimetokea katika Hospitalini Jijini Johannesburg alikokuwa akipatiwa matibabu kutokana na kuugua maradhi ya ini kwa takriban Wiki 2. Pia kuna taarifa kuwa maradhi hayo yalisababishwa na sumu aliyowekewa na mmoja wa Mwanafamilia katika Sherehe ya baada ya kutolewa Mahari.

Vyombo vya Habari nchi humo vimeripoti kuwa siku chache kabla ya Kifo cha Zahara, Dada zake walichukua Kadi zake za Benki na kwenda 'Shopping' huku ndugu yao akipigania uhai wake Hospitali.

Enzi za Uhai wake Zahara aliwahi kuja Tanzania Oktoba 2018 ambapo alitoa burudani Jukwaa moja na Juliana Kanyomozi wa Uganda, na LadyJayDee katika Tamasha la Vocals Night liliondaliwa na Lady JayDee.
I am truly saddened by this uncalled for loss to Africa. I loved her voice really loved her.
 
...hakuna namna, mpatie, machozi ni tiba na msibani hawazuiliwi kulia maana ndiyo namna bora ya kumsahau marehemu kwa mabaya yake na kuyaishi mazuri yake
Bora nikaushe tu maana anaupenda hatari wala hatakagi kujua maana yake wala alie uimba... yeye nikuusikiliza kutwa
 
Dunia ilipofikia usimuamini mtu yoyote,jiamini mwenyew watu wabaya sana bora hata wanyama wana huruma
Tusiamini mtu ?

Wewe mbona umeamini hili li story la kuambiwa la kulishwa sumu na uvumi na umbea wa familia ya marehemu ?

Mmemfanyia toxicology exam kutafuta sumu kwenye figo, damu na mkojo ?

Au mshazika tayari?

Waafrika bana! Tunaishi kama Homo Erectus.
 
Aiseee, huyu sister kafariki!? Mimi ni mmoja ya mashabiki zake wakutupwa. Apumzike salama Zahara. Destiny ni wimbo wangu bora kabisa kati ya nyimbo kali nyingi alizowahi kutoa.
Destiny ndo wimbo wa kwanza kwangu pia kumfahamu huyu dada aisee [emoji24][emoji24][emoji24]
 
Duniani alijichetua chetua kwa Yesu mara asifunike nywele ....saivi anaenda kukutana na aliyemuumba ajibu (Allah)
 
Back
Top Bottom