Zaidi ya ndege 30 za Israel zimeanza kunyesha mabomu ndani ya Yemen

Zaidi ya ndege 30 za Israel zimeanza kunyesha mabomu ndani ya Yemen

Hamna cha maana atapiga hapo Yemen atapiga piga visehemu ila utashangaa kesho asubuhi kimerushwa kitu hapo Israel. Kwa kifupi mpaka sasa marekani, Israel na wenzao hawajui hao wahouth viwanda vyao vya silaha vipo wapi. Halafu hiyo picha uliyotuwekea ni ya mwaka 2018 badilisha weka ya leo
 
...hizi Siasa za Ki Dunia za nchi za kutunishiana misuli ni siasa za kale sana-kwa maoni yangu naona ina manufaa kwa watu wachache sana, na inatumiwa na viongozi ili waonekane wagumu mbele za wapiga kura wao kama ilivyokuwa kale

Mambo ya kale sana
 
Hii ni ukweli jana warirusha kibom kikapiga uwanja wa ndege iselael kati Netanyahu ndo akasema ataalpiza kumbe ni leo leo analipiza
 
Kutoka Israel hadi Yemeni zaidi ya 2000 kilometres.
Mtuambie hizo ndege zina matank mawili mawili ya mafuta ama!?

Ndege za kijeshi za Israel, hasa zile za kivita kama F-15, F-16, na F-35, zina uwezo wa kufanya safari za umbali mrefu, lakini kufikia Yemen, ambayo iko takriban kilomita 2,000 kutoka Israel, kunahitaji mipango ya makini ya kimkakati.

Hapa kuna uchanganuzi wa uwezekano:Uwezo wa Ndege:Ndege za Israel kama F-35 na F-15 zinaweza kusafiri umbali wa zaidi ya kilomita 2,000, lakini hii inategemea mambo kama mzigo wa silaha, mafuta, na hitaji la kurudi. Kwa mfano, F-35 ina radius ya mapigano ya takriban kilomita 1,100, na F-15 inaweza kufikia hadi kilomita 2,000 bila kujaza mafuta angani.Ili kufikia Yemen, ndege hizi zingeweza kuhitaji kujaza mafuta angani kwa kutumia ndege za tanka kama Boeing 707 za Israel, ambazo zimeonyesha uwezo wa kusaidia operesheni za mbali.

Mifano ya Operesheni Zilizopita:Israel imefanya mashambulizi ya umbali mrefu hapo awali. Kwa mfano, mwaka 1985, ndege za Israel ziliruka hadi Tunisia (kilomita 2,400) kushambulia makao makuu ya PLO katika Operesheni Wooden Leg, zikisaidiwa na kujaza mafuta angani.

Hivi majuzi, ripoti zinaonyesha kuwa Israel imefanya mashambulizi Yemen dhidi ya malengo ya Wahouthi. Kwa mfano, Desemba 2024, ndege za Israel ziliripotiwa kushambulia maeneo ya Yemen, zikilenga bandari na miundombinu ya kijeshi, zikidai kutumia ndege 14 na kurusha mabomu 60 na makombora ya usahihi.
 
zaidi ya ndege 30 za kivita za Israel zimezingira muda huu ndani ya Yemen huku zikipiga bandari , uwanja wa ndege na vituo vyote vya mawasiliano.

Hali ya tahadhari imetolewa muda huu Kwa raia nchini Yemeni kuhama kwenye maeneo yote yaliyo chini ya wapiganaji wa houthi.View attachment 3325460
UZURI WA MYAHUDI anatoa taarifa haendi kama jambazi.
Mbarikiwe vijana wa Yakobo
 
Hamna cha maana atapiga hapo Yemen atapiga piga visehemu ila utashangaa kesho asubuhi kimerushwa kitu hapo Israel. Kwa kifupi mpaka sasa marekani, Israel na wenzao hawajui hao wahouth viwanda vyao vya silaha vipo wapi. Halafu hiyo picha uliyotuwekea ni ya mwaka 2018 badilisha weka ya leo
Sijahakiki habari maana nipo mbali na TV ila shambulio hili naona ni kazi bure maana maeneo yanayosemekanwa kupigwa ni yale yale aliyoyapiga USA wiki iliyopita.
Na shambulio hili ni dogo kuliko la USA la wiki iliyopita.
La USA lilikua kubwa mno na liliua watu wengi zaidi ila bado Houthi walirusha makombora.
 
Kutoka Israel hadi Yemeni zaidi ya 2000 kilometres.
Mtuambie hizo ndege zina matank mawili mawili ya mafuta ama!?
Zipo na mama yao-wakijisikia kunyonya wananyonya kwa raha zao
 

Attachments

  • images - 2025-05-05T204031.073.jpeg
    images - 2025-05-05T204031.073.jpeg
    4.5 KB · Views: 18
  • download - 2025-05-05T203959.784.jpeg
    download - 2025-05-05T203959.784.jpeg
    7.2 KB · Views: 13
  • images - 2025-05-05T204026.011.jpeg
    images - 2025-05-05T204026.011.jpeg
    5.1 KB · Views: 15
Sijahakiki habari maana nipo mbali na TV ila shambulio hili naona ni kazi bure maana maeneo yanayosemekanwa kupigwa ni yale yale aliyoyapiga USA wiki iliyopita.
Na shambulio hili ni dogo kuliko la USA la wiki iliyopita.
La USA lilikua kubwa mno na liliua watu wengi zaidi ila bado Houthi walirusha makombora.
Kwa hiyo sifa ni kubaki na uwezo wa kurusha makombora?
Hawaangalii casualties?
 
Shambulio hili bado sio zito kama la USA la wiki iliyopita.
Nakuhakikishia hao Houthi wataendeleza mashambulizi tu baada ya hili.
Lengo halikuwa kuwanyang'anya uwezo wa kurusha makombora. Lengo ni kulipiza kwa kile walichokifanya na kujisifia kuwa watafunga anga la Israel, yule msemaji wao sijui alilewa mirungi.
 
Sasa Kwa akili yako km 2000 ni kikwazo Kwa teknolojia ya leo?
Ulimwambia ameshindwa hoja ndio maana akatukana.
Lakini yeye alimjibu alieanza kumuita mpumbavu, wala haihusiani na hizo 200kms. Kaangalie vizuri
 
Back
Top Bottom