Sehemu ya Tano
View attachment 2659398
Ukiwauliza wale jamaa kwamba hayo mataji 43 wanayomiliki kwa pamoja ni ya ubingwa wa mashindano gani, watakujibu kuwa ni ligi ya bara.
Hapa ndipo wanapojifichia kwa kuwa hatuna udadisi na tunakosa vitengo vya rekodi, kumbukumbu na historia kwenye taasisi zetu za mpira.
Kimsingi ni kwamba Ligi ya Bara haikuishi miaka mingi kiasi cha kutoa mataji yote hayo.
Ilianza mwaka 1982 na kuisha mwaka 2003...miaka 21 tu. Yanga mara 11 na Simba mara 6!
Sasa wao wanayahesabu mataji haya na kuyachaganya na yale ya ligi ya kwanza ya 1965 hadi 1981, kisha wanahesabu mataji ya ligi ya sasa, ndiyo wanapata 43!
Iwe kwa kutojua au kwa makusudi, hayo ni makosa makubwa.
Ligi iliyoanza 1965 haikuwa ya Bara, ilikuwa ya Muungano na hata vilabu vya Zanzibar vilishiriki, kama nilivyofafanua kwenye sehemu zilizopita.
Kwa hiyo bingwa wa ile ligi ya zamani hakuwa wa bara, alikuwa wa Muungano.
Wao kama wanataka kuhesabu mataji ya bara pekee, basi wahesabu ya 1982 hadi 2003...kwa sababu hiyo ndiyo ilikuwa ligi ya bara.
Ligi iliyoanza 1965 kama klabu bingwa ya taifa, ilikuwa ya muungano na kuanzia 1982, ikabadishwa jina muundo na mfumo.
Jina la kwanza lilikuwa Klabu Bingwa ya Taifa, jina jipya likawa Ligi ya Muungano.
Muundo wa kwanza ulikuwa kuanzia ngazi ya wilaya hadi taifa, muundo mpya ukawa wa madaraja, la kwanza hadi nne, kutokea pande zote mbili za Muungano.
Mfumo wa kwanza ulikuwa kwa mtoano, muundo mpya ukawa wa mzunguko, nyumbani na ugenini na kuhesabu alama.
Lakini licha ya mabadiliko hayo, bingwa alibaki na hadhi ile ile, yaani kutambuliwa na FIFA na CAF na kupata tiketi ya kushiriki Klabu Bingwa/Ligi ya Mabingwa Afrika.
Sasa hawa jamaa wanaacha kuhesabia ubingwa wa ligi ya muungano wa kuanzia 1982 hadi 2003, wanahesabu ubingwa ile ligi ya bara ambayo ilikuwa sawa na mtihani wa moko.
Kwa sababu kwenye hiyo ligi ya Muungano hawakupata mataji mengi hivyo haina maana kwao.
Kwa hiyo wanajifariji kwa kuwa Tanzania One kwenye Moko na kujitangaza walifaulu, kisha wanayaacha matokeo ya mtihani wa taifa kwa sababu walipata Zero!
Itaendelea...