Zamani kuoa Mzungu ilikuwa Dili lakini siku hizi kijana usije ukajichanganya.

Zamani kuoa Mzungu ilikuwa Dili lakini siku hizi kijana usije ukajichanganya.

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Hamjambo!

Zamani kidogo nchi yetu ilikuwa maskini Sana. Yaani ninaposema Maskini namaanisha Maskini Mno, fukara, apeche Alolo.

Kama huelewi nazungumzia nini nasi nikusaidie kuunda picha kichwani Mwako.
Fikiria zamani kuwa na Luninga ikionekana ni Tajiri.
Fikiria kuwa na baiskeli au Pikipiki ilionekana unamaisha mazuri.
Fikiria wenye makochi na masofa walionekana matajiri.

Fikiria ATI kuwa na jokofu, brenda, sijui Simu, na vikorokoro vingine ulionekana ni Tajiri.
Kama hiyo haitoshi, Fikiria atu kutumia Blueband, jam, peanut butter, na Kula mkate ilionekana upo mambo Safi.

Ati zamani kuwa na Gari ilionekana unamaisha mazuri.

Sasa bhana kipindi hicho hivyo ndio vitu ambavyo ukioa Mzungu unaweza kuvipata. Jambo ambalo wazazi na Vijana wengi WA Wakati huo waliona wameyapatia maisha, na huenda walikuwa sahihi.

Lakini siku hizi Wazungu ukiwaoa Hawana ziada yoyote katika suala la kiuchumi ambalo litafanya uheshimike ndani ya jamii.

Wengine tulibahatika kuingia katika mahusiano na hao Watoto wa kizungu.
Na Baadhi ya marafiki zetu bado wako na hao Wazungu. Hakuna tofauti yoyote ya kiuchumi wanayotofautiana na Sisi.

Vitu vyote vya kawaida ambavyo wanapewa na Wazungu unaweza kuvipata wewe mwenyewe Kwa jasho lako.
Na wapo Vijana wengi wanapambana wenyewe na wanamiliki vitu vizito na wakiwa huru tofauti na wakiwa na mabinti wa kizungu.

Faida kubwa ya kuwa na hivi vibinti vya kizungu, ni exposure, Kubadili mtazamo, kwenda nje ya nchi. Lakini Kwa habari za uchumi ambazo Vijana wengi ndio lengo Lao Huko mtapoteza muda tuu.

Labda uchukue kibibi cha kizungu ukitapeli, hivi vibibi angalau ndio vinapesa. Lakini hawa mabinti ambao Sisi kina taikon ndio tunataka Hawana Pesa.

Na kumzalisha Mzungu sio Pouwa, labda umzuge Kwa Kufunga naye ndoa, alafu Baada ya kuzaa naye Watoto ndio umkimbie.
Kama Rafiki yangu mmoja wa Arusha, lakini huo ni Utapeli.

Anyway
 
Wazungu wa generation hii ni choka walio kuwa na pesa ni Ile generation ya babu zao wao walikuwa nazo walizopata Afrika kabla ya Uhuru.
 
Hao watoto wa kizungu wanaowapata Sio wale classic wengi wanauziwa rangi tu.
 
Back
Top Bottom