Zamani nilikuwa namshangaa mtu aliyefanikiwa kimaisha na hasaidii ndugu zake, Leo mimi natamani hata kuwapiga Risasi

Kwani huwezi kumsaidia mtu wakati huo huo ukaweka mipaka ya mazoea ya kijinga jinga?? Kitu tunachokosea wabongo ni kuleta mazoea yasiyo na msingi na ile dhana ya polygamy family, unakuta mtoto wa shangazi sijui mama mdogo, mtoto wa dada wote wanakaa kwako.. Hapa lazima kuna lawama..

Mzee Mkapa alikuwa na ndugu wengi tu na alikuwa akiwasaidia sana sana pasipo kuwa na mazoea yaliyovuka mipaka na ki ukweli hao ambao aliweka nao mipaka waliupokea msaada na wakautumia vizuri. Sasa cha kushangaza Kuna binti mtoto wa dada yake aliyemchukua na kuishi nae, huyo ndiye akaja kuwa sifuri na wa ajabu kabisa.

Tujifunze kusaidia wengine na kuweka mipaka ya mazoea, ndugu wana lawama lakini kuacha kuwasaidia eti kuogopa hizo lawama hiyo nayo ni roho mbaya iliyovuka mipaka.
Mimi kusaidia ndugu haina shida na Wala huwa sipati changamoto shida Ni marafiki au majirani unatoa msaada kwa roho mmoja then baadae mtu anaanza kubadili maneno na kukuchongea chuki kwa watu wakati uko busy ili uonekane vibaya kwa watu unaoishi nao.
Mimi ndugu hata akinisema naona kawaida shida uko sehemu tofauti na nduguzo unajitoa kwa moyo then inakuletea shida Ni heri nisingetoa kabisa huo msaada
 
Zegota Msaada una hatarisha uhuru wa mtu, mimi ningekuwa ndugu yako ningekuroga hasa ufilie kwa mbali, ndugu zako wako sahihi kukuumiza, kukuombea mabaya!

kwa nini unawasaidia? kwani wao vilema? hawana mikono? akili, na utashi? au Mazezeta pa kutoa misaada hupajui? Ndugu zake Matonya, Mayatima! shule ya viziwi Buguruni Malapa, hupajui? peleka misaada huko!

Misaada hatari kwa uhuru, kwa nini ulihatarisha uhuru wao kwa misaada yako? na ulijuaje ulicho wapa kinakidhi mahitaji yao? wewe ndiyo una roho mbaya! unachuki ambayo huijui, unawaroga kisaikolojia kwa kile unachoona binafsi ni Misaada! umtatulie ndugu yako matatizo usiyo yajua?

Ndugu zangu wa Damu, popote mlipo Diasporas na kwingineko ole wenu mnisaidie mimi Nyarusare, naanza nanyi kuwamaliza! wengine wanajipendekeza kupenyeza vijimisaada maksudi sababu Baba ya mtu ni tajiri, ili wamsimange baadaye! na ku gain popularity! kupitia mgongo wangu!

Ndugu Mpe njia yatosha, usimuonyeshe njia, bali Mpe njia ya mafanikio halafu mtupe nje ya Mawanda yako, Mtukane on the spot! atajiju hiyo safi sana, atarudi kukushukuru! na mtakuwa kitu kimoja!

Na ndugu mpenda vya kupewa toka hapo kwa bro! wako, anza hivo ulivo! kalale chini sokoni kariakoo! kashinde stendi, kula kwa ma ntilie, osha vyombo/suuza, atakulipa, Malori ya Mkoa yakija usiku jichanganye na Matingo piga kazi upate msingi. Msaidie wewe huyo anaye penda kukupa misaada wewe.

Weye ndiyo uwe tegemeo la misaada kwao, siyo wewe ndiyo upewe kataa vya kupewa hata ukilala njaa! ikibidi watie Bakora seriously wale watoa misaada kwako wote! then watupie hela zao usoni, japo huna kitu! hii itawachanganya, soon watakuiga mwenendo wako wa maisha!

Mleta Mada wewe ni Hatari sana! kuliko siraha za maangamizi au Bomu la Nuclear! Msaada haujawahi kuiletea jamii yeyote Maendeleo Duniani! Leo miaka zaidi ya hamsini bado Tanzania mnatega Bakuri chanzo humuhumu yaani ni watu km wewe!
Mkuu japo kama umenisimanga vile lakini nimekuelewa chief
 
Ukiendekeza ndugu utakufa kibudu na Mungu hautamwabudu,utamkana wa joto utamkana wa baridi atabaki wa vuguvugu naye ataleta gubu.🚶🚶
 
kaa nao mbali ila usiache kuwasaidia panapo ulazima mfano suala la elimu,afya,na uhitaji wowote muhimu,pia usaidiapo usiwekeze kwenye kutegemea kuja kulipwa,fanya kama mabeberu wao jukumu lao ni kusaidia haijalioshi wananangwa vipi kwa walamba misaada kina jiwes and company
Mkuu sina tegemeo la kulipwa ninaposaidia, tatizo wamejawa na chuki bila sababu za msingi. Wamenitafuta mimi nimewakwepa kwa kila namna sasa wanamchokonoa mama, wadogo zangu na familia yangu kwa kiwango ambacho hakivumiliki kwa binadamu yoyote yule. na Hili linafanyika mlengwa haswa nikiwa ni mimi hao wengine wanatumika kama chambo

Niliyumba kimaisha kidogo wakaonesha furaha za waziwazi na bado sikujali nikaendelea kuwakumbatia niliporudi katika hali yangu ya kwaida,lakini wanachokifanya kwa sasa siwezi kukitaja hapa ni mambo yanayoumiza sana hayavumiliki
 
Ni mara chache kumkuta Mchaga,Mhaya,Msukuma na Mnyakyusa analalamika ndugu hivi ndugu vile!

Binafsi sijutii kuwa karibu na ndugu zangu hata ila kuna watu mnatokea koo za ajabu sio siri
 
I like the phrase "Koo za ajabu sio Siri"
 
Mkuu sina tegemeo la kulipwa ninaposaidia, tatizo wamejawa na chuki bila sababu za msingi. Wamenitafuta mimi nimewakwepa kwa kila namna sasa wanamchokonoa mama, wadogo zangu na familia yangu kwa kiwango ambacho hakivumiliki kwa binadamu yoyote yule. na Hili linafanyika mlengwa haswa nikiwa ni mimi hao wengine wanatumika kama chambo

Niliyumba kimaisha kidogo wakaonesha furaha za waziwazi na bado sikujali nikaendelea kuwakumbatia niliporudi katika hali yangu ya kwaida,lakini wanachokifanya kwa sasa siwezi kukitaja hapa ni mambo yanayoumiza sana hayavumiliki
Kaa nao mbali jiadhari nao mbali. Hapo ndo ile dhana ya kumsiadia masikini ni kuhatarisha maisha yako inapojitokeza.
 
Mkuu sina tegemeo la kulipwa ninaposaidia, tatizo wamejawa na chuki bila sababu za msingi. Wamenitafuta mimi nimewakwepa kwa kila namna sasa wanamchokonoa mama, wadogo zangu na familia yangu kwa kiwango ambacho hakivumiliki kwa binadamu yoyote yule. na Hili linafanyika mlengwa haswa nikiwa ni mimi hao wengine wanatumika kama chambo

Niliyumba kimaisha kidogo wakaonesha furaha za waziwazi na bado sikujali nikaendelea kuwakumbatia niliporudi katika hali yangu ya kwaida,lakini wanachokifanya kwa sasa siwezi kukitaja hapa ni mambo yanayoumiza sana hayavumiliki
Mkuu kazi ndogo sana hiyo! wabwatukie km huna akili nzuri vile! usiwe mlaini! nina waza tu!
 
Acha uzwazwa

Tangu uzaliwe umewahi kuona maiti inaozea barabarani kwa kukosa watu wa kuizika ?
Ndugu yangu ndiye ZWAZWA unayeshabikia mtu awpige risasi ndugu zake na wazazi wake waliomfikisha kwenye mafanikio eti kisa hataki kuwapa msaada! Huo ni ujinga wa kiwango cha kutisha ndo ninyi mkihamia mijini hata mzazi wako akija kukusalimia unambulisha eti ni mama wa rafikiako mko nae kabila moja! Mlaaniwe wote mlio na mawazo ya kipuuzi kama hayo! Eti siku ukifa limwili lako lipelekwe kwa haohao unaowakana ndio wakakupe heshima na wakusetiri kabulini, kwanini wasikuzike hao huko ulokula nao mafanikio yako! Aisee kama ni mimi naweza hata kulipasua sanduku kwa teke kali sana!
 
Heading tu imenivunja mbavu
Sitaki kusoma ulichoandika
 
Mambo mrembo, ni rahisi Sana kushirikiana na rafiki kiuchumi kuliko ndugu,ndugu ni vichomi
Safi momy ale..za masiku...nakumiss.hivi sijui kwanini inakua hivi? Ila Kuna rafiki yangu kwao wako 5! Wanasaidiana Sana...Yani hakuna kukopa nje .wanakopana wenyewe na kupigana tafu balaa! Sijui wengine inakuwa ishu
 
Mimi kusaidia ndugu haina shida na Wala huwa sipati changamoto shida Ni marafiki au majirani unatoa msaada kwa roho mmoja then baadae mtu anaanza kubadili maneno na kukuchongea chuki kwa watu wakati uko busy ili uonekane vibaya kwa watu unaoishi nao.
Mimi ndugu hata akinisema naona kawaida shida uko sehemu tofauti na nduguzo unajitoa kwa moyo then inakuletea shida Ni heri nisingetoa kabisa huo msaada
Mkuu marafiki na sijui jirani kusaidia hiko kiherehere acha kabisa...

Hao ni watu wa kushirikiana nao kwenye mambo ya kijamii tu kama misiba, sherehe na vitu ka hivyo..

Mzee Mengi alikuwa anawasaidia sana watu wenye ulemavu lakini alichokipata ni kuambiwa anapewa pesa nyingi na wazungu then ye anaishia kuwapa wali tu..
 
Sasa kibongo bongo ukisema uache kushirikiana ni hatari Sana wanaweza hata kukudhuru imagine tu hata ukiwa busy na yako bado inakuwa shida na matatizo.
Ila ndio nimekoma na kujifunza binadamu hatuna jema
 
Kwakweli mie kusaidia ndugu zangu hata siwazi mara mbili mbili. Kama kuna mengine ndani ya nafsi zao basi ni juu yao mie hainihusu, i just do my part.
 
Sasa kibongo bongo ukisema uache kushirikiana ni hatari Sana wanaweza hata kukudhuru imagine tu hata ukiwa busy na yako bado inakuwa shida na matatizo.
Ila ndio nimekoma na kujifunza binadamu hatuna jema
Sasa kushirikiana kivipi zaidi ya misiba na sherehe?? Kwenye msiba onekana toa na rambirambi na sherehe hivyo hivyo..

Ushirikiano zaidi ya huo ni kujipendekeza na uswahili tu.. We pambana na yako mkuu usiogope ya watu
 
Mkuu sina tegemeo la kulipwa ninaposaidia, tatizo wamejawa na chuki bila sababu za msingi. Wamenitafuta mimi nimewakwepa kwa kila namna sasa wanamchokonoa mama, wadogo zangu na familia yangu kwa kiwango ambacho hakivumiliki kwa binadamu yoyote yule. na Hili linafanyika mlengwa haswa nikiwa ni mimi hao wengine wanatumika kama chambo

Niliyumba kimaisha kidogo wakaonesha furaha za waziwazi na bado sikujali nikaendelea kuwakumbatia niliporudi katika hali yangu ya kwaida,lakini wanachokifanya kwa sasa siwezi kukitaja hapa ni mambo yanayoumiza sana hayavumiliki
Hao sio ndugu na wachawi khaa![emoji15][emoji15][emoji15]

Ishi kibandindu mkuu, huelewi?
 
Sasa kushirikiana kivipi zaidi ya misiba na sherehe?? Kwenye msiba onekana toa na rambirambi na sherehe hivyo hivyo..

Ushirikiano zaidi ya huo ni kujipendekeza na uswahili tu.. We pambana na yako mkuu usiogope ya watu
Ndio shajifunza navaa tinted ya mbao, hawana nafasi
 
Back
Top Bottom