cariha
JF-Expert Member
- Apr 9, 2015
- 22,077
- 46,549
Mimi kusaidia ndugu haina shida na Wala huwa sipati changamoto shida Ni marafiki au majirani unatoa msaada kwa roho mmoja then baadae mtu anaanza kubadili maneno na kukuchongea chuki kwa watu wakati uko busy ili uonekane vibaya kwa watu unaoishi nao.Kwani huwezi kumsaidia mtu wakati huo huo ukaweka mipaka ya mazoea ya kijinga jinga?? Kitu tunachokosea wabongo ni kuleta mazoea yasiyo na msingi na ile dhana ya polygamy family, unakuta mtoto wa shangazi sijui mama mdogo, mtoto wa dada wote wanakaa kwako.. Hapa lazima kuna lawama..
Mzee Mkapa alikuwa na ndugu wengi tu na alikuwa akiwasaidia sana sana pasipo kuwa na mazoea yaliyovuka mipaka na ki ukweli hao ambao aliweka nao mipaka waliupokea msaada na wakautumia vizuri. Sasa cha kushangaza Kuna binti mtoto wa dada yake aliyemchukua na kuishi nae, huyo ndiye akaja kuwa sifuri na wa ajabu kabisa.
Tujifunze kusaidia wengine na kuweka mipaka ya mazoea, ndugu wana lawama lakini kuacha kuwasaidia eti kuogopa hizo lawama hiyo nayo ni roho mbaya iliyovuka mipaka.
Mimi ndugu hata akinisema naona kawaida shida uko sehemu tofauti na nduguzo unajitoa kwa moyo then inakuletea shida Ni heri nisingetoa kabisa huo msaada