Zambia: Hakainde Hichilema atangazwa mshindi wa Urais

Zambia: Hakainde Hichilema atangazwa mshindi wa Urais

Sawa sawa. Naye aanze retaliation sasa kama kawaida ya mtu mweusi! The best he can do ni kusamehe yaliyopita na kuanza enzi Mpya isiyo na visasi. Otherwise, the cycle shall continue over and over again endlessly. Huyu jamaa aliumizwa sana; pamoja na hayo asamehe kwa ustawi wa Zambia ya leo na kesho.
Sahihi kabisa alikuwa incarcerated for 127days kabla ya kuachiwa baada ya UK kuingilia Kati
 
Chanzo cha taarifa yako na Edgar Lungu wa PF ameshakubali matokeo na kumpengeza mshindi. Taarifa yako haioneshi wapiga kura walikuwa wangapi, hii idadi ya watu uliowataja inaonyesha Kama wapiga kura walikuwa wachache Sana.
Population ya Zambia ni 18m as per 2010.census. wapiga kura waliojiandikisha walikua 7m.hivi, waliojitokeza kujipiga kura walikua 5.6m...tu.sasa piga hesabu mwenyewe hapo.
 
Ni jambo jema! Ila kushinda upinzani haina maana na matatizo ya Nchi yataondoka! Leo hii wamalawi wanatamani Mutharika arudi madarakani, mpinzani aliyechukua nchi anazingua mbaya mnoo!

Ana kashfa sasa hivi nchini kwake ya kubeba family members (ambao walichukua nafasi za maofisa wa serikali waliotakiwa kuhudhuria vikao) kwenda kwenye mkutano wa wa kiofisi London, kikubwa kilichowapeleka ni kutalii! Mimi nafikiri dhamira ya mtu ni jambo muhimu kuliko upinzani/utawala! Leo hii US na demokrasia yake yote, lakini signature moja tu ya Biden imetosha kuwarudisha Taliban Afghanistan
Umeandika ukweli mtupu. Nakupa kongole! Haitoshi kufanya mabadiliko ya watawala na vyama pasipo kufanya au kuleta mabadiliko ya kweli katika maisha ya watu. Hilo ndilo tatizo sugu kwa Malawi na Zambia.

Kwa Malawi alianza kuingia mpinzani Bakili Muluzi, akafanya madudu na ufisadi wa kutisha. Akaja Bingu wa Mutharika na kuanza na upendeleo (nepotism), akaja Joyce Banda na hata kutaka kutunyang'anya ziwa Nyasa lote! Akaja Profesa Arthur Peter Mutharika na madudu yake mengi.

Amekuja mchungaji Chakwera na upendeleo wa kifisadi kuliko hata watangulizi wake. Hadi anawateua mtu na mkewe kuwa mawaziri! Wamalawi wamefanya kazi kubwa ya mabadiliko lakini watawala hawabadiliki, wanakuja na uozo uleule!

Zambia walimtoa KK na kumleta Chiluba aliyelewa madaraka na kuwa fisadi mpaka wazambia wakamkumbuka KK. Akaja Levy Mwanawasa lakini akafa haraka kabla ya kuleta mabadiliko.

Akaja Rupiah Banda na ufisadi mwingi. Akaja Michael Satta na udikteta na kisha kufa haraka. Akaja Lungu na kumtwanga lungu rais mteule Hakainde Hichilema aka "HH" hadi kumsweka rumande kwa uhaini wa kubambikiza kama tufanyavyo hapa.

Lakini Wazambia wameonesha hawajachoka kufanya mabadiliko ya vyama na watawala. Sasa tunaomba HH asiwe kama waliomtangulia, bali afanye mabadiliko ya kweli katika maisha ya watu pasipo kuwatwanga na kuwatwika "tozo kandamizi" za SSH!

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
Kaunda alishindwa na mipinzaniChiluba alikubali matokeo na nusu saa tu baada ya kutangazwa ameshindwa alihama ikulu
Huu ndiyo ulikuwa msingi wa uchaguzi huru na haki. Kaunda alifanya jambo kubwa sana. Hulu kwetu hakuna kitu kama hiki, sio kwa sababu wapinzani hawashindi, bali wanaoshindwa hawakubali kushindwa.
 
Sawa sawa. Naye aanze retaliation sasa kama kawaida ya mtu mweusi! The best he can do ni kusamehe yaliyopita na kuanza enzi Mpya isiyo na visasi. Otherwise, the cycle shall continue over and over again endlessly. Huyu jamaa aliumizwa sana; pamoja na hayo asamehe kwa ustawi wa Zambia ya leo na kesho.
Kawa muungwana kasema anawasamehe wote waliomkwaza na kuwakamata wapinzani,kazi iendelee
 
Umeandika ukweli mtupu. Nakupa kongole! Haitoshi kufanya mabadiliko ya watawala na vyama pasipo kufanya au kuleta mabadiliko ya kweli katika maisha ya watu. Hilo ndilo tatizo sugu kwa Malawi na Zambia.

Kwa Malawi alianza kuingia mpinzani Bakili Muluzi, akafanya madudu na ufisadi wa kutisha. Akaja Bingu wa Mutharika na kuanza na upendeleo (nepotism), akaja Joyce Banda na hata kutaka kutunyang'anya ziwa Nyasa lote! Akaja Profesa Arthur Peter Mutharika na madudu yake mengi.

Amekuja mchungaji Chakwera na upendeleo wa kifisadi kuliko hata watangulizi wake. Hadi anawateua mtu mkewe kuwa mawaziri! Wamalawi wamefanya kazi kubwa ya mabadiliko lakini watawala hawabadiliki, wanakuja na uozo uleule!

Zambia walimtoa KK na kumleta Chiluba aliyelewa madaraka na kuwa fisadi mpaka wazambia wakamkumbuka KK. Akaja Levy Mwanawasa lakini akafa haraka kabla ya kuleta mabadiliko.

Akaja Rupia Banda na ufisadi mwingi. Akaja Michael Sata na udikteta na kisha kufa haraka. Akaja Lungu na kumtwanga lungu rais mteule Hakainde Hichilema aka "HH" hadi kumsweka rumande kwa uhaini wa kubambikiza kama tufanyavyo hapa.

Lakini Wazambia wameonesha hawajachoka kufanya mabadiliko ya vyama na watawala. Sasa tunaomba HH asiwe kama waliomtangulia, bali afanye mabadiliko ya kweli katika maisha ya watu pasipo kuwatwanga na kuwatwika "tozo kandamizi" za SSH!

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
Kweli mkuu,sijui tatizo ni nini!?
 
Usiku wa leo mda wa saa 0200, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi wa nchi hiyo amtangaza Mpinzani wa Chama cha UNDP kuwa Rais wa nchi baada ya kushinda Kwa kura 2.8m akimuacha Rais Edga Lungu wa PF kwa kura kama 1M. VivA Zambia!

======

View attachment 1893970
Hichilema is popularly referred to by his initials 'HH' or Bally (slang for dad)

Zambian opposition candidate Hakainde Hichilema won Zambia's presidential election, defeating incumbent Edwar Lungu, the southern African nation's election commissionannounced early on Monday.

Hichilema secured more than 2.8 million votes, while Lungu was in second place with over 1.8 million votes in the vote held last Thursday. Hichilema, 59, had been leading in exit polls and preliminary election results released throughout the weekend.

Now, Hichilema faces the daunting task of turning around the economic fortunes of debt-laden Zambia.

Zambia, a copper-rich nation, defaulted on a $42.5 million sovereign debt payment in November.

Zambian voters look for change

Rising costs of living and the impact of the pandemic had led to frustration with Lungu's rule. He had been in office since 2015.

Voters were also concerned about rising costs of living and crackdowns on dissent. Young Zambian's often complain of a lack of opportunity.

World Bank sounds alarm over developing world's debt

A former business tycoon who entered politics, Hichilema, ran for the presidency for the sixth time this year. The 2021 election was his first victory, after he campaign was able to take advantage of dissatisfaction over Lungu's handling of the economy.

During one of his final campaign speeches, Hichilema said, "It hurts to see citizens go to bed without food in such a country," adding that Zambia's rich natural resources have not translated to well-being for the population.

"Assets worth billions of dollars are yielding nothing... to better our lives," he said.

Lungu says election was 'unfair'

Hichilema has challenged Lungu three times previously for the presidency.

Lungu had cried foul before a winner was declared, claiming the elections were neither free nor fair due to alleged acts of violence at polling stations. He would have to approach Zambia's Constitutional Court within a week to formally lodge a complaint.

Hichilema's victory comes with the backing of ten opposition parties under the banner of United Party for National Development (UPND), the largest opposition party.

Source: DW
Chama tawala walizima mitandao kama CCM wafanyavyo, walimfunga siku 127 na akatoka, MBOWE anaandaliwa kuwa raisi, CCM jiandaeni, mmebaki na Polisi ndio wanawalinda na kuona watanzania kama mazombi.
 
Hopefully this change of the country’s administration from one party to another will soon take place in our beautiful country too.
Wapi?TZ au Burundi tulikohamia?[emoji38]
 
Zambia sio Tanzania, chadema msijifariji kupitia nchi ya Zambia,ninyi mtaendelea kuwa ndugu watazamaji Hadi miaka 1000 ijayo.
😀 😀 😀 hata Malawi raisi Mutharika alikuwa anajifariji kama wewe. Kumbuka kwamba kizazi chetu si kizazi cha hawa waliozaliwa 2000 kuja chini, hao nao wataandika historia yao. Kizazi cha wapigania uhuru kinatokomea
 
Siyo mara ya kwanza mgombea wa upinzani kushinda. Hata hapa imetokea mara kadhaa wagombea wa ubunge na udiwani kutoka upinzani wakatangazwa kushinda. Tatizo kwetu ni kuwa wapinzani wanaposhindwa kiti cha urais basi wanalalamikia tume hata kama namba haziwasapoti kabisa
Mkuu mazingira ya uchaguzi uaofayika Zambia sio sawa kabisa a hapa kwetu! Huwezi hata kidogo kuligaisha a sisi katiba ya wazambia waastahili kutemea kifua mbele! Level yao iakaribia Wamarekani, sisi hapa kwetu imekuwa ni ngumu sana maana kule kuwa Ikulu anatumia vibaya mamlaka yake kupenyeza maagizo kwenye vyombo vyote vinavyohusika na uchaguzi! Ndio maana kila wapinzani wakipaza sauti kuhusu katiba wananyamazishwa kwa nguvu kubwa sana sababu siku tukipata angalau katiba kama ya Wazambia hakika utakuwa ndi mwisho wa utawala wa ccm!
 
Mwaka 1991 Chiluba alishinda Urais wa Zambia akiwa mpinzani.Akimuondoa Kaunda.Lakin mpaka Leo mbona uchumi wao mbovu tu.Naipenda China ,hakuna tamaa ya vyama vingi kushika madaraka.Kazi tu ndio italeta maisha bora.
Hakuna tamaa au wana lazimishwa?!!unafikiria wananchi wa china/urusi hawapendi demokrasia?!sio kuwa kuna uhakikisho kuwa mpinzani, akiongoza ataleta mabadiriko!!lakini haiwezi ku justify, kuwalazimisha wananchi wasichague chama wanachokitaka!!
 
Hongera nyingi kwa Wazambia kuwezesha mabadiliko, Huu ndio mfumo sahihi wa upinzani sio kila uchaguzi chama kimoja tu kinang'ang'ania kushinda hata kwa njia zisizo za haki!
Tunaomba siku flani Mungu wa Wazambia ashukie na hapa kwetu Tanzania, awezeshe mabadiliko ya aiuna hiyo bila umwagaji wa damu wala kukamata watu hovyo!
 
Zambia sio Tanzania, chadema msijifariji kupitia nchi ya Zambia,ninyi mtaendelea kuwa ndugu watazamaji Hadi miaka 1000 ijayo.
Yeah. Uko sawa. Maana ya halisi ya kauli hii ni kuwaambia Watanzania wote kuwa wataendelea kushuhudia utawala wa CCM hadi miaka 1000 ijayo. Hii ni jeuri kama zile zisizotambua hata uwezekano wa “unusual divine intervention”. Jeuri ya wana CCM. Not bad. Imezoeleka.

Itakuwa vyema pia kama unafikiri kuna chama kingine zaidi ya CHADEMA kinachoweza kuibadili CCM madarakani karibuni ukiwafahamisha Watanzania angalau wasione umewadharau kupita kiasi.
 
Siyo mara ya kwanza mgombea wa upinzani kushinda. Hata hapa imetokea mara kadhaa wagombea wa ubunge na udiwani kutoka upinzani wakatangazwa kushinda. Tatizo kwetu ni kuwa wapinzani wanaposhindwa kiti cha urais basi wanalalamikia tume hata kama namba haziwasapoti kabisa
Wanalalamika sababu katiba hairuhusu wakapinge matokeo mahakamani sasa watafanyaje zaidi ya kulalamika.

We mzee unazeeka vibaya.... Toka upotoshe kuwa classmate yupo kwenye mfungo kumbe yupo kuzimu tayari! umepoteza credibility mpaka leo.
 
Hakuna tamaa au wana lazimishwa?!!unafikiria wananchi wa china/urusi hawapendi demokrasia?!sio kuwa kuna uhakikisho kuwa mpinzani, akiongoza ataleta mabadiriko!!lakini haiwezi ku justify, kuwalazimisha wananchi wasichague chama wanachokitaka!!
Anajiita baba wa demokrasi USA ,mbona kila siku kuna malalamiko?Demokrasi ya marekani ina popular vote na vote za watu 550 wenye kuchagua Rais na mwelekeo wa nchi.Si kila MTU mpaka muuza maandazi anachagua Rais kama Africa. Nafikiria democracy za kiafrika ni kusaidia watu wasio na kazi nao pia waibe na familia zao.Naipenda China.Kila MTU akafanye kazi. Sio kina Heche hawana kazi,wanawaza kuwa wabunge.Utopolo mtupu.
 
Wanalalamika sababu katiba hairuhusu wakapinge matokeo mahakamani sasa watafanyaje zaidi ya kulalamika.

We mzee unazeeka vibaya.... Toka upotoshe kuwa classmate yupo kwenye mfungo kumbe yupo kuzimu tayari! umepoteza credibility mpaka leo.

Unaweza kujifurahisha kwa kutafuta sababu za kukufanya ujisikiea vizuri hata kama sababu hizo siyo za kweli. Hata kama Katiba yetu ina mapungufu, mtu mwenye akili timamu hawezi kukubali kuwa:

(1) Mwaka 1995 Mrema alimshinda Mkapa ila tume ikabadili matokeo ilihali CCM ilivuna wabunge zaidi ya robo tatu ya bunge zima na viti vya udiwani zaidi ya asilimia 85 vilichukuliwa na CCM. (Kampeini hii mimi nilishiriki sana nikiwa NCCR-Mageuzi, lakini data zilitusuta tukanyamaza)
(2) Mwaka 2000 Lipumba alimshinda Mkapa ila tume ikabadili matokeo ilihali CCM ilivuna wabunge zaidi ya robo tatu ya bunge zima na viti vya udiwani zaidi ya asilimia 85 vilichukuliwa na CCM.
(3) Mwaka 2005 Mbowe alimshinda Kikwete ila tume ikabadili matokeo ilihali CCM ilivuna wabunge zaidi ya robo tatu ya bunge zima na viti vya udiwani zaidi ya asilimia 85 vilichukuliwa na CCM.
(4) Mwaka 2010 Slaa alimshinda Kikwete ila tume ikabadili matokeo ilihali CCM ilivuna wabunge zaidi ya nusu ya bunge zima na viti vya udiwani zaidi ya asilimia 75 vilichukuliwa na CCM.
(5) Mwaka 2015 Lowassa alimshinda Magufuli ila tume ikabadili matokeo ilihali CCM ilivuna wabunge zaidi ya nusu ya bunge zima na viti vya udiwani zaidi ya asilimia 70 vilichukuliwa na CCM.
(6) Mwaka 2020 Tundu Lissu alimshinda Magufuli ila tume ikabadili matoke ilihali CCM ilivuna wabunge zaidi ya asilimia tisini na tisa ya bunge zima na viti vya udiwani zaidi ya asilimia 99 vilichukuliwa na CCM.

Vyama vyote vya upinzani Tanzania havijui kuendesha siasa, ila vinajua sana kulalamikia tume. Siasa zinaanzia kwenye grassroots, huwezi kupata kura za watu wasiokufahamu; vyama vya upinzani viko kwenye maeneo fulani ya nchi tu. Havikusambaa nchi nzima na kwa muundo huo usitegemee kuwa vitakuja kushinda kiti cha uraisi bila kubadili mbinu kuwafikia wapiga kura kwa karibu.

Kujiaminisha kuwa wagombea wa uraisi huwa wanabadalishiwa matokeo na tume ya uchguzi ni uwongo usiokuwa na msingi wowote. Mbona kuna waliokuwa wabunge wengi wa upinzani walikuwa wanashinda viti vyao na hawakuilalamikia tume kuwa imefanya upendeleo. Mbowe amekuwa mbunge wa Hai kwa miaka 15 ukiachia kipindi alichogombea uraisi, Zitto pia amekuwa mbunge kwa miaka 15 mfululizo kwa sababu wanatoka majimbo ambayo vyama vyao vimejiimarisha.
 
Back
Top Bottom