Uchaguzi 2020 Zanzibar: Askari wanaolinda usalama wa watu na mali zao, washambuliwa kwa Mawe!

Uchaguzi 2020 Zanzibar: Askari wanaolinda usalama wa watu na mali zao, washambuliwa kwa Mawe!

Sawa..waache waendelee kutumia silaha zao duni za stone age.

Leo na kesho, Askari wa usalama wakianza kutumia chuma, serikali inaanza kuonekana ina matatizo na wananchi wake.

Wananchi Msijaribu kucheza na vyombo vya usalama na askari wake pasipo na sababu ya msingi.Tutawaumiza.
Hakuna sehemu kwenye katiba polisi aliporuhusiwa kumdhuru mwananchi kwa silaha ya moto ikiwa mwananchi huyo hana silaha ya moto.

Kama wakiwapiga risasi na wananchi hawana risasi wana la kujibu ,kama ni mawe kuna njia nyingi tu za kuwatawanyisha .
 
Waathirika wa vikwazo ni sisi wananchi na sio watawala,waadhibiwe watawala ikiwezekana physical na sio sisi wanan

ukitaka kujua ni usanii mtupu na hakuna namna ya kudeal na viongozi ambao nchi zinaingia machafukoni,rejea ya ruto wa kenya na ICC yake.saa hizi ni makamu wa rais na anatarajia kuwa rais ajaye wa kenya.
 
Kuna Message CCM wameipata kupitia huu uchaguzi ila kama ilivyokawaida mtu kuupokea ukweli na kukiri ni ngumu baadhi ya wakongwe wa chama wameamua kukaa kimya tu ila kuna ujumbe umeonekana tayari
 
Hakuna sehemu kwenye katiba polisi alipiruhusiwa kumdhuru mwananchi kwa silaha ya moto ikiwa mwananchi huyo hana silaha ya moto.

Kama wakaiwapiga risasi na wanachi hawana risasi wana la kujibu ,kama ni mawe kuna njia nyingi tu za kuwatawanyisha .

wewe unayajua mawe sawa sawa mkuu!!!

ukitaka dunia nzima ikutetee ingia barabarani match bila hata mwamvuli huku unaimba,halafu upigwe risasi.hapo kitanuka sio poa.
 
Polisi ongezeni askari wasio na uniform mitaani hapo mbona ilikuwa rahisi tu kuwadaka hao watupa mawe sio lazima wadakwe wote mnakamata wachache tu katika wengi wanaotupa mawe halafu mnawabana korodani na koleo hadi wakumbuke bibi zao waliofariki

Tatizo hapo in kutokuwa na askari wasio na uniform mitaani.Chukueni makomandoo wavalisheni nguo za mitaani waingie mitaani

Zanzibar mitaa mingi imebanana nyumba kuwadaka hao wahuni kazi ndogo mno sababu vichochoro vichache na vidogo rahisi kuwazingira pande zote na kuwabana kati

Sehemu korofi shusheni makomandoo wavalisheni hata hijabu na kanzu
Simple sana ukiwa nyuma ya keyboard , cha msingi watu wapewe wanachokitaka si kuleta figisu daily, we unadhani malawi walichofanya juzi tu hapa inashindikana?
 
Vipaumbele vyote ni lzm viguse maslai ya wananchi na sio vipaumbele vya watawala thus ndo jukumu la kulipa Kodi ili uletewe maendeleo, huwezi ridhisha wote lkn upimwa angalau 75% .Mtz gani aliyekaa chini akalalamika maisha yake ni magumu sababu hakuna ikulu mpya,Chato international,makao makuu Dom, ndege.Vipaumbele vya watawala sio vipaumbele vya wananchi.

Tatizo ndio hapo mie na wewe tunapishana..

Unakubali huwezi kuwaridhisha wote.. lakini hapo hapo unajitoa wewe katika kundi la wasioridhika na kutengeneza kundi jipya la watanzania wote milioni sitini wasioridhika.

Yaliyofanyika kuna watu wasio watawala wameridhika na wanaendelea kunufaika nayo. Kuhamia Dodoma ni matokeo ya watanzania wenyewe miaka ya ya sabini yeye anatekeleza tuu..

Ndege hazijaajiri wabunge na wanaopanda sio mawaziri tuu.. na barabara wanendelea kuzitumia mimi na wewe na wengine.. uwanja wa Chato sioni kwann umeleta taharuki sana... I swear.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Look yaani wameshindwa kuondoka hata na mtupa Mawe mmoja tu wakamwonyeshe cha mtema kuni? Hapo ilitakiwa waondoke na sampuli moja tu

Polisi wa bara wapelekwe Zanzibar kudhibiti huo uhuni askari hawezi.kimbia RAIA mtupa mawe akashindwa kuondoka nao hata wawili tu wa kuwafungulia kesi ya ugaidi waozee ndani miaka huku wakiwa wametiwa vilema vya maisha

IGP omba maelezo ya kueleweka kama hawakuondoka na gaidi hata mmoja hapo

Hao ni magaidi wakidakwa hiyo ndio kesi yao ni vikosi vya kigaidi vikishambulia vikosi vya serikali.Kusiwe na huruma hata chembe kwenye hilo
We unaota na wakati kumesha pambazuka ?
 
kama the Hague imemuacha mkapa mpaka amefariki kifo cha kawaida kabisa,haikuwahi kusema neno.unadhani mwaka huu mtakuwa mmewapa kitu gani,ili mtakapofanya uhuni mgongwe ianze kushughulika na nyinyi!!!!

nenda kachunguze ya nigeria yanavyoendelea,ndio utajua duniani hapa hakuna haki,bali una nini ili upate nini,that simple.
Mkapa hakwenda the Hague kwa sababu hakukuwa na Watanzania waliomshikia bango aende huko.

Sasa hivi watashikiwa bango ndani na nje ya nchi mpaka watafikishwa huko!. Waambie waue watu kisha waje waone!
 
Mpaka sasa najiuliza kwa nini awamu hii imeamua kumwaga damu za watu kwa kiwango hicho?

Hivi Magufuli haoni kuwa wanaomzunguka wandanganya ? Hata kama atarudi kwa nguvu lakini atastaafu na kuishi kwa shida sana.
Kenneth Kaunda mpaka sasa Yupo Hai. Anaheshimika na anatambulika kama Baba wa Taifa la Zambia. Hakutaka kuingiza Taifa lake kwenye Umwagaji wa Damu kwa kutaka abaki madarakani. Alikubali kuwa Chama chake kimeshindwa na maisha yanandelea . Zambia hawajapigana vita kwa sababu walizingatia haki.

Sasa Naona kila dalili ya JPM kuwanufaisha wachache wenye uroho wa madaraka na Mali ndani ya CCM lakini yeye baada ya kustaafu atakuwa na wakati mgumu sana mana Tanzania CCM inazidi kupukutika kwa kadiri wanzanilishi wake wanavyozidi kuzeena na wengine kutangulia mbele za haki. Ukiangali kwenye mikutano mingi ya CCM wengi ni wazee lakini Upinzani wengi ni vijana wadogo ambao wanaonekana kuupenda uoinzani kwa dhati bila kupewa fedha wala vyeo kama ilivyo kwa CCM ambao wengi wapo kwa sababu ni Chama chenye maslahi yote ya nchi hii.

Hua naangalia hata kwenye magrup ya kijamii wengi wanaoiunga mkono CCM ni wazee na watu wenye nafasi za madaraka au wanaonufaika kimadaraka moja kwa moja au ndu zao.

Hivyo ningekua ni Mimi ndio JPM nisingevuruga Mwafaka uliofanywa na watangulizi wake na kuifanya Zanzibar kuwa moja na kutulia kabisa .
Nisingedharau Katiba mpya iliyoanzishwa na mtangulizi wake kwa gharama kubwa sana.
Nisingevuruga Demokrasia iliyoasisiwa na watangulizi wake.

Kuvuruga Mwafaka wa Zanzibar, kuvuruga Katiba ya warioba ,Kuvuruga Demokrasia ni wazi kabisa kuwa Awamu hii haiwajali wananchi moja kwa moja na mahitaji ya mioyo yao zaidi ya kuwafanya kama watumwa kwenye nchi yao kwa sababu hayo ndiyo mambo yanayowafanya waishi kama watu waliostarabika.
Tunaletewa maendeleo Kikaburu kwa mitutu ya Bunduki .

Awamu ya Tano itampa wakati mgumu sana Rais wa awamu ya Sita hata kama atatoaka ndani ya CCM . Kama Ufisida uliofanywa na awamu zilizopita ulivyoisumbua awamu hii ndivyo pia na uvuniifu wa haki za watu na mauaji vitakavyoisumbua awamu ya sita. Awamu ya sita ikijaribu kurejesha muafaka itajikuta inatengeneza vikundi vya kulipa visasi,vinginevyo tuwe tumeamua rasmi kuwa Tanzania tunaendelea kutawaliwa Kwa mkono wa Chuma daima.
Awamu hii imeturudisha nyuma sana na itakuwa ni vigumu sana kuirejesha Tanzania kwenye umoja na mshikamano mana kuna watu wametumia miaka mitano yote kuhubiri mauaji kama alivyofanya Musiba na Kheri. Sasa watu wa vyama vingine nao wakaamua kuhamasishana na kupinga kuuawa wao tuu na familia zao kubaki zinateseka huku familia za wauaji ndani ya CCM zikipeta na kula raha kana waliomuua Alfonsi Mawazo ambao hawajakamatwa mpaka Leo. Hali inayosababisha watu wahisi kuwa hakuna Haki kwa wapinzani.

Rais wa awamu ya Tano amekua zaidi kama Mwenyekiti wa CCM kuliko Rais wa nchi kwa muda wote hata maendeleo ameyatoa kama vile wakoloni walivyotoa kwa malengo ya kwao huko Ulaya naye ametoa kwa baadhi ya maeneo kwa mikakati ya kushika dola tu na kujenga Chama chake lakini sio kama Jukumu la Rais na serikali inayochukua kodi kwa wananchi.

Kuna changamoto kubwa sana inayotunyemelea chini ya Awamu hii iliyojaa wapenda madaraka na watu katili wabinafsi wanaojiona kuwa hawana Mwisho wa kuishi duniani baada ya kuona mifuko yao imejaa mapesa na mali zimewazunguka kila kona na benki kuu ni Mali ya familia zao.
Hii ndiyo maana ya uzalendo wa kweli .
 
kama the Hague imemuacha mkapa mpaka amefariki kifo cha kawaida kabisa,haikuwahi kusema neno.unadhani mwaka huu mtakuwa mmewapa kitu gani,ili mtakapofanya uhuni mgongwe ianze kushughulika na nyinyi!!!!

nenda kachunguze ya nigeria yanavyoendelea,ndio utajua duniani hapa hakuna haki,bali una nini ili upate nini,that simple.
Kwa hiyo mkuu we unafurahia kutokuwepo haki
 
Mkapa hakwenda the Hague kwa sababu hakukuwa na Watanzania waliomshikia bango aende huko.

Sasa hivi watashikiwa bango ndani na nje ya nchi mpaka watafikishwa huko!. Waambie waue watu kisha waje waone!

eh haaya[emoji16][emoji16].

kaandamane maana the hague ipo kwa ajiri yako.
 
kwa ufupi tu muelewe ,autatokea fujo la kiuhakika,weka mbali alishababu,sisi wenyewe kwa wenyewe ,watakaopata tabu na shida ni wanachama wa CCM wanaojifanya wanagemea na kubebwa na polisi.

Hawa hawakai kambini wamo humuhumu na wanajulikana kwa idadi na hao polisi ndugu na jamaa zao hawaishi kambini wamo humuhumu mitaani na wanajulikana,iwe ndugu zake wapo mtwara yeye yupo mwanza wananchi wanawaelewa.
CCM wanaosheherekea sapoti ya polisi wajitathmni.
 
Askari siku zote ndo chanzo cha vurugu tendeni haki na sio kuumiza watu kwa maslai ya wasiowaongeza mishahara Wala kujali maslai yenu
Jukumu letu kubwa ni kutenda yale ambayo sheria inatutaka kutenda.

Pia, Kudeal na raia wanaofanya mambo ambayo sheria haiwaruhusu kufanya hayo tu.

Hii kusema, Raia usijaribu kuvuka mipaka ya haki yako. Ni bora Ukadai haki yako kwa lawful means kuliko unlwaful means ambako lazima ukutane na Law enforcers
 
Look yaani wameshindwa kuondoka hata na mtupa Mawe mmoja tu wakamwonyeshe cha mtema kuni? Hapo ilitakiwa waondoke na sampuli moja tu..
Mkuu haya maneno yako yanaonesha kwamba wewe ni Intarahamwe.Mtu mwovu. Shetani Mbaya sana wewe.Wale askari wametumi busara na uumilivu mkubwa sana. Wameondoka eneo la tukio baada ya kuona kwamba wataweza kujikuta wanamwaga damu sababu ya mihemuko.Ni heshima sana kwa Jeshi La POLISI kuwa na weledi wa kujua ni wakati gani kutumia nguvu na wakti gani kutumia hekima.
 
Back
Top Bottom