Swali zuri lakini siyo sahihi; kwani China wananchi wote wana umeme, elimu, makazi na madawa? India yenyewe wanajenga ile ring ya barabara kuzunguka Delhi lakini haina maana India watu wote wanaishi peponi. Wamarekani walipojenga hizi interstate highways miaka ya 1950s haina maana watu wote wa Marekani walikuwa wanaishi maisha mazuri - wengi walikuwa hata haki ya kupiga kura hawakuwa nayo! Kuwepo kwa matatizo mengine siyo sababu ya kutofanya mambo makubwa! Vinginevyo, tusijenga kabisa barabara au madaraja mengine hadi tuhakikishe kila mtu ana elimu, nyumba na chakula kizuri.
Wakuu,
Kwa jinsi nilivyomuelewa huyu MMKJJ lengo lake haswa ni kutaka kutuamsha waTanzania ili tuanze kujiamini tena na kuanza kufikiria kuwa tunaweza kufanya mambo makubwa sisi wenyewe. Kwa kweli tangu Mwalimu aondoke tumebaki kama watu waliodumaa na tuliokosa kujiamini....:A S-coffee:
China hakuna ufisadi baba,Huko wakikukamata tu wanakunyonga ,Hawa Kima EL,RA,AC ingekuwa ni china ingekuwa historia tu
I just refuse to give in to defeatism! I really believe if we wanted to we could do it. It's just too bad that some people don't have the will.
If we wanted we could, lakini tunaongelea scope gani? Tunaongelea kutenga hela leo na kutafuta mkandarasi wa kichina au tunaongelea kubadili mentality nzima kuhusu maendeleo, na sio kutenga hela tu, bali kuandaa kizazi kizima kwa kukisomesha na kuboresha uchumi ili kusudi hata kukijenga daraja hili miaka 15-30 ijayo, tunanyanyua miundombinu ya nchi nzima, sio kujenga daraja moja tu, na ma engineer wa kutosha tunao kwa sababu tunaanza kwa kuongeza vyuo vikuu kwanza?
kweli tunataka kuanza kujenga daraja wakati ma engineer wa kulikarabati hatuna?
Ukitaka kukimbia kabla ya kutambaa utaumia.
Kabla ya kuota kujenga midaraja ya ajabu somesha watu wako angalau uwe na ma engineer wa kulifanyia ukarabati, sio unajengewa daraja bovu na wachina huku wakijua wazi huna hata ma engineer wa kulihakiki, na utawaita kila baada ya kiaka mitano na kuwalipa kufanya ukarabati.
Kuwa ambitious ni kitu kizuri, kujua uwezo wako ni kitu kizuri zaidi.
Ama sivyo unaweza kwenda juu ya PPF Towers huku unaimba wimbo wa R. Kelly "I Belive I Can Fly...." ukajirusha, na kujikuta unaanguka na kufa.
Kila kitu kwa scale. Mie ningeona post ina maana kama tungeonyeshwa jinsi tunavyopaswa kuona haya kwa Wachina kujenga daraja hilo kabla ya sie kujenga daraja la Kigamboni. Hapo unaongea kwa kutumia proportionality.
Lakini hizi habari za kumlinganisha tembo na sisimizi (ashakum) zinatoka katika kujenga inspiration, zinatupeleka katika a total disregard for reality.
Unatambaa kwanza kabla ya kukimbia. Let's look at goals that are realistically within our reach. Sio tunaumia kwa sababu hatujafika mwezini wakati kuamisha mji mkuu kwenda Dodoma tumeshindwa.
If we wanted we could, lakini tunaongelea scope gani? Tunaongelea kutenga hela leo na kutafuta mkandarasi wa kichina au tunaongelea kubadili mentality nzima kuhusu maendeleo, na sio kutenga hela tu, bali kuandaa kizazi kizima kwa kukisomesha na kuboresha uchumi ili kusudi hata kukijenga daraja hili miaka 15-30 ijayo, tunanyanyua miundombinu ya nchi nzima, sio kujenga daraja moja tu, na ma engineer wa kutosha tunao kwa sababu tunaanza kwa kuongeza vyuo vikuu kwanza?
kweli tunataka kuanza kujenga daraja wakati ma engineer wa kulikarabati hatuna?
Kwani ni wahandisi wangapi tutahitaji kulikarabati hilo daraja?
Hii mentality ya kujiona kuwa hatuwezi kufanya vitu flani flani au hatustahili kuwa na vitu flani flani ndiyo moja ya mambo yanayotukwamisha katika maendeleo.
Uthubutu wa kujenga daraja kama hilo kwangu mimi nauchukulia kama ni confidence booster. Na maendeleo huwa hayaji hivi hivi tu bila kuthubutu kufanya yale ambayo yanaonekana kama hayawezekani.
I believe and I know we can do it.
Hivi kinachokutisha wewe ni gharama au nini?
Maana sababu ya kujenga ipo wazi kabisa, na uwezo tunao pia..
Tunachosema hapa ni kwamba pamoja na kwamba tunahitaji shule, vyuo na railways..
Tunahitaji daraja la umoja kutoka zanzibar hadi tanganyika..pia
Ni swala la kuajdili ipi ianze..kwangu mimi zote zina umuhimu ulio sawa lolote litakaloanza ni sawa tu..
tujenge daraja bana
Nadhani hapa ndio tatizo lilipo; Tanzania ina maenjinia wengi tu - tunayo madaraja tayari mengi na mengine mengi yanatengenezwa. Tumekuwa tukijenga madaraja toka wakati wa uhuru hadi leo hii. Hatuanzi kwenye sifuri. Na kinyume na mtazamao siwaangalii Watanzania kama watu wasioweza, wasio na kitu, au wasiokuwa na sababu ya kujaribu. Tulipojenga reli ya Tazara mapingamizi yaliyotolewa ni kama haya - ni ndefu, ni fedha nyingi, nchi maskini n.k na hii ilikuwa in the 1970s? Sasa kama tuliweza kuingia mradi huo mkubwa miaka hiyo - it was the largest construction project in Africa chini ya Sahara wakati ule - leo kinatushinda? Tumejenga dams kubwa tu wakati mahitaji ya umeme hayakuwa makubwa hivyo. Sasa leo tukisema tujenge dam ya Stielger's Gorge kwa bilioni 3 dola unaweza ukasema hakuna sababu kwa sababu ni mradi mkubwa sana!
Hoja pekee ambayo tunaweza kukubaliana - partially - ni hoja ya return on investment au kama "inalipa". Lakini hii pia siyo hoja sahihi, wakati mwingine si lazima kuangalia miradi hii kwa maana ya matumizi ya fedha tu lakini pia on utilitarian principle kwamba tunahitaji kwa ajili ya kurahisisha usafiri tu - siyo kwa ajili ya fedha, siyo kwa ajili ya kulipa n.k kwamba kulipa kwake ni kuwa ni kuunganisha sehemu mbili za nchi moja na kuwarahisishia wananchi usafiri baina yao. Inawezekana hili lisiwe kubwa hivyo kwa sababu halina "economic value" lakini kwangu naamini ni sababu tosha ya kuunganisha.
Mimi ninaamini kuwa tunaweza na tunayo sababu; siyo gharama kubwa hata kama ikiwa dola bilioni 5 bado ni ndani ya uwezo wetu. Umeuliza kuwa na space program well kwangu mimi sina tatizo mbona Nigeria wanayo au kwa sababu Nigeria nayo imewaondoa watu wake wengi kutoka kwenye umaskini ndio maana imefanikiwa hivyo? Afrika ya Kusini wamejenga treni ziendazo kasi ni kwa vile watu wake wengi wametoka kwenye umaskini? Morocco walikuwa wamepanga kuanza high speed train ni kwa vile wao ni matajiri sana? Iraq wanataka kutengeneza high speed train toka Baghdad hadi Basra ni kwa vile wanaamani zaidi na hawana maskini?
Sasa nikija na pendekezo la kuwa na high speed rail kati ya Dar na Tanga na kubadilisha existing tracks kuwa high speed rail ambapo ni chini ya kilomita 150 tu utasema ni matumizi mabaya ya fedha wakati maelfu ya watu wa Tanga wanashi katika nyuma duni? Je tukiamua kutengeneza high speed rail kati ya Dar na Morogoro itakuwa ni kutamani makubwa sana?
Binafsi naamini Watanznai awanatakiwa kutamani makubwa na kwenda kuanza kufanya makubwa. KUna vitu tunahitaji kuvipanga na kuanza kuvifanya sasa sio miaka 10 au 15 ijayo. I too refuse to succumb to defeatism na kujiona duni kiasi kwamba hata kutamani mambo makubwa tunatakiwa kuogopa.
Tanzania:
Ijenge daraja kati ya sehemu zake mbili za Muungano au hata kati ya Pemba na Unguja na kuunganisha visiwa hivi.
Ijenge a high speed rail kati ya Dar na Tanga na Dar na Moro na baadaye a high speed rail kati ya Dar -Mwanza!
Sasa niambie kwa nini daraja hili liwe na umuhimu kuliko hiyo mipango mingine yote?
I could see us doing a project this big if the survival of our nation depended on this. Like say we are some Burkina Faso and are threatened with desertification and we need to divert some river for this many miles, because if we don't do it the nation risks going extinct.
Sankara did put his people to work similarly. I would find that admirably.
Lakini kujenga daraja expensive hivi wakati kuna alternatives kibao? Nchi yenye priorities nyingine kibao? Bila kuonyeshwa the need? the technical feasibility? the long term maintenance projection?
Ukinunua printer usiangalie bei ya printer tu, unaweza kukuta printer bei rahisi sana, lakini kila baada ya miezi michache inabidi uinunue upya hiyo printer kwa sababu catridge zake mbili tu ni bei ya printer nyingine.
Ndiyo maana nawabana washabiki wa ujenzi huu watoe namba hapa, sio kuongea katika a utopia vacuum.
Hakuna aliyesema hayo mambo mengine (au mipango kama ulivyoiita wewe) hayana umuhimu. Na haimaanishi kama tuki-embark kwenye project kama hiyo basi mambo mengine yote yatasimama! La hasha!
Kuna mambo mangapi sasa hivi ambayo yanaendelea kwa pamoja? And what makes you think that if we embark upon such a project everything else will be put on the back burner? Hatuwezi kuacha kufanya mengine kisa tu eti tunajenga daraja la kuunganisha Tanzania bara na Visiwani.
Na kuhusu wahandisi, kitivo cha uhandisi cha chuo kikuu cha Dar Es Salaam kimekuwepo kwa zaidi ya miaka 35 sasa. Yaani katika miaka yote hiyo unataka kuniambia kweli hatuna wahandisi wenye sifa za kuweza kusimamia mradi kama huo na baadae kuweza ku oversee its maintenance? You don't need hundreds of thousands of engineers to do that.
Priorities, and more priorities! Mambo kama haya wala yasingekuwa issue kama tungekuwa na strategic plannings.Kulinganisha daraja hili na mradi wa umeme, kilio cha wengi Tanzania, ni kukosa kuelewa concept nzima ya utility.
Mimi kilio changu hapa ni kuona kila mradi unakuwa na utility. Habari za kudumisha muungano and all ni nzuri, lakini zije under the auspices of economic utility. Ukitaka kwenda na utopian political projects ndipo hapo utakapotaka tuwe na space project wakati watu hawana umeme.
Kabla ya kujenga daraja na high speed rail jenga na dumisha efficiency bandarini Dar, ondoa msululu wa magari Dar, jenga daraja kwenda Kigamboni, jenga mji Kigamboni, vunja mbavu za mbwa Dar ujenge nyumba za uhakika, weka system ya ,maji na umeme ya kueleweka nchini, then unaweza kuongelea some fancy footwork.
Wewe unacheza mpira goli hujafunga unataka kuleta show za chenga?
Kiranga hapa unataka kutupa sisi wengine jukumu lisilo letu; mwisho utatutaka twende tukapime kina cha maji, tupige hesabu hadi ya spana zitakazotumika. Kimsingiunatutaka tuwe waandika project ya mradi huo. Hilo siyo lengo la mada hii hata kidogo. Lengo ni kuchokoza fikra zetu kuona kitu kama hiki kinawezekana kufanywa na sisi? Hata kwa kuhusisha Wamarekani,Wachina na Wajerumani kwani wote waliojenga uarabuni ni waarabu watupu au vyoote vinavyojengwa China vinajengwa na Wachina peke yao?
Hatuwezi kutoa namba kwa sababu sisi siyo wajenzi au wataalamu wa ujenzi wa madaraja! Kilichotolewa hapa ni wazo la udadisi tu; sasa tukikubaliana au wazo likikubaliwa ndio mambo ya feasibility studies (visibility studies according to somebody else) itafanyika, ndio EIA nayo itafanyika, mambo ya bajeti yatafanyika, n.k Siyo lengo la thread hii ndogo hapa kujaza vyote vilivyomo kwenye mradi mkubwa kama huo! Moja ni kwa sababu siyo wataalamu wa madaraja na pili hatuna resources za kuweza kukuridhisha na details zote hizo unazotaka ili kukushawishi.
Ndiyo maana nawabana washabiki wa ujenzi huu watoe namba hapa, sio kuongea katika a utopia vacuum.