DOKEZO Responded Zanzibar iungwe na Bara kwa Daraja - Wazo Jipya

DOKEZO Responded Zanzibar iungwe na Bara kwa Daraja - Wazo Jipya

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kiranga, kina cha bahari yetu kinajulikana; unaweza kugoogle hiyo; suala la teknolojia kama alivyosema companero ipo tayari - hatuhitaji kuinvent new technology. Suala kubwa tukiamua litakuwa ni la mazingira zaidi kuliko kitu kingine chochote.

Kwa nini usi google wewe na kutuonyesha kina hapa?

Teknolojia iliyopo unayoisema ipo ni ipi? Uchina kuna teknolojia ya madaraja ya bamboo, nayo ni teknolojia pia, sasa hiyo yenu mnayoongelea ni ipi?

Hilo swala la mazingira unalolisema ushalichunguza? Au unapendekeza tu bila uchunguzi?
 
naona leo unakana mambo ya forward and backward economic linkages ya investment za infrastructure mnazotuhubiria kila siku

ps. barabara kuu ya dar arusha ilipotolewa kwetu na kupelekwa mkomazi-hedaru-same mabadiliko makubwa yalitokea!

Nimehutubia wapi ku commit kwenye project isiyo na specifics? Nionyeshe hapa.
 
Umesahau 20/80 formula. Kujenga 20, Maintanance 80%. Watanzania wasivyopenda kufanyia maintanance, investment yote itapotea.

haitakuwa 100% toll free, wenye uwezo mkubwa mtakatwa zaidi ili daraja liji-maintain,mkishindwa,lol, 'mtapiga mbizi'
 
Nimeiona Kindle Fire. Nasubiri dili.

Huja-file tax returns wewe? Kindle Fire mpya inagharimu $199.00 ukiongeza na kodi inakuwa kama kwenye $213-$220.00 hivi....

Ila unaweza ukapata dili ebay....
 
Nimehutubia wapi ku commit kwenye project isiyo na specifics? Nionyeshe hapa.

it all start with an idea, hili suala ni wazo - now build on it, find the details if you can't wait for those who will find them
 
naona leo unakana mambo ya forward and backward economic linkages ya investment za infrastructure mnazotuhubiria kila siku

ps. barabara kuu ya dar arusha ilipotolewa kwetu na kupelekwa mkomazi-hedaru-same mabadiliko makubwa yalitokea!

Mabarabara yanaleta mabadiliko makubwa. Na kwa maoni yangu binafsi serikali ingefumbia macho mambo fulani na kuangalia infrastructures kwanza.
 
Huja-file tax returns wewe? Kindle Fire mpya inagharimu $199.00 ukiongeza na kodi inakuwa kama kwenye $213-$200.00 hivi....

Ila unaweza ukapata dili ebay....

Kila mwaka inabidi nirudishe tax. Nimeandikisha dependents 7. Nitapata dili tu.
 
Umesahau 20/80 formula. Kujenga 20, Maintanance 80%. Watanzania wasivyopenda kufanyia maintanance, investment yote itapotea.

Tukitaka kuendelea itabidi tubadilike kabisa tofauti na tulivyo sasa na baadhi ya mabadiliko tunayohitaji kuyafanya ni kuacha uoga na kuwa wajasiri wa kuthubutu kufanya mambo ambayo tunaona kama vile hatuwezi kuyafanya.

Hilo la maintenance nalo neno.
 
Kiranga...kwa nini unadhani ujenzi wa hilo daraja utazorotesha ama kusimamisha kabisa mambo mengine?

Sijasema kwamba ujenzi wa daraja hili utasimamisha kabisa mambo mengine.

Ninachosema ni kwamba, katika uchumi, kwa sababu hatuna "unlimited resources", ukiamua kununua kitu kimoja, unapunguza uwezo wako wa kununua kingine.

Hata mtu mwenye fedha ziso mwisho ana opportunity cost kwa sababu at the end of it all, akiamua kuangalia movie inawezekana aka forego kwenda dinner, hawezi kwenda dinner kwenye restaurant fulani na kwenda movie kwenye theatre fulani at the same time.

Kwa hiyo kuamua kujenga daraja hili, ni kunyima wengine shule, zahanati, barabara etc, kwa sababu hatuna "unlimited resources".

Ndiyo maana ni muhimu tuchunguze na ku prioritize projects kwa details, ili kusudi tukiamua kujenga kinu kipya cha kufua umeme tujue kuwa kwa kujenga hivi tunatumia fedha zetu in the most desirable way, kinu kitafanya kazi kwa watu wengi sana, kitakuza uchumi wa nchi, watoto watapata mwanga wa kusoma, viwanda vitazalisha zaidi,tutauza umeme mpaka nje, tutarudisha hela kwa muda mfupi zaidi na pengine hata tukaweza kuzizungusha fedha hizo hizo tukaamua kujenga daraja.

Sio tunaamua kujenga daraja halafu tunajikuta sio tu daraja halirudishi hela, bali pia linanyonya hela zaidi kwa kuhitaji matengenezo ya gharama ambayo hatuna hata wataalam wa kukidhi, inabidi tuwalipe wachina.

Kwa hiyo utaona kupangilia nini cha kuanza na nini cha kufuata ni muhimu sana.
 
Mabarabara yanaleta mabadiliko makubwa. Na kwa maoni yangu binafsi serikali ingefumbia macho mambo fulani na kuangalia infrastructures kwanza.

Miundombinu ni linchpin ya maendeleo! Na ni muhimu sana kui-diversify.
 
Kila mwaka inabidi nirudishe tax. Nimeandikisha dependents 7. Nitapata dili tu.

kweli u can take mbongo out of bongo but you cannot take ubongo out of mbongo, kwa mwendo huu change is not gonna come hata ukijengewa madaraja kutoka kiwanja hadi bongo!
 
Hapana,

Mie ninachosema nikwamba kabla ya kujenga daraja angalau watoto waende shule kesho daraja liwe na wahandisi wa kulikarabati wa kutoka nyumbani.

Wewe kwa kutaka kujenga daraja bila ya kuwa na bajeti ya kutosha ndiye unayekataza watoto kuenda shule.

Tayari kuna watu wengi wanajifunza na wamejifunza uhandisi; tuna wahandisi wengi sasa hivi kuliko wakati tunajenga Tazara, au kufanya upanuzi wa bandari mbalimbali. Leo hii hatujengi daraja kubwa wala hakuna mradi mkubwa unaoendelea nchini je watoto wote wanaenda shule? Leo hii hatujaanza hata kujenga daraja la Kigamboni je watoto wote wanasoma kwenye shule nzuri? Sasa kinachowafanya watoto wengi wasiende shule au kuwa katika shule nzuri ni nini? of course haiwezi kuwa daraja!

Sasa hatuwezi kujisikia hatia kwa kupendekeza mradihuu ati tutasababisha watoto wasiende shule; well nani anayesababisha watoto wasiende shule leo? Tuache kujenga barabara, tuache kujenga mabwawa ya umeme, tuache kujenga ofisi mpya kwa sababu kwa kufanya hivyo tutasababisha watoto wasiende shule?

Lakinivile vile ni kana kwamba unataka tuone kuwa kuna choice mbili tu - ama kujenga daraja la Zenji au watoto kwenda shule - this is a fallacy of false dilemma. Kwanini tusifikirie kuweza kufanya vyote viwili na zaidi kwa kutumia resources tulizonazo? Kwa mfano, tukitenga dola bilioni 1 kwa mwaka kwa ajiili ya ujenzi wa daraja hilo kwa miaka minne ijayo (jumla ya dola bilioni 4) unafikiri hatutaweza? In comparison, mpango "wa maendeleo wa miaka mitano" uliopitishwa mwaka jana iliyopita ulikuwa unafikiria kutumia shilingi trilioni 42.6 katika miaka mitano (wastani wa trilioni 8.5 kwa mwaka!).

Sasa tayari tuna mpango wa trilioni 42.5 kwa miaka mitano, kumbuka bajeti yetu ya mwaka jana peke yake ilikuwa ni kama trilioni 13 tu! Sasa kutenga trilioni 1 kwa mwaka kwa ajili ya daraja hili ni tatizo la kusababisha shughuli nyingine zote nchini zisimame? kwamba tukitenga trilioni 1 kwa mwaka shule zitafungwa, polisi watakosa kazi, umeme hautalipwa n.k? Really? Kweli tunafikiria kwa vile tutakuwa na mradi huu mkubwa hatutaweza kweli kumudu mambo mengine?

Nadhani we are understimating our own potential to transform our beloved country and catapult it into beauty of greatness. I for one, I don't.
 
Sijasema kwamba ujenzi wa daraja hili utasimamisha kabisa mambo mengine.

Ninachosema ni kwamba, katika uchumi, kwa sababu hatuna "unlimited resources", ukiamua kununua kitu kimoja, unapunguza uwezo wako wa kununua kingine.

Hata mtu mwenye fedha ziso mwisho ana opportunity cost kwa sababu at the end of it all, akiamua kuangalia movie inawezekana aka forego kwenda dinner, hawezi kwenda dinner kwenye restaurant fulani na kwenda movie kwenye theatre fulani at the same time.

Kwa hiyo kuamua kujenga daraja hili, ni kunyima wengine shule, zahanati, barabara etc, kwa sababu hatuna "unlimited resources".

Ndiyo maana ni muhimu tuchunguze na ku prioritize projects kwa details, ili kusudi tukiamua kujenga kinu kipya cha kufua umeme tujue kuwa kwa kujenga hivi tunatumia fedha zetu in the most desirable way, kinu kitafanya kazi kwa watu wengi sana, kitakuza uchumi wa nchi, watoto watapata mwanga wa kusoma, viwanda vitazalisha zaidi,tutauza umeme mpaka nje, tutarudisha hela kwa muda mfupi zaidi na pengine hata tukaweza kuzizungusha fedha hizo hizo tukaamua kujenga daraja.

Sio tunaamua kujenga daraja halafu tunajikuta sio tu daraja halirudishi hela, bali pia linanyonya hela zaidi kwa kuhitaji matengenezo ya gharama ambayo hatuna hata wataalam wa kukidhi, inabidi tuwalipe wachina.

Kwa hiyo utaona kupangilia nini cha kuanza na nini cha kufuata ni muhimu sana.

kuna vitu haviwezi kusubiri hasa vile ambavyo social and economic return yake ni kubwa sana!

eg kuifanya dar kuwa hub ya ndege (inayoshindana na johannesburg, nairobi na addis) na kuifanya atc ipambane na kq,saa na ethiopian airline economic return yake ni kubwa mno na itatrickle down to zahanati, shule n.k!
 
haitakuwa 100% toll free, wenye uwezo mkubwa mtakatwa zaidi ili daraja liji-maintain,mkishindwa,lol, 'mtapiga mbizi'

Mimi nipo viwanja hapa na Governor wetu anapandisha tax kila siku kwa kufanyia maintanance barabara na madaraja. Nimejiunga na Tea Party.
 
it all start with an idea, hili suala ni wazo - now build on it, find the details if you can't wait for those who will find them

Demanding details is building the conversation in the right direction.

Kesho keshokutwa tutapata makatibu wakuu wa wizara kutoka watu wa JF hapa, wataletewa mikataba rosy na "economic hitmen" wa world bank and the rest of these predators, tunataka wa sign mikataba bila details?
 
huku nyanda za kuu kusini kwenye milima ya kilolo nilikutana na lori la mbao limekwama siku 3 kisa barabara mbovu, mmiliki akawa anapiga pombe tu maana hana jinsi, ndio huu upumbavu wa kuzuia swift movement unaotulostisha!
 
Tukitaka kuendelea itabidi tubadilike kabisa tofauti na tulivyo sasa na baadhi ya mabadiliko tunayohitaji kuyafanya ni kuacha uoga na kuwa wajasiri wa kuthubutu kufanya mambo ambayo tunaona kama vile hatuwezi kuyafanya.

Hilo la maintenance nalo neno.

right on.
 
Mimi nipo viwanja hapa na Governor wetu anapandisha tax kila siku kwa kufanyia maintanance barabara na madaraja. Nimejiunga na Tea Party.

du ujamaa umekufrustrate kiasi hicho mpaka umejiunga na chama cha chai! by the way palin wenu kaishia wapi?
 
Back
Top Bottom