DOKEZO Responded Zanzibar iungwe na Bara kwa Daraja - Wazo Jipya

DOKEZO Responded Zanzibar iungwe na Bara kwa Daraja - Wazo Jipya

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Baada ya uchaguzi mkuu wa 2005 na baada ya kuapishwa kuwa Rais, JK alikuja Washington DC. Mi sina mapenzi na viongozi lakini jinsi watanzania walivyokuwa na imani naye wakati hule ilibidi niende kwenye mkutano.

kwenye mkutano alisema kuwa Mwinyi alipoondoka aliacha kama dollar 800 Milioni katika reserve ya taifa. Na Mkapa aliacha kama dollar bilioni 2 katika reserve. Watu wakalipuka kwa vifijo. Na mimi bila kujijua nikajiunga kwenye frenzy ya kushangilia. Lakini akili ilipotulia ikabidi nigawe 2 Bilioni kwa population ya watanzania. Nikaona jamaa anasema upuuzi nikaondoka.

Thamani ya daraja mnalotaja ni dollar 1.4 Bilioni. Hii ni reserve ya Tanzania. Na kulikamilisha itabidi nchi iingie madeni makubwa.

Kama mafuta yamegunduliwa mradi huu unaweza kufanyika. Lakini kwa sasa itabidi ziwe ndoto.


We lose 1 billion USD kila mwaka through corruption; mwaka 2008 tulitengeneza stimulus package ya dola bilioni moja kwa ajili ya kilimo; posho za watumishi mbalimbali kwa mwaka huu peke yake ni karibu shilingi trilioni moja! Unaweza kuona kuwa suala nipolitical will and leadership tu siyo resources.
 
Kakisiwa kenyewe kako wapi kakupokea gari 5000 - 10000 (future)? mnataka kwenda kukajaza kale kakisiwa ufisadi tu, uliokuwa exported sasa unatosha. Hatutaki daraja. Kama mnaogopa kuja kwa boti pandeni ndege, kama hamna uwezo msije.

Kawekeni daraja Pangani mpate shortcut ya kuja Dar mkitokea Arusha na mtapa watalii wengi wataoenda Saadani kutazama tembo wanaoogelea baharini.
 
Kakisiwa kenyewe kako wapi kakupokea gari 5000 - 10000 (future)? mnataka kwenda kukajaza kale kakisiwa ufisadi tu, uliokuwa exported sasa unatosha. Hatutaki daraja. Kama mnaogopa kuja kwa boti pandeni ndege, kama hamna uwezo msije.

Kawekeni daraja Pangani mpate shortcut ya kuja Dar mkitokea Arusha na mtapa watalii wengi wataoenda Saadani kutazama tembo wanaoogelea baharini.

It won't hurt if you just listen.
 
Mbona wa Finn wanaotufadhili kila mwaka hawajajenga daraja kutoka Helsinki mpaka Tallin? Hawana uwezo?

Ndo maana nikauliza kama hili la kwetu ni "Daraja la muungano."

Nadhani sikueleweka.
 
Kiranga,Zakumi,Companero,Nyani Ngabu,jmushi1,

..nadhani Mwanakijiji is daring wa-Tanzania to think big and come up with an ambitious project itayatukwamua toka hapa tulipo.

..nakumbuka kusoma kuhusu jinsi gani mradi wa interstate highways za USA uliovyosaidia ktk kukuza biashara na uchumi wa Marekani.

..wa-Tanzania na sisi tunatakiwa tuibue mradi mkubwa ambao utasaidia kuinua sekta nyingine hapa nyumbani.
 
sasa kushindwa kutoa hizo ameamua kudismiss the whole idea kwasababu hatujaweza kuweka hesabu zote na undani wa mpango mzima ili kujua kama unafaa au la!

Tafadhali tofautisheni mtu anayekuja hapa na kutaka michoro ya daraja na nitty gritties za construction na mtu anayeuliza vitu general kama kina cha channel na aina gani ya daraja mnapendekeza kujenga.

Mnakuwa hamnitendei haki kwa ku suggest kwamba nataka nitty gritty details ambazo hamna, najua mmesema ninyi si wataalam kwa hiyo sitegemei mnichoree model na vipimo vitakavyoonyesha wind resistance ya daraja.

Nimeomba very basic general aspects za project. Mnajua kina cha channel nasehemu daraja litakapopita? Companero kaniletea mramani una vitalu vya mafuta as if vitalu vya mafuta ndio swali nililouliza.

The devil is in the details. Ukitoa pendekezo uwe tayari ku justify pendekezo lako with data. Hapa unaonekana kama vile umekurupuka kupendekeza kitu ambacho hujakifanyia hata the very basic of researches, ile ya generalist tu, nothing special.

Until you build your case, this bridge will remain a white elephant for prudent people who choose to err on the side of caution.

Especially because there are so many other projects that are competing for the same money and are backed by people with justifying figures.
 
Tuna VITU VINGI SANA VYA KUFANYA VIPAUMBELE, KWA SASA HATUHITAJI HILO DARAJA!

Mfano kujenga na kuboresha bandari ya MTWARA na TANGA ambazo zitatupa impact kubwa sana za kimaendeleo KULIKO HILO DARAJA, kufufuliwa miundo mbinu ya treni na kuboreshwa barabara zetu nyingi hazina lami nyingine ni mbovu kabisa, wnafunzi hawana madawati, mabweni, maabara....

ZANZIBAR ina watu MILIONI MOJA TU, hilo daraja litatupa impact gani kama si hasara kwa sasa??

LAKINI TUKIIMARISHA RELI NA KUJENGA HIZI BANDARI ZA MTWARA NA TANGA WATU ZAIDI YA MILION 20 WATANUFAIKA!!

WAZO LA DARAJA LA MUUNGANO ZURI LAKINI LIJE BAADAYE SAANA..
 
Kiranga,Zakumi,Companero,Nyani Ngabu,jmushi1,

..nadhani Mwanakijiji is daring wa-Tanzania to think big and come up with an ambitious project itayatukwamua toka hapa tulipo.

..nakumbuka kusoma kuhusu jinsi gani mradi wa interstate highways za USA uliovyosaidia ktk kukuza biashara na uchumi wa Marekani.

..wa-Tanzania na sisi tunatakiwa tuibue mradi mkubwa ambao utasaidia kuinua sekta nyingine hapa nyumbani.

Hakuna tatizo kuwa daring, hakuna tatizo ku think big.

Lakini ku think big ni lazima u adopt the right project, na ku adopt the right project lazima ucheze na details, otherwise unaweza kutaka kujaza mi castle ya Kireno kwa mvinyo adimu kama Mobutu, that was "big", but it was wasteful.

Mimi ninacho demand hapa, think big in the right direction.

And unless one shows us this makes sense with the details, including the hows and whys, including return on investmen and impact to economic growth, what you may be thinking as thinking big may actually be a self-sacrifical lamb for the economic hitmen.

Ukisoma "Confessions of An Economic Hitmen" utaona ujinga wa nchi masikini kujiingiza katika miradi mikubwa bila kuangalia details kwa umasikini.

Na anavyaoandika Mwanakijiji hapa anakuwa kama an unintentional self-wounding economic hitman.

Anawafungia goli hitmen wa World Bank bila kulipwa, na Watanzania wengine wanashangilia. Miaka kumi baada ya daraja kujengwa daraja likakosa traffic na deni ku mount, watu wanaanza kulalama "ayaa weeee, tumeboogie step kama IPTL"

When will we learn to value details?
 
Nimeomba very basic general aspects za project. Mnajua kina cha channel nasehemu daraja litakapopita?

Kina cha maji si general kihivyo. Huwezi kujua bila kuzama na kupima. Sasa unategemea Mwanakijiji awe anajua vina vya sehemu zote ambazo daraja litapita?
 
Kina cha maji si general kihivyo. Huwezi kujua bila kuzama na kupima. Sasa unategemea Mwanakijiji awe anajua vina vya sehemu zote ambazo daraja litapita?

Sasa kama hajui kina hawezi kujua challenge ya kujenga ikoje na teknolojia ya kutumia ni ipi, na kama hajui challenge hajui gharama, kama hajui gharama na anataka daraja lijengwe.... hatari!!
 
Sasa kama hajui kina hawezi kujua challenge ya kujenga ikoje na teknolojia ya kutumia ni ipi, na kama hajui challenge hajui gharama, kama hajui gharama na anataka daraja lijengwe.... hatari!!

Yeye katoa wazo. Wazo lake kubwa si uamuzi. Wewe unageuza wazo lake kuwa kama vile ndiyo uamuzi ambao umeshafanywa. Hapo ndipo unapokosea!

Na ukirudia kusoma bandiko la Mwanakijiji utaona kuwa daraja kalitumia kama mfano tu wa mawazo makubwa na yenye uthubutu ambayo viongozi wetu wanaweza kuja nayo

Maswali ya Kutafakari:
Je kuna uongozi wowote ndani ya CCM wenye mawazo ya namna hii au mwitikio wa kwanza 'hatuwezi?

Na kweli, mwitikio wa kwanza wa baadhi ya watu ni kwamba "hatuwezi"!!
 
Yeye katoa wazo. Wazo lake kubwa si uamuzi. Wewe unageuza wazo lake kuwa kama vile ndiyo uamuzi ambao umeshafanywa. Hapo ndipo unapokosea!

Katoa wazo ambalo limekuwa backed up na siasa tu

g. Bara nako kutanufaika sana na kufunguliwa kwa njia hii mpya.
 
Hivi mnafikiria huko China hakuna ufisadi? Au China viongozi wote ni wazuri na wazalendo?
Mzee Mwanakijiji, unaongelea kuhusu Tanzania hii ya CCM au ya kufikirika? Tanzania unayotaka ijenge muungano bridge!!!!! Imeshindwa kufinance service ya Kiwira Coal mine izalishe mw 200 wakati nchi inaupungufu wa mw 150, imeshindwa kuthubutu hata kuanza kwa upembuzi yakinifu wa stigglers Gorge inayohisiwa kuwa na uwezo wa mw 2000, Liganga imepata ufadhili wa China, Leo hii bidhaa zote za viwanda bei juu, lita ya maji ya kunywa inakimbizana bei na lita ya petrol. Tanzania ipi, hii inayoshindwa kuwalipa stahiki zao wastaafu wa EAC, hii inayochemsha kulipa malimbikizo ya mishahara ya walimu, hii yenye malumbano ya mikopo ya elimu ya juu. Naheshimu sana ideas zako, na hii idea ni one of the best, cause inawezekana kwa watu huru. But kwa hawa mental slaves, ambao wanaamini hata kutokomeza maralia tunahitaji wajomba, never till the end of time.
 
Wengi wetu humu hatuna hata chembe ua uthubutu wa kufiri na kujaribu kufanya makubwa ambayo hayajawahi kabisa kufanyika nchini.

Na bila kubadili fikra zetu tutaendelea kula mavumbi na kuishi kwenye vijumba vya udongo huku wenzetu wakijenga vikwangua anga vyenye condos kibao.
 
Tuna uwezo wa kujenga daraja mpaka z'bar, hata shimbo tu anaweza. Lakini sababu za kufanya hivyo hatuna kwa sasa, labda vizazi vijavyo.
 
Back
Top Bottom