Tayari kuna watu wengi wanajifunza na wamejifunza uhandisi; tuna wahandisi wengi sasa hivi kuliko wakati tunajenga Tazara, au kufanya upanuzi wa bandari mbalimbali. Leo hii hatujengi daraja kubwa wala hakuna mradi mkubwa unaoendelea nchini je watoto wote wanaenda shule? Leo hii hatujaanza hata kujenga daraja la Kigamboni je watoto wote wanasoma kwenye shule nzuri? Sasa kinachowafanya watoto wengi wasiende shule au kuwa katika shule nzuri ni nini? of course haiwezi kuwa daraja!
Sasa hatuwezi kujisikia hatia kwa kupendekeza mradihuu ati tutasababisha watoto wasiende shule; well nani anayesababisha watoto wasiende shule leo? Tuache kujenga barabara, tuache kujenga mabwawa ya umeme, tuache kujenga ofisi mpya kwa sababu kwa kufanya hivyo tutasababisha watoto wasiende shule?
Lakinivile vile ni kana kwamba unataka tuone kuwa kuna choice mbili tu - ama kujenga daraja la Zenji au watoto kwenda shule - this is a fallacy of false dilemma. Kwanini tusifikirie kuweza kufanya vyote viwili na zaidi kwa kutumia resources tulizonazo? Kwa mfano, tukitenga dola bilioni 1 kwa mwaka kwa ajiili ya ujenzi wa daraja hilo kwa miaka minne ijayo (jumla ya dola bilioni 4) unafikiri hatutaweza? In comparison, mpango "wa maendeleo wa miaka mitano" uliopitishwa mwaka jana iliyopita ulikuwa unafikiria kutumia shilingi trilioni 42.6 katika miaka mitano (wastani wa trilioni 8.5 kwa mwaka!).
Sasa tayari tuna mpango wa trilioni 42.5 kwa miaka mitano, kumbuka bajeti yetu ya mwaka jana peke yake ilikuwa ni kama trilioni 13 tu! Sasa kutenga trilioni 1 kwa mwaka kwa ajili ya daraja hili ni tatizo la kusababisha shughuli nyingine zote nchini zisimame? kwamba tukitenga trilioni 1 kwa mwaka shule zitafungwa, polisi watakosa kazi, umeme hautalipwa n.k? Really? Kweli tunafikiria kwa vile tutakuwa na mradi huu mkubwa hatutaweza kweli kumudu mambo mengine?
Nadhani we are understimating our own potential to transform our beloved country and catapult it into beauty of greatness. I for one, I don't.