Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,256
- 44,597
- Thread starter
-
- #321
Baada ya uchaguzi mkuu wa 2005 na baada ya kuapishwa kuwa Rais, JK alikuja Washington DC. Mi sina mapenzi na viongozi lakini jinsi watanzania walivyokuwa na imani naye wakati hule ilibidi niende kwenye mkutano.
kwenye mkutano alisema kuwa Mwinyi alipoondoka aliacha kama dollar 800 Milioni katika reserve ya taifa. Na Mkapa aliacha kama dollar bilioni 2 katika reserve. Watu wakalipuka kwa vifijo. Na mimi bila kujijua nikajiunga kwenye frenzy ya kushangilia. Lakini akili ilipotulia ikabidi nigawe 2 Bilioni kwa population ya watanzania. Nikaona jamaa anasema upuuzi nikaondoka.
Thamani ya daraja mnalotaja ni dollar 1.4 Bilioni. Hii ni reserve ya Tanzania. Na kulikamilisha itabidi nchi iingie madeni makubwa.
Kama mafuta yamegunduliwa mradi huu unaweza kufanyika. Lakini kwa sasa itabidi ziwe ndoto.
Kakisiwa kenyewe kako wapi kakupokea gari 5000 - 10000 (future)? mnataka kwenda kukajaza kale kakisiwa ufisadi tu, uliokuwa exported sasa unatosha. Hatutaki daraja. Kama mnaogopa kuja kwa boti pandeni ndege, kama hamna uwezo msije.
Kawekeni daraja Pangani mpate shortcut ya kuja Dar mkitokea Arusha na mtapa watalii wengi wataoenda Saadani kutazama tembo wanaoogelea baharini.
It won't hurt if you just listen.
Mbona wa Finn wanaotufadhili kila mwaka hawajajenga daraja kutoka Helsinki mpaka Tallin? Hawana uwezo?
It won't hurt if you just listen.
Wazo zuri pesa za kulijenga zitapatikana tukianza kuchimba mafuta 'yetu'
sasa kushindwa kutoa hizo ameamua kudismiss the whole idea kwasababu hatujaweza kuweka hesabu zote na undani wa mpango mzima ili kujua kama unafaa au la!
Tuna VITU VINGI SANA VYA KUFANYA VIPAUMBELE, KWA SASA HATUHITAJI HILO DARAJA!.
Kiranga,Zakumi,Companero,Nyani Ngabu,jmushi1,
..nadhani Mwanakijiji is daring wa-Tanzania to think big and come up with an ambitious project itayatukwamua toka hapa tulipo.
..nakumbuka kusoma kuhusu jinsi gani mradi wa interstate highways za USA uliovyosaidia ktk kukuza biashara na uchumi wa Marekani.
..wa-Tanzania na sisi tunatakiwa tuibue mradi mkubwa ambao utasaidia kuinua sekta nyingine hapa nyumbani.
Nimeomba very basic general aspects za project. Mnajua kina cha channel nasehemu daraja litakapopita?
Kina cha maji si general kihivyo. Huwezi kujua bila kuzama na kupima. Sasa unategemea Mwanakijiji awe anajua vina vya sehemu zote ambazo daraja litapita?
Sasa kama hajui kina hawezi kujua challenge ya kujenga ikoje na teknolojia ya kutumia ni ipi, na kama hajui challenge hajui gharama, kama hajui gharama na anataka daraja lijengwe.... hatari!!
Maswali ya Kutafakari:
Je kuna uongozi wowote ndani ya CCM wenye mawazo ya namna hii au mwitikio wa kwanza 'hatuwezi?
Yeye katoa wazo. Wazo lake kubwa si uamuzi. Wewe unageuza wazo lake kuwa kama vile ndiyo uamuzi ambao umeshafanywa. Hapo ndipo unapokosea!
g. Bara nako kutanufaika sana na kufunguliwa kwa njia hii mpya.
Mzee Mwanakijiji, unaongelea kuhusu Tanzania hii ya CCM au ya kufikirika? Tanzania unayotaka ijenge muungano bridge!!!!! Imeshindwa kufinance service ya Kiwira Coal mine izalishe mw 200 wakati nchi inaupungufu wa mw 150, imeshindwa kuthubutu hata kuanza kwa upembuzi yakinifu wa stigglers Gorge inayohisiwa kuwa na uwezo wa mw 2000, Liganga imepata ufadhili wa China, Leo hii bidhaa zote za viwanda bei juu, lita ya maji ya kunywa inakimbizana bei na lita ya petrol. Tanzania ipi, hii inayoshindwa kuwalipa stahiki zao wastaafu wa EAC, hii inayochemsha kulipa malimbikizo ya mishahara ya walimu, hii yenye malumbano ya mikopo ya elimu ya juu. Naheshimu sana ideas zako, na hii idea ni one of the best, cause inawezekana kwa watu huru. But kwa hawa mental slaves, ambao wanaamini hata kutokomeza maralia tunahitaji wajomba, never till the end of time.Hivi mnafikiria huko China hakuna ufisadi? Au China viongozi wote ni wazuri na wazalendo?