Zanzibar kukodisha/kuuza visiwa vyake: Iko vipi?

Ile kauli ya kupigwa mnada ya masta Ndugai isije kuwa kweli tu jamani.

Ibakie tu kwamba vinakodishwa na tusiwape wageni ardhi yetu.
Kukodisha au kuuza ni kitu kilekile; mtu anakodi kwa miaka 100 ni vizazi vingapi hivyo vitapita bila kuwa na haki ya kupatumia mahali hapo? Neno kukodisha huwa ni neno laini linalotumiwa kuwapooza wale wanaohoji lakini madhara ya kukodidha kwa wa a chi ni yaleyale sawa na kuuza.
Hivi serikali ikitaka kutumua visiwa hivyo kwa mambo ya kijeshi labda miaka kumi ijayo jiulize itakuwaje ? Itabidi wavilipie kwa waliyemkodisha?
Huo ni mwanzo tu baadae wataingilia hata maeneo wanayoishi watu wa tabaka la chini kwa gia ya miji ya kisasa au kuboresha. Nakwambia hata national parks na game reserve zitamegwa na kuuzwa/ kukodishwa.

Hata haya madeni tunayofakamia huenda wadai wetu wakalazimisha wamegewe ardhi pale itakapodhihiri tumeshindwa kulipa.

Ukizingatia idadi ya watu inaongezeka kwa kasi maana yake wananchi watahitaji ardhi zaidi kwa kujenga, mashamba na makaburi lakini viongozi wamekazana kuwapa ardhi wageni!

Maisha ya watoto wetu na wajukuu yatakuwa magumu sana kutokana na maamuzi ya hovyo yanayofanywa sasa.
 
Kuanzia miaka hiyo mpk leo na hatujui mkataba ule upoje,wanyama wanapakiwa kwenye ndege huko huko kimya kimya,watanzania tunaendaga kufanya vibarua vya ujenzi mkuu,Pori la Loliondo ni nchi ya muarabu
Mtafanya nn watu wana haki ya kutokushtakiwa!
 
Nadhani sio uamuzi mbaya kukodisha visiwa. Kwani pesa inayopatikana inakwenda kuendeleza huduma za jamii. Mleta uzi kaja kisiasa zaidi.

Kaandika mada kiuchokozi ili kuigombanisha serikali ya Mwinyi na wote watakaosoma andiko lake.
 
Mkuu, kwa vile wewe unajua hilo suala vizuri sana, ni vyema sasa kumuelimisha huyo ndugu na wengine wengi ambao hili jambo ni mara ya kwanza kulisikia kwa kueleza ukweli wa jambo hilo kama walivyouliza:

1. Ni lini suala hilo lilijadiriwa? Je ni kikao cha Bunge/Baraza la Wawakilishi liliridhia?
2. Je nini matumizi ya pesa za mauzo ya hivyo visiwa
3. Jambo hilo kiujumla linafaida gani hasa kwa nchi?
 
Na je mgao wa pesa hizo zinaihusu pia Upande wa Tanganyika? Au pesa kutoka zenji ni inaihusu zenji peke yake?
 
nashauri Environment impact assement iwe kali TOR ziwe za kimataifa idara ya mazingira wawezeshwe usafir na vifaa vya kuvizungikia mara kwa mara kufanya tathmin
Naamini ushauri wako utafanyiwa kazi kikamilifu
 
Mbona nyie mmekodisha ardhi watu wachimbe madini wao wapo kimyaa
 
Tafadhali naomba kujua yafuatayo.
= Vinakodishwa kwa muda gani?
= Majenzi yatakayowekwa huko yatakuwa ya aina na ubora gani?
=Baada ya muda wa kukodi kuisha, majenzi yatakuwa ya nani?
= Suala la mazingira limezingatiwa kwa kiasi gani?
Mkuu,

Inategemea bid na bid. Inategemea na negotiations pia ila kuanzia ni miaka 33 na haitozidi miaka 99.

Majenzi yatakayokuweko huko yatakuwa ni hotel na zenye ubora. Kila kampuni itakuwa inapeleka proposal yake na serikali kupitia mamlaka zake itaamua kwa kutumia vigezo mbali mbali.

Baada ya muda kuisha wewe unaondoka na unaacha kila kitu. Ni kama vile mnavyoingia ubia hapo kariakoo mkuu.

Moja ya eneo ambalo serikali imekuwa serious sana kuhusiana na miradi hii ni kwenye mazingira.

Tutumieni muda wetu kuishauri serikali yetu.
 
We we waonyesha in msomi wa hali ya juu,unajibu maswali kisomi na kistaarabu.Napenda unavyojibu maswali,ningekuwa na kiwango cha elimu kama yako,ningeringa sana.
Mkuu mimi nimesoma kawaida tu.

Bado najifunza mengi mno!

Thanks for the compliment though, really appreciate it.
 
Nadhani sio uamuzi mbaya kukodisha visiwa. Kwani pesa inayopatikana inakwenda kuendeleza huduma za jamii. Mleta uzi kaja kisiasa zaidi.

Kaandika mada kiuchokozi ili kuigombanisha serikali ya Mwinyi na wote watakaosoma andiko lake.
Ni kweli mkuu,

Kamwe si uamuzi mbaya. Hebu fikiria, uwepo wa visiwa hivi tangu mwaka 1964 baada ya Mapinduzi ya Zanzibar mpaka Leo ni kwa namna na ukubwa gani umevifaidisha/umeifaidisha jamii ya Wazanzibari??

Leo kwa maamuzi haya Bora kabisa kutoka kwa serikali watu wanaenda kufaidika kwa asilimia kubwa kabisa. Watu watapata ajira na serikali itapata fedha za kufanyia miradi mengine ya maendeleo.

Nauunga mkono uamuzi wa serikali kwa asilimia 100.
 
Mimi nalijua hili suala kwa kiasi mkuu. Hofu yangu tu niliitanguliza mwanzo kabisa kwamba huu uzi usije ukatumika kupotosha jambo jema lililofanywa na serikali ya mainduzi ya Zanzibar.

Kiufupi kwa nijuavyo

1) ZIPA kama mamlaka imepewa ridhaa na serikali (wananchi) kushughulika na masuala ya uwekezaji ndani ya Zanzibar. Kule Zanzibar kuna hotel kama Neptune hotel, Serena hotel, Park Hyatt hotel, RUI hotel, Melia hotel, hizi zote zinamiliki ardi kubwa kubwa tu tena zaidi ya ukubwa wa baadhi ya visiwa na hizi hotel hiyo ardhi pia wamepewa kwa njia ya kukodishwa (lease agreement). Kwahiyo kwa mfumo na sheria za Zanzibar, ardhi yote iliyopo baharini inayotaka kufanyiwa uwekezaji itatolewa kwa mfumo wa lease tu, hata kama ni kwa wazawa. Sasa kwanini watu watake kupotosha linapokuja suala la KUKODISHA ardhi hizi ambazo utofauti ni kwamba ni visiwa tu. Mbona Kisiswa cha Chumbe kimekodishwa na kila kitu kipo sawa tu???

2) Matumizi ya fedha zitakazopatikana kutoka kwenye ukodishwaji wa hivyo visiwa ni kama matumizi ya fedha nyengine zote ambazo hotel za kawaida zinalipa through taxes and levies and rent fees. Zitaingia kwenye mapato ya taifa na kupangiwa matumizi through budgets, so hopefully zitakwenda kwenye elimu, afya, miundombinu, maji, umeme, etc. Hivi mkuu unafahamu kwamba as it is huduma za afya ni bure ndani ya Zanzibar?? Hivi mkuu unakifahamu kipimo cha CT- SCAN?? MRI je??? Hivi vipimo vinatolewa bure kabisa pasi na malipo yoyote na serikali ya Zanzibar. Hivi ni vipimo ghali sana kwenye sekta ya afya. Hivi vipimo nchi za ulaya havitolewi bure, naeleza haya kwa uzoefu.

3) Jambo hili kiujumla wake lina faida nyingi sana kwa taifa la Zanzibar and hopefully Tanzania kwa ujumla. Naomba niziainishe kwa uchache wake hapo chini:-
(a) Kuongezeka kwa ajira kwa wananchi wetu
(b) Kuongezeka kwa pato la taifa
(c) kuongezeka kwa fedha za kigeni
(d) Kuboreka kwa huduma mbali mbali za kijamii kama vile elimu, afya, maji, umeme.
(e) Serikali itaweza kuendelea na mipango ya utoaji wa makazi bora kwa wananchi wake kama vile ilivyo sasa kupitia nyumba za mapinduzi zilizotapakaa Zanzibar nzima.
(f) Hali za maisha ya wananchi wa Zanzibar zitaboreshwa kwa kiasi kikubwa.

Mkuu kiufui tu ninalotaka kusema hapa ni "YAJAYO NEEMA TUPU"

Tunamuomba Mungu ampe umri na afya njema rais wetu Mheshimiwa HUssein Mwinyi ili tufike tunapostahili kufika.
 
Mimi nadhani mgao wa pesa hizi ni kwa ajili ya Zanzibar tu. Ila najua kwamba kwa namna mbali mbali hata Tanzania itafaidika na suala hili.
Hivyo visiwa hiyo Project ni ya huko huko. Hata Huku Tanzania bado tuna nafasi kubwa zaidi ya kuwekeza Kwenye eneo letu la Bahari. Tuna visiwa Vingi Kwenye mwambao wa Bahari ukianzia Tanga Mpaka Mtwara wengi wetu tunavijua Mbudya,Bongoyo,Pole pole kipo Mafia.
 
Kwahiyo na Tanganyika wakodishe visiwa vyao
 
Kwahiyo na Tanganyika wakodishe visiwa vyao
Inawezekana mkuu,nadhani kama kisiwa Cha Pole Pole kule Mafia wale wamekodishiwa wale wazungu ili sio geni.

Moja ya rasilimali kubwa ni bahari ila tunashindwa kufanya full utilization of resources kuanzia visiwa,fukwe,uzalishaji wa umeme,maji safi, ujenzi wa Artificial Island. Nimefurahi kuona ZIPA wame cover kutafuta wawekezaji kila angle Ili watumie vyema bahari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…