Zanzibar kukodisha/kuuza visiwa vyake: Iko vipi?

Right on the spot.Ni ujinga kulalama kuhusu kisichokuhusu.
 
Umeuweka kwenye mtindo wa swali. Jibu ni kwamba, visiwa hivyo vinakodishwa na wala haviuzwi.
Vinakodishwa kwa muda gani? Hiyo ni ardhi ya Jamhuri ya Muungano Tanzania. Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania imeshirikishwaje katika ukodishaji huo na pato lake katika ukodishaji huo ni kiasi gani?
 
Mbwa ana tabia fulani huwa inanishangaza.Atafukuzwa mbuzi wasile majani na huku mbwa huyo huyo hali majani.
Ataishia kuyachunga tu mbuzi asile.Huku hafaidiki kwa kuyachunga.
 
Ukiwasikiliza Tanzania Bara na kupenda kujiona ni watoa maamuzi ya mambo ya Zanzibar mpaka utacheka. Etu "Serikali ya Jamhuri ya Muungano imeshirikishwaje".
 
Mbwa ana tabia fulani huwa inanishangaza.Atafukuzwa mbuzi wasile majani na huku mbwa huyo huyo hali majani.
Ataishia kuyachunga tu mbuzi asile.Huku hafaidiki kwa kuyachunga.
Hahahhaahahaha
 
Reactions: Tui
Ukiwasikiliza Tanzania Bara na kupenda kujiona ni watoa maamuzi ya mambo ya Zanzibar mpaka utacheka. Etu "Serikali ya Jamhuri ya Muungano imeshirikishwaje".
Maskini hajui kwamba hajui.Usimlaumu muelimishe.Anajifanya guardian.
 
Vinakodishwa kwa muda gani? Hiyo ni ardhi ya Jamhuri ya Muungano Tanzania. Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania imeshirikishwaje katika ukodishaji huo na pato lake katika ukodishaji huo ni kiasi gani?
Hili swali nimelijibu mara kadhaa, wewe utakuwa member wa mwisho kumjibu swali hili. Hivi visiwa na ardhi nyengine zitakuwa zinakodishwa kwa miaka 33 kwa kuanzia lakini inaweza ikaongezwa mpaka miaka 99 na si zaidi ya hapo, Naamini umenielewa hata kama uelewa wako ni mdogo.

Hiyo ni ardhi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?? Mkuu unatumia kilevi chochote?? Umeona wapi nchi ikawa na ardhi nchi nyengine?? Zanzibar ni nchi kamili na hiyo ni ardhi ya Zanzibar. Kwa vile ni ardhi yao hawana haja ya kumshirikisha yoyote yule, sio JMT wala Kenya wala Kuwait.

Kuhusu pato katika ukodishwaji itategemea kisiwa na kisiwa, lakini minimum amount for any investor to invest ni USD 2,500,000.00
 
Mtanzania nikiyapinga kuna dhambi ? Maana Tanzania ikiwemo Zanzibar ni urithi wetu sote. Wakinogewa tutapigwa mnada
 
Uchumi wa buluu ndio huo yakye, sijui mtavua wapi pweza.
 
Mtanzania nikiyapinga kuna dhambi ? Maana Tanzania ikiwemo Zanzibar ni urithi wetu sote. Wakinogewa tutapigwa mnada
Hakuna dhambi, hata Warundi wanaweza wakapinga tu hamna neno mkuu.

ila nakusihi usiyapinga maana utakuwa unapoteza muda wako tu.
 
Nimeelewa, na hapa kweli Katiba ya Jamhuri ya Muungano Tanzania inatakiwa itafisiriwe vizuri zaidi hasa kipengele cha mipaka ya Jamhuri hii na matumizi ya ardhi.
 
Mkuu unatumia kilevi chochote??
Hivi hapa anayetumia kilevi ni nani? Je unaijua Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania...
Katiba: 1. Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano.
Umeona wapi nchi ikawa na ardhi nchi nyengine?? Zanzibar ni nchi kamili na hiyo ni ardhi ya Zanzibar.
Je linapotajwa neno eneo, je ni pamoja na ardhi?
Katiba: 2.-(1) Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania inapakana nayo.
Kwa vile ni ardhi yao hawana haja ya kumshirikisha yoyote yule, sio JMT wala Kenya wala Kuwait.
Kweli wewe ndiye mlevi wa kutupwa, je unajua JMT ni mdudu gani?
Mimi nilidhani JMT ni pamoja na Zanzibar yenyewe, sasa Kenya na Kuwait zinaingiaje hapa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…