Zanzibar kupo ovyo sana. Kweli au nahitaji kueleweshwa?

Zanzibar iko kwenye miji inayotambulika kuwa urithi wa Dunia, Historia ya miaka ya 1700-1800 inaakisiwa na majengo yake mengi makuu kuu. Kuwa kwenye orodha ya urithi ni wazi kuwa magofu yote yatakuwa na thamani pale hivyo, hakuna ruksa ya kuingiza usasa pale.... Labda ujengwe mji mpya seheme nyingine kama ilivyo kwa miji mingi mikongwe ya nchi za bara ulaya.
 
Mtoa mada unamatatizo sio bure watu wenye wadhifa wao, utajiri na wafanyabiashara na mashuhuri wanaipenda Zanzibar ni sehemu moja iko kipekee kabisa kama una hela za kutumia nenda Zanzibar Tembelea stone town na uinjoy hotel za kifahari.

inasemekana Zanzibar ni sehemu pekee ukienda msikitini unaweza kuonana na waziri, wabunge , Rpc na ukapiga swaga nao bila shida yoyote ufahari, majivuno hawana wanaishi maisha yakawaida kabisa.
 
Ila Serikali yao inawapenda sana, huduma zote zinazotolewa na Serikali kama Elimu,Afya Umeme,Maji na n.k. aidha ni bure ama kwa gharama ya chini kabisa, hakuna magereza, badala yake kuna vyuo vya Mafunzo na humo ndani ya hivyo vyuo kunapatikana michezo ya kila aina, "mpira wa miguu,basketball,netball,Keram, draft na michezo mingine tele na anaemaliza kifungo chake kuna pesa ya kwenda kuanzia maisha huwa anapewa. Wenyewe wanaita "mshahara"yaani kipindi chote unachokaa jela unakuwa unalipwa.
 
Kumbe Tz bara tunanyonywa hivi daah..

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ndio unawaza chini..nani alikwambia lodge zinatengeezwa kwa ajili ya wazinzi..?hizo ni nyumba kwa ajili ya wageni.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe unawaza chini, umefikia kwa mwenyeji lodge gesti ya nini? Acheni ujinga wa kujiona mnajua sana maisha kwa kupenda luxury! Na maisha ya dunia si chochote ila ni starehe ya ubatili!
 
Wewe unawaza chini, umefikia kwa mwenyeji lodge gesti ya nini? Acheni ujinga wa kujiona mnajua sana maisha kwa kupenda luxury! Na maisha ya dunia si chochote ila ni starehe ya ubatili!
Kwamfano mtu anakuja zanzibar kwaajili ya biashara ama utalii na hana wenyeji..ulitaka afikie kwako ama?lodge muhimu sana.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee we mtu punguza fiksi kidogo basi... dah!
 
Kama Bagamoyo sio?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…