Jana nikiwa sehemu fulani nilisikia baadhi ya wasomi wakijadili mambo kadhaa hasa wakiitaja nchi iitwayo Zanzibar.
Kwa walio na ufahamu vizuri nitaomba msaada hapa. Kwa uelewa wangu, ili sehemu ya ardhi inayokaliwa na watu iitwe nchi(state), ni lazime pawepo na mambo yafuatayo:
1. Mipaka kamili inayotambulika kimataifa
2. Serikali
3. Watu na makazi
4. Iwe na uwezo wa kuingia makubaliano na nchi nyingine bila kuingiliwa au kuhitaji ruhusa kutoka sehemu nyingine.
Ikiwa sehemu inajitosheleza kwa mambo yote hayo manne basi, huitwa na kutambulika kama nchi.
Lakini sehemu hiyo (nchi) inaweza kupoteza sifa ya kuitwa nchi na jumuia za kimataifa kama:
1. Itaungana na nchi nyingine kutengeneza nchi au taifa moja
2. Itakubali kutawaliwa na nchi nyingine
3. Mipaka yake itamezwa na nchi nyingine
4. Itagawanyika katika sehemu ndogondogo zenye mamlaka kamili
Je, baada ya Zanzibar kuungana na Tanganyika na kuunda serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bado Zanzibar inatambulika kama nchi? ni vigezo gani huifanya zanzibar kuitwa nchi?